Friday, April 29, 2011

HAMMAM KUZIWEZESHA NCHI ZA AFRIKA.

Blatter (Kulia) akiwa na mpinzani wake Hamman (kushoto).

NCHI za bara la Afrika huenda zikafaidia zaidi katika utaratibu wa kuhakikisha soka la barani humo linakua endapo wajumbe wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) watamchagua Mohamed Bin Hammam kuwa Rais wa shirikisho hilo katika uchaguzi utakaofanyika June mosi mjini Zurich, Uswiz.

Mohamed Bin Hammam amepania kuendeleza kasumba ya kufanya mapinduzi ya maendeleo ya soka barani Afrika huku akiahidi kuongeza fedha ambazo hutumwa kila mwaka katika nchi za bara hilo kutoa dola za kimarekani 250,000 hadi 500,000.

Mpinzani huyo wa Rais wa sasa wa FIFA Sepp Blatter ametoa ahadi ya kuongeza fedha hizo alipofanya ziara barani Afrika katika nchi za Equatorial Guinea, Chad, Jamhuri ya Afrika kati, Rwanda, Gabon pamoja na Cameroon.

Mohamed Bin Hammam ambae pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Barani Asia ameahidi kuongeza fedha za mradi wa GOAL ambao husimamiwa na FIFA kutoa dola za kimarekani 400,000 hadi dola za kimarekani million moja.

Baada ya kumaliza ziara ya kufanya kampeni barani Afrika Mohamed Bin Hammam hii leo alikua barani ulaya katika nchi Uingereza kwa ajili ya harakati hizo za kuomba kura na ameelezea furaha yake ya kukutana na viongozi wa soka wa nchi hiyo.

Baada ya kuzulu nchini Uingereza Mohamed Bin Hammam anatarajia kufunga safari hadi katika barala la Amerika ya kusini ambapo huko atahudhuria mkutano mkuu wa shirikisho la soka la ukanda huo utakaofanyika nchini Paraguay.

No comments:

Post a Comment