Friday, April 29, 2011

TEVEZ, ETHERINGTON KUIWAHI FAINALI FA.

LONDON, England
WINGA wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ya Stoke City Matthew Etherington ameripotiwa huenda akauwahi mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la chama cha soka nchini humo FA dhidi ya Man city utakaochezwa katika uwanja wa Wembley May 14 mwaka huu.

Kocha wa klabu Stoke City Tony Pulis alisema Matthew Etheringto, amefanyiwa vipimo na imeonekana amaumia sehemu ya nyama za paja zinazoshikilia nyuma ya goti hivyo madaktari wamemuahidi kufanya kila linalowezekana ili kuweza kuuwahi mchezo huo dhidi ya Man City.

Winga huyo mwenye umri wa miaka 29, alipatwa na maumivu hayo ya nyama za paja katika mchezo wa ligi uliochezwa usiku wa kuamkia jana dhidi ya Walves ambao walikubalia kisago cha mabao matatu kwa sifuri.

Wakati huo huo mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina pamoja na klabu ya Man City Carlos Tevez nae ameripotiwa huenda akauwahi mchezo huo wa hatua ya fainali kutokana na kuendelea kupata matibabu mazuri.

Carlos Tevez alipatwa na maumivu ya nyama za paja katika mchezo wa ligi dhidi ya Liverpool ambapo katika mchezo huo majogoo wa jiji waliibuka na ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.

No comments:

Post a Comment