MSHAMBULIAJI nguli wa zamani kutoka Brazil Pele anaamini kuwa bado yeye ndio mchezaji bora aliyepata kutokea pamoja na ujio wa wachezaji wa sasa Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Mchezaji huyo wa zamani wa Santos aliweka rekodi ya kipekee ya kufunga mabao 1,281 katika michezo 1363 aliyocheza katika kipindi cha miaka 23 aliyocheza soka.
Pele alishinda Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza akiwa na Brazil mwaka 1958 akiwa na umri wa miaka 17, na aliendelea kuchukua makombe mengine ya dunia mawili akiwa na timu hiyo ya Amerika Kusini.
Katika miaka ya karibuni Messi na Ronaldo wameonekana kuiteka dunia kwa vipaji walivyonavyo wanapokuwa uwanjani lakini Pele anaamini hakuna hata mmoja aliyemfikia.
"Kwangu mimi Pele bado ni bora. Hakuna yoyote aliyefanya zaidi ya Pele. Ni mchezaji pekee aliyeshinda ubingwa wa dunia akiwa na miaka 17, kushinda vikombe vitatu vya Kombe la Dunia na kufunga zaidi ya magoli 1,208," alikaririwa Pele akiongea na Mwandishi mmoja wa Marekani.
No comments:
Post a Comment