BEKI wa kimataifa kutoka nchini Ubelgiji Thomas Vermaelen hii leo anarajea uwanjani kucheza mchezo wa wachezaji wa akiba kati ya Arsenal dhidi ya Manchester United.
Vermaelen anarejea uwanjani hii leo baada ya kupona maumivu ya kisigino yaliyomsumbua kwa muda wa miezi minane iliyopita hatua ambayo ilipelekea kufanyiwa upasuaji mwezi januari mwaka huu.
Hata hivyo kurejea kwa beki huyo mwenye umri wa miaka 25 katika mchezo wa wachezaji wa akiba, bado kunahisiwa huenda kukamfanya meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger kupata ushawishi wa kumtumia kwenye michezo ya ligi kabla ya msimu huu kumalizika.
No comments:
Post a Comment