KOCHA wa klabu ya Aston Villa Gerard Houllier usiku wa kuamkia hii leo alilazimika kukimbizwa hospitalini huko mjini Birmingham kufuatia hali yake ya kiafya kutokua nzuri.
Uongozi wa klabu ya Aston Villa uliowakilishwa na mtendaji mkuu Paul Faulkner mbele ya vyombo vya habari umetoa taarifa hizo huku ukisisitiza kwamba hali ya meneja huyo wa kimataifa toka nchini Ufaransa ni shwari na wala hakuna shaka na hii ni kwa mujibu wa madaktari wanao mshughulikia.
Paul Faulkner alisema mapema hii leo alikwenda hospitali kumjulia hali Gerard Houllier ambapo amemkuta katika hali nzuri na yenye kuridhisha hivyo wanamichezo pamoja na mashabiki wa klabu ya Aston Villa wametakiwa kuwa watulivu.
Hata hivyo Paul Faulkner amesema bado meneja huyo mwenye umri wa miaka 63 ataendelea kupatia matibabu kwa siku kadhaa hatua ambayo itamkosesha mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo kikosi chake kitakua nyumbani Villa Park kikiwakaribisha Stoke City.
Kutokana na hali hiyo meneja msaidizi Gary McAllister, amepewa jukumu la kukisimamia kikosi cha Aston Villa ambacho atakiongoza katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili akiwa kama mkuu wa benchi la ufundi.
No comments:
Post a Comment