MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Italia Marco Borriello amewataka radhi mashabiki wa klabu ya AS Roma baada ya kukosa mkwaju wa penati kwenye mchezo wa pili wa hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Shakter Donetsk usiku wa kuamkia jana.
Borriello imemlazimu kufanya hivyo baada ya klabu ya AS Roma kuondolewa kwenye michuano hiyo kwa jumla ya mabao sita kwa mawili dhidi ya Shakter Donetsk ambao wametinga kwenye hatua ya robo fainali.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alikosa mkwaju wa penati katika dakika ya 28 kipindi cha kwanza huku AS Roma wakiwa tayari wameshafungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya wapinzani wao.
Alisema hana budi kusamehewa kwa kosa alilolifanya na amekiri kitendo hicho kimewakera mno mashabiki wa AS Roma ambao hawakutegemea kama angekosa nafasi hiyo pekee ambayo huenda ingewarejesha kwenye mchezo na kuibuka na ushindi wakiwa ugenini.
Hata hivyo mazingira yaliyokuwepo kwenye kikosi cha AS Roma bado yalikua yakimpa nafasi Borriello kupiga mkwaju huo wa penati kufutia mshambuliaji Francesco Totti aliezoeleka kufanya hivyo kuwa benchi sambamba na David Pizarro ambae pia hutumika kama mbadala wa kutumia nafasi kama hizo zinapojitokeza mchezoni.
No comments:
Post a Comment