Sunday, May 1, 2011

FIFA YATOA RATIBA YA KOMBE LA DUNIA LA UNDER 20.

GENEVE, Switzerland.
WAKATI fainali za mataifa ya bara la Afrika chini ya umri wa miaka 20 zikitarajiwa kufikia tamati mwishoni mwa juma hili huko nchini Afrika kusini kwa timu ya taifa ya Nigeria kupambana vikali na Cameroon, Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limepanga makundi pamoja na kutoa ratiba ya fainali za Kombe la Dunia kwa vijana zitakazofanyika nchini Colombia July 29 mwaka huu.

Ratiba ya fainali hizo yaonyesha kwamba timu ya taifa ya Misri ambayo jana imeshindwa kujihakikishai nafasi ya kucheza hatua ya fainali za mataifa ya bara la Afrika baada ya kufungwa na Cameroon kwa changamoto ya mikwaju ya penati itafungua fainali hizo za dunia kwa kucheza na timu ya taifa ya Brazil.

Timu ya taifa ya Misri iliyopangwa katika kundi la tano mara baada ya mchezo wa Brazil itarejea tena uwanjani kupambana na Panama na kisha itamaliza michezo ya hatua ya makundi kwa kucheza na Austria.

Nchi nyingine ya barani Afrika ni Mali ambayo imepangwa katika kundi la kwanza na itaanza kamepni ya kuwania ubingwa wa fainali hizo kwa kucheza na Korea kusini na baada ya hapo watakiputa na wenyeji Colombia na kisha watamaliza na Ufaransa.

Cameroon wao wamepangwa katika kundi la pili ambapo katika mchezo wa kwanza watacheza na mshiriki kutoka Oceania ambae bado hajapatikana, na mchezo wa pili utakuwa dhidi ya Ureno na kisha watamaliza na Uruguay.

Nigeria, wapo katika kundi la nne ambapo mchezo wao wa kwanza utawakutanisha na Guatemala kisha watakutana na Croatia na mwishowe watamaliza na Saudi Arabia.
Draw for the Under-20 World Cup:

Group A (Bogota/Cali):
Colombia
France
Mali
South Korea

Group B (Cali/Bogota):
Portugal
Uruguay
Cameroon
Champion of Oceania (TBD)

Group C (Manizales/Pereira):
Australia
Ecuador
Costa Rica
Spain

Group D (Armenia/Pereira):
Croatia
Saudi Arabia
Nigeria
Guatemala

Group E (Barranquilla/Cartagena):
Brazil
Egypt
Austria
Panama

Group F (Medellin/Cartagena):
Argentina
Mexico
England
North Korea

No comments:

Post a Comment