Tuesday, March 1, 2011

ANCELOTTI NA COLYE WAMGOMBANIA STURRIDGE.

LONDON, England.
MSHAMBULIAJI wa kimataifa toka nchini Uingereza Daniel Andre "Danny" Sturridge mwishoni mwa msimu huu huenda akazusha vita kubwa kati ya meneja wa klabu ya Bolton Wanderers Owen Coyle dhidi ya meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti.

Vita inayohofiwa huenda ikasababishwa na mshambuliaji huyo ni harakati za kusajiliwa moja kwa moja ndani ya klabu ya Bolton Wanderers ambayo kwa sasa anaitumikia kwa mkopo baada ya kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza cha Chelsea ambacho kimesheheni washambuliaji wengi na wazuri.

Tayari Coyle ameshatangaza kuwa tayari kutuma ofa huko Stamford Bridge ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo moja kwa moja baada ya kuridhishwa na kiwango chake toka alipomsajili kwa mkopo mwezi januari mwaka huu.

Alisema anafurahishwa na maendeleo ya Sturridge ambae tayari ameshaifungia klabu hiyo mabao manne ndani ya michezo minne aliyocheza.

Kwa upande wa Ancelotti nae ameshatoa msimamo wake wa kutokua tayari kumuuza mshambuliaji huyo kufuatia kuwepo kwenye mipango yake ya baadae mara tu atakapo maliza mkataba wake wa mkopo huko Reebok Stadium.

No comments:

Post a Comment