Tuesday, March 1, 2011

HUGHES AMJIA JUU MANCINI.

Mark Hughes

LONDON, England
KOCHA wa klabu ya Fulham Mark Hughes amesema hakufurahishwa na kitendo alichofanyiwa na Kocha Man city Roberto Mancini mara baada ya mchezo wa jana kumalizika huko City Of Manchester.

Hughes amesema kitendo cha kocha wa Man city kumpa mkono huku akishindwa kumtazama usoni kilimchukiza hadi kufikia hatua ya kumuona ni mtu mbinafsi na asiyependa kumuona machoni mwake.

Amesema si mara ya kwanza kwa kocha huyo kufanya kitendo hicho kwani hata alipozulu Craven Cottage alifanya hivyo mara baada ya kipyenga cha mwisho kupulizwa.

Hughes ambae jana alirejea City of Manchester akiwa kama kocha wa klabu pinzani ameongeza kwamba Mancini amekua na tabia za dharau ambazo haziwezi kuvumiliwa na yoyote yule.

Katika hatua nyingine kocha huyo wa kimataifa toka nchini Wales ameonyesha kufurahishwa na matokeo ya sare yaliyopatikana katika mchezo huo ambao ulishuhudia wakienda mapumziko wakiwa nyuma kwa idadi ya bao moja kwa sifuri lililofungwa na Mario Balotelli.

Roberto Mancini.
Hughes amesema alitumia muda wa mapumziko vyema kwa kuwaasa wachezaji wake kucheza kwa ukakamavu na juhudi ambazo hata hivyo zilisawaidia na mwisho wa dakika tisini walijikuta wanaondoka uwanjani hapo wakigawana pointi na wenyeji wao kufuatia bao lililofungwa na Damian Duff.

Mancini baada ya matokeo hayo ya bao moja kwa moja ametoa kisingizo cha uchovu uwanaowakabili wachezaji wake kutokana na ratiba ya ligi kuwabana kwa hivi sasa.

Alisema ni vigumu kwa mchezaji wa kawaida kucheza kila baada ya siku tatu hivyo inamlazimu kuwapumzisha baadhi ya wachezaji wake muhimu ambao anaamini endapo wangejumuika na baadhi ya wachezaji wengine katika mchezo huo walikua na kila sababu ya kuzibakisha point tatu nyumbani.

No comments:

Post a Comment