Wednesday, April 27, 2011

BREAKING NEWS: BAFANA BAFANA KUJIPIMA NGUVU NA TAIFA STARS.

Wachezaji wa Bafana Bafana wakiwa katika mazoezi.

JOHANESBURG, South Afrika
SHIRIKISHO la Soka la Afrika Kusini (Safa) na wawakilishi kutoka Tanzania wamefikia mkubaliano jioni hii juu ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki baina ya timu za mataifa hayo utakaochezwa katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Mei 14 mwaka huu.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) Pitso Mosimane alithibitisha kuwa ameletewa taarifa kutoka Safa kuhusiana na mchezo huo ambapo atatangaza kikosi kitakachoivaa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika tarehe hiyo waliyokubaliana.

"Naishukuru Safa na PSL kwa ushikiriano wanaompa kuhusu mipango yetu," alisema Mosimane. "Tuna mchezo mgumu dhidi ya Misri katika kutafuta tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika Juni 3, hivyo mchezo huu utakuwa ni mzuri kwa sisi kujipima nguvu.

"Naweza kusema kuwa kama tukishinda mchezo huu tutakuwa tumejiweka katika nafasi nzuri ya kukata tiketi ya kucheza michuano ya Mataifa ya Afrika 2012, Equatorial na Gabon. Hivyo mchezo huu tutakaocheza Tanzania utakuwa ni muhimu kwa maandalizi ya mchezo wetu huko Misri na nitateua kikosi imara kwa ajili ya mchezo huo."

Nae wakala anayetambulika na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Damas Ndumbaro alithibisha kuwa tayari wamefikia makubaliano na wote Rais wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) Leodgar Tenga na Safa CEO Pinky Lehoko kwa ajili ya mchezo huo kwa tarehe iliyotajwa hapo juu na tayari wamepeleka taarifa FIFA.

Rais wa Safa Kirsten Nematandani pia alithibisha juu ya kuwapo kwa mchezo huo kwa tarehe hiyo. Ingawa sio tarehe ya FIFA, lakini Ligi Kuu nchini itakuwa imesimama kufuatia mchezo wa nusu fainali wa Kombe la Nedbank hivyo wameona ni wakati muafaka kwa timu ya Taifa kupata mchezo wa kujipima nguvu.

No comments:

Post a Comment