MADRID, Hispania
SHIRIKISHO la Soka Barani Ulaya UEFA limefungua milango ya kufanya uchunguzi wa vioja vilivyojitokeza katika mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali kati ya mahasimu wawili wa nchini Hispania Real Madrid dhidi ya FC Barcelona.
UEFA wamefungua milango ya kufanya uchunguzi huku wakiyalenga matukio yaliyosababisha vurugu na kuelekea wahusika wengine kuzungumza maneno ya kashfa dhidi ya klabu pinzani ama mtu wa klabu pinzani.
• Tukio la kwanza litakalofanyiwa uchunguzi ni kuonyeshwa kadi nyekundu kwa Pepe.
• Tukio la pili ni kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kipa wa akiba wa klabu ya Barcelona Jose Pinto.
• Tukio la tatu ni kuondolewa kwa meneja wa klabu ya Real Madrid Madrid Jose Mourinho katika benchi na kutakiwa kukaa jukwaani.
• Tukio la tatu ni maneno ya kashfa yaliyotolewa na meneja wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo.
Wakati huo huo Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger ambae ni muhanga wa kucheza na Barcelona huku kikosi chake kikisaliwa na wachezaji kumi ambapo hali hiyo imeshamtokea mara mbili amesema hawezi kuzungumza lolote zaidi ya kubaki na mawazo yake kichwani lakini akaipinga kauli iliyotolewa na meneja wa klabu ya Real Madrid Jose Mourinho.
Alisema kauli ya Mourinho ya kudai fc Barcelona wanapendelewa haiafiki hata kidogo na amebainisha wazi kwamba lazima watu wakubali na kutambua kwamba klabu hiyo ya Catalan ina uwezo mkubwa wa kusukuma kandanda.
Kama itakumbukwa vyema Arsene Wenger alikishuhudia kikosi chake kikitota mbele ya Barcelona huku kikiwa pungufu katika mchezo wa hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa mwaka 2006 kufuatia kipa Jens Lehman kuonyeshwa kadi nyekundu, na kwa mara pili kikosi chake kikakutwa na mkasa huo katika hatua ya 16 bora ya michuano hiyo msimu huu baada ya Robin Van Parsie kuonyeshwa kadi nyekundu.
Nae Carlo Ancelotti meneja wa klabu bingwa nchini Uingereza Chelsea ambayo pia imeshakumbwa na tatizo la kumaliza mchezo dhidi ya Barcelona huku kikosi chake kikiwa pungufu amesema anaamini kabisa Jose Mourinho alikua amechukizwa na vitendo vilivyojitokeza uwanjani na hatua hiyo ilimpelekea kusema maneno mazito mbele ya waandishi wa habari.
Lakini pamoja na kusema hayo bado Ancelotti akawataka mashabiki ulimwenguni kote kuelewa kwamba waamuzi nao huwa wanafanya makosa bila kutegemea hivyo wanatakiwa kuchukuliwa kama binadamu wengine.
Wakati huo huo Real Madrid pamoja na FC Barcelona wanategemea kuwasilisha malalamiko yao ndani ya shirikisho la soka barani ulaya UEFA juu ya kile kilichojitokeza katika mchezo wao uliochezwa usiku wa kuamkia jana huko Estadio Stantiago bernabeu.
Uongozi wa klabu ya Real Madrid unafikiria kuwasilisha malalamiko yao ambayo wameyaelekeza moja kwa moja kwa muamuzi pamoja na kwa wapinzani wao ambapo wamedai walifanya makusudi kumshurutisha muamuzi huyo kutoka nchini Ujerumani ili aweze kutoa adhabu kwa wachezaji wa The Merenguez.
Nao uongozi wa klabu ya Barcelona unatarajia kuwasilisha malalamiko yake kufuatia shutuma nzito zilizotolewa na meneja wa klabu ay Real Madrid Jose Mourinho ambazo zilidai kwamba klabu hiyo ya catalan imekua ikibebwa kwa makusudi.
Hata hivyo katika suala hilo uongozi wa klabu ya Real Madrid umeahidi kuwa sambamba na Jose Mourinho kwa lolote litakalomkabili kutokana na malalamiko hayo.
No comments:
Post a Comment