WAZIRI Mkuu wa Italia ambae pia ni mmiliki wa klabu ya AC Milan Silvio Berlusconi amesema naamini kiungo wa kimataifa toka nchini uholanzi pamoja na klabu hiyo ya mjini Milan Clarence Seedorf bado ana uwezo wa kucheza soka kwa kipindi kirefu kijacho.
Berlusconi alisema kiungo huyo ambae kwa sasa ana umri wa miaka 35 bado anaonekana mwenye nguvu na imani yake yamtuma kwamba ana uwezo mkubwa wa kufikisha hata miaka 52 akiwa uwanjani na akaonyesha uwezo mkubwa na kijana anaechipukia katika mchezo wa soka.
Alisema ni vigumu kuamini lakini kwa upande wake anaamini hivyo kutokana na kuwa karibu na Clarence Seedorf aliejiunga na Ac Milan mwaka 2002 akitikea Inter Milan.
Clarence Seedorf toka alipoanza kusukuma soka katika klabu hiyo tayari ameshacheza michezo 278 na kupachika mabao 44 huku akiwa miongoni mwa wachezaji walioisaidia AC Milan kutwaa ubingwa wa michuano ya;’
• Kombe la ligi nchini Italia *Serie A*: 2003–04
• Kombe la nchini Italia *Coppa Italia*: 2002–03
• Supercoppa Italiana: 2004
• Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya 2003, 2007
• UEFA Super Cup: 2003, 2007
• Klabu bingwa duniani *FIFA Club World Cup*: 2007
No comments:
Post a Comment