Tuesday, May 31, 2011

UTETEZI WA WARNER WAITIA MATATIZONI QATAR.

ZURICH, Uswis
MAKAMU wa Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Jack Warner, ametoboa siri kwa kuonyesha hadharani barua pepe ambayo inadai Mohamed Bin Hammam alinunua kura ambazo ziliiwezesha nchi yake ya Qatar kushinda nafasi ya kuandaa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2022.

Jack Warner amefanya hivyo kwa kuwaonyesha waandishi wa habari barua hiyo ikiwa ni sehemu ya kutaka kujitetea na tatizo linalomkabili kwa sasa ambalo limepelekea kusimamishwa kwa muda na kamati ya maadili iliyokutana jana na kuafiki maamuzi hayo.Kiongozi huyo amedai kwamba bado kuna baadhi ya watu ndani ya FIFA wanahusika kuchukua mlungula na si yeye pekee yake huku akimuhusisha katibu mkuu Jerome Valcke ambae anadaiwa alipata taarifa hizo kupitia barua pepe ambayo ilionyesha majina ya Josep Sepp Blatter pamoja na Mohamed Bin Hammam kwa kifupi.

Katika barua hiyo ujumbe wa Valcke unasomeka kwamba Bin Hammam anadhani unaweza kuinunua FIFA kama alivyonunua fainali za Kombe la Dunia.

Hata hivyo katibu mkuu wa FIFA Jerome Valcke amekiri alipokea barua hiyo kwa njia ya mtandao wa Internet kutoka kwa Jack Warner, ambae alikua anahoji kigezo kilichotumika kumruhusu Bin Hammam kuwania nafasi ya uraisi ili hali anahusika na uchafu huo alioufanya?

Katika utetezi wake mbele ya waandishi wa habari Valcke ameeleza kwamba barua hiyo ilikua ni ya kibinafsi na si ya kiofisi na bado Jack Warner alikuwa amehusika katika sehemu ya barua hiyo.
Valcke pia amekanusha taarifa za kuishurutisha kamati ya maadili ya FIFA ambayo imemsimamisha kwa muda Jack Warner pamoja na na Bin Hammam kufuatia tuhuma zinazowakabili za kutoa mlungula kwa wajumbe wa CONCACAF kwa ajili ya kumpgia kura Bin Hammam katika uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika June mosi mjini Zurich nchini Uswiz.

Maamuzi ya kusimamishwa kwa watuhumiwa hao wawili yalitangazwa jana na makamu mwenyekiti wa kamati ya maadili ya FIFA Petrus Damaseb.

Katika hatua nyingine Jopes Sepp Blatter raisi wa sasa wa FIFA amewashiwa taa za kijani kwa ajili ya kuendelea na kampeni zake za kutetea kiti cha uraisi baada ya kuonekana hana kesi ya kujibu katika sakata hilo.

Blatter nae alihojiwa kuhusiana na sakata hilo ambapo inadaiwa alifahamu kilichokua kikiendelea kati ya wajumbe wa Caribian dhidi ya Mohamed Bin Hammam na Jack Warner lakini alikaa kimya.
Kufuatia hatua hiyo Katibu mkuu wa FIFA Jorome Valke ametangaza utaratibu wa kuendelea kwa uchaguzi mkuu kama ulivyokua umepangwa siku za nyuma.

Na taarifa tulizozipata hivi punde zinaeleza kwamba raisi wa shirikisho la soka barani Asia Mohamed bin Hammam anatarajia kukata rufaa kufuati maamuzi ya kusimamishwa kwake na kamati ya maadili ya shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA.

Mohamed bin Hammam anatarajiwa kuwasilisha rufaa yake katika kamati ya rufaa ya FIFA siku yoyote ndani ya juma hili huku akiamini kwamba bado ana haki kufuatia tuhuma zinazomkabili za utoaji wa rushwa ambao umetajwa kufanyika katika kampeni zake huko Amerika ya kati.

Wakati huo huo Shirikisho la Soka nchini Qatar limekanusha vikali taarifa zilizotolewa makamu wa raisi wa FIFA aliesimamishwa Jack Warner ambazo zimedai kwamba nchi hiyo ilimtumia mlungula ili iweze kuibuka kidedea katika kinyang’anyiro cha kuwa mwenyeji wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2022.

Monday, May 30, 2011

MAELFU YA WAKAZI WA BARCELONA WAMPOKEA MWALI WAO.

Shujaa wa Barcelona Lionel Messi akiingiwa katika Uwanja wa Camp Nou na Kombe la Klabu ya Ulaya walilonyakua katika Uwanja wa Wembley Uingereza juzi usiku.

Timu ya Barcelona ikipita katika basi la wazi katika mitaa ya mji wa Barcelona mara baada ya kuwasili.

Wafanyakazi na wachezaji wa Barcelonja wakiwa katika picha ya pamoja.

Umati wa watu wapatao 94,000 ambao walihudhuria katika mapokezi ya timu yao katika Uwanja wa Camp Nou.

Kocha wa Barcelona Pep Guardiola akiwasalimia mashabiki.

Nderemo na vifijo vikiendelea uwanjani.

Saturday, May 28, 2011

BARCELONA 3 MANCHESTER UNITED 1: KWA MARA NYINGINE BARCA YAIBURUZA MAN UNITED CHAMPIONS LEAGUE.

Kutoka kushoto Victor Valdes, Xavi na Erick Abidal wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa Kombe la Klabu Bingwa ya Ulaya usiku huu katika Uwanja wa Wembley, Uingereza.

Wachezaji wa Barcelona wakishangilia bao lao la kwanza dhidi ya Manchester United.

Mshambuliaji wa Barcelona David Villa akipigilia  msumari wa mwisho katika jeneza la Man United bao ambalo lilizamisha ndoto za timu hiyo kunyakua ubingwa huo.

Mshambualiaji Leonel Messi akipiga shuti kali ambalo lilimshinda golikipa wa Man United Edwin Van de Sar na kutinga wavuni kuandika bao la pili la timu hiyo.

Messi akishangilia bao lake huku mabeki wa Man United wakiwa wamepigwa na butwaa.

Mshambualiaji wa Man United Wayne Rooney akifunga bao la kufutia machozi.

Van de Sar akiangalia mpira ukitumbukia nyavuni.

Mshambuliaji wa Man United Chicharito ambaye hakung'aa usiku wa leo akipambana na Valdes katika moja ya heka heka za mchezo huo.

Kocha wa Manchester United akiwapongeza wachezaji wa Barcelona kwa ushindi wao.

Nyota wa mchezo Xavi akiwa katika moja ya heka heka ambazo zilizaa bao la kwanza katika mchezo huo.

Rooney na Ryan Giggs wakiwa hawaamini kulipoteza kombe hilo kwa mara ya pili kwa Barcelona tena wakiwa nyumbani, mara nyingine ilikuwa ni fainali za mwaka 2009 zilizofanyika Rome, Italia.

Thursday, May 26, 2011

Which of these boys grew into the world's best footballer and is coming to torment United at Wembley?

Pichani waliosimama wa pili kutoka kushoto anaonekana kijana mdogo ambaye amevaa fulana ambayo haimtoshi, nani angeweza kudhania kwamba angukuja kuwa mchezaji bora duniani? kijana huyo ndio Messi hapo alipokuwa na miaka 6.  

Leonel Messi wa hivi leo ambaye ndiye mchezaji Bora wa Dunia.

Wednesday, May 25, 2011

ETO'O AIPIGIA CHAPUO BARCELONA KUNYAKUA CHAMPIONS LEAGUE.

MILAN, Italia
MSHAMBULIAJI wa kimataifa kutoka nchini Cameroon, Samuel Eto'o anamatarajio kuwa timu yake ya zamani Barcelona itaifunga Manchester United kkatika mchezo wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya itayochezwa Jumamosi hii kkatika Uwanja wa Wembley.

Eto'o ambaye pia nachezea klabu ya Inter Milan sio mgeni sana na kombe hilo haswa ukizingatia kuwa ameshawahi kushinda kombe hilo mara mbili akiwa na Barca na moja akiwa na Inter.

Alishinda moja ya magoli dhidi ya Man United katika fainali zilizofanyika Rome, Italia 2009, na anatarajia kuwa historia inaweza kujirudia tena kwa timu yake hiyo ya zamani kunyakuwa kombe hilo tena.

"Nikitakuwa katika fainali hiyo nikiwa na imani kwasababu nina marafiki wazuri ambao watakuwa wanacheza hivyo moyo wangu utakuwa kwao," alisema Eto'o akihojiwa na mtandao wa UEFA.

"Moja kwa moja naipigia chapuo Barcelona kushinda. Lakini huwezi kujua kitu gani kitatokea. Wote Barcelona na Manchester United wana vikosi bora zaidi ukilinganisha na mwaka 2009. Naamini itakuwa ni fainali za kuvutia."

Tuesday, May 24, 2011

BAYERN YAONEKANA KUSHINDWA DAU LA NEUER.

MUNICH, Ujerumani
KIPA wa kimataifa toka nchini Ujerumani Manuel Neuer huenda akasalia katika hima Veltins-Arena, huko Gelsenkirchen kufuatia mpango wake wa kutaka kujiunga na klabu ya Bayern Munich kusua sua.

Mwenyekiti wa klabu ya Schalke Clemens Toennies amesema mazungumzo kati yao na viongozi wa Bayern Munich yamekua katika mazingira magumu kufuatia suala la fedha ambayo imeshaanikwa hadharani kama ada ya uhamisho wa kipa huyo.

Ada ya uhamisho wa kipa huyo ni paund million 20 na uongozi wa Bayern Munich umekua ukibembeleza kupunguziwa kiasi hicho hadi kufikia paund million 12.

ALIsema kufuatia hatua hiyo wanafikiri kukaa chini na Manuel Neuer kwa ajili ya kuanza upya utaratibu wa kufanya nae mazungumzo ya kusaini mkataba mpya ambao utaendelea kumuweka huko Veltins-Arena.

Ikumbukwa kwamba Neuer tayari ameshagoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki klabuni hapo huku mkataba wake wa sasa na klabu ya Schalke ukitarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu ujao, hivyo hatua ya uongozi wa klabu hiyo ya kutaka kukaa nae mezani itakua ikifanywa kwa mara ya pili.

MANCINI AKIRI NAFASI YA TATU TIMU YAKE ILIYOPATA NI KAMA BAHATI.

LONDON, England
KOCHA wa klabu ya Manchester City Roberto Mancini amekiri kwamba hatua ya kikosi chake kumaliza kwenye nafasi tatu za juu katika msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza msimu huu ameichukulia kama bahati ya mtende iliyowaangukia.

Mancini aliekabidhiwa kikosi cha klabu hiyo mwezi Oktoba mwaka jana baada ya kutimuliwa kazi Mark Hughes huko City Of Manchester amesema ni vigumu kuamini lakini hana budi kukubaliana na hali halisi kwani majuma mawili yaliyopita alikua hadhani kama wangemaliza na kufikia walipo hivi sasa.

Alisema juhudi za kikosi chake pamoja na kuhizana kila wakati imekua ni hatua kubwa kwao kufikia malengo waliyojiwekea hivyo kwa sasa wanajipanga kucheza ligi ya mabingwa barani ulaya tena wakianzia katika hatua ya makundi.

City wamefanikiwa kushika nafasi ya tatu baada ya kuifunga Bolton Wanderers mabao mawili kwa sifuri huko Reebok Stadium huku Arsenal wakilazimisha sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Fulham huko Craven Cottage.

Katika hatua nyingine Mancini amesema bado anaamini mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez ataendelea kubaki huko City Of Manchester licha ya kuwepo kwa taarifa za kutatanisha.

Mancini alisema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 bado ana mkataba wa muda mrefu hivyo imani yake yamtuma ataendelea kubaki.

Carlos Tevez mwishoni mwa juma lililopita alieleza wazi kwamba atakuwa mwenye furaha zaidi endapo ataondoka Manchester City na kusaka sehemu nyingine ambayo itamuwezesha kupata changmoto mpya katika soka lake baada ya kuipa mafanikio klabu hiyo ya City Of Manchester.

WILSHERE AJITOA TIMU YA VIJANA.

LONDON, England
HATIMAYE kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza pamoja na klabu ya Arsenal Jack Wilshere ametangaza kujiondoa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza chini ya umri wa miaka 21 ambacho mwezi ujao kitaanza kampeni ya kusaka ubingwa wa barani ulaya katika fainali zitakazochezwa huko nchini Denmark.

Wilshere amefikia maamuzi hayo baada ya kufanya mazungumzo na kocha wa timu ya taifa ya vijana ya nchini Uingereza Stuart Pearce, ambapo amemueleza kwamba katika kipindi hiki anahitaji kupumzika baada ya shuruba za ligi kuu kumalizika hapo jana.

Kabla ya maamuzi hayo kufikiwa na kiungo huyo tayari alikua ameshajumuishwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza hatua ambayo ilipingwa vikali na meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger kwa kuidai kwamba Wilshere anahitaji muda wa kupumzishwa.

Mchezaji mwingine alietangaza kujiondoa katika timu ya taifa ya vijana ya nchini Uingereza chini ya umri wa miaka 21 ni mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Andy Carroll ambae pia ameomba kupumzishwa baada ya heka heka za ligi kuu.

MASIKINI ANCELOTTI ALIKUWA HAFAHAMU KWAMBA KIBARUA KIMEOTA NYASI.

LONDON, England
KUNA tetesi kwamba aliekua kocha wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti alikua hafahamu lolote juu ya hatua ya kutimuliwa kwake zaidi ya kutambua mpango wa kuwepo kwa mkutano kati yake na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.

Ancelotti alionyesha hatua hiyo mara baada ya mchezo wa mwisho wa ligi msimu huu, kati ya kikosi chake dhidi ya Everton kumalizika huko Goodson Park ambapo alisema hana budi kusubiri kikao ambacho kitaamua mustakabali wa maisha yake ya baadae huko Stamford Bridge.

Ancelotti pia alikua hana hakika kama angeendelea kusalia klabuni hapo kufuatia kukiri yeye mwenyewe kwamba msimu huu matokeo hayakua mazuri kwake mbali na msimu uliopita hivyo alitarajia lolote katika mkutano huo na bosi Abramovich.

Maamuzi ya kutimuliwa kazi kwa kocha huyo wa kimataifa toka nchini Italia yalichukuliwa akiwa safarini akitokea mjini Liverpool sambamba na kikosi cha klabu ya Chelsea ambacho kilikua kikirejea jijini London.

Taarifa rasmi iliyochapishwa kwenye mtandao wa klabu ya Chelsea imeeleza kwamba Ancelotti ametimuliwa kazi kufuatia matokeo mabovu yaliyokiandama kikosi chake mwishoni mwa mwaka jana hatua ambayo ilipelekea klabu hiyo kupoteza muelekeo wa kutetea ubingwa.

Pia taarifa hiyo imedai kwamba mbali na kupoteza muelekea wa kutetea ubingwa wa nchini Uingereza, meneja huyo alishindwa kukiwezesha kikosi chake kufanya vyema katika michuano mingine waliyoshiriki ikiwa ni pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Hata hivyo Ancelotti ataendelea kukumbukwa klabuni hapo baada ya kuiwezesha Chelsea kutwaa ubingwa wa kombe la ligi msimu uliopita sambamba na kombe la chama cha soka nchini Uingereza FA hatua ambayo ilimfanya kuonyesha furaha mwishoni mwa msimu uliopita tena kwa kuimba nyimbo mbali mbali walipokua wakipita mitaani kwa ajili ya kushangilia ubingwa walioupata.

Solomon Kalou mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast ameelezea masikitiko yake baada ya Ancelotti kupokea taarifa za kufungashiwa viwago huko jijini London.

Hata hivyo amedai kwamba walikua hawafahamu lolote juu ya kutimuliwa kwake lakini ametoa wito kwa wachezaji wenzake kuutumia vyema muda wa mapumziko kabla hawajakutana tena mwezi July tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Monday, May 23, 2011

WAMISRI KUCHEZESHA PAMBANO LA SIMBA NA WYDAD.

DAR ES SALAAM, Tanzania
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Misri
kuchezesha pambano la mkondo mmoja kati ya Simba ya Tanzania na Wydad Casablanca
ya Morocco litakalofanyika Mei 28 mwaka huu Uwanja wa Petrosport jijini Cairo,
Misri.

Mechi hiyo ya kutafuta timu ya kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa
Afrika itaanza saa 12 kamili jioni kwa saa za Cairo.

Waamuzi hao ni Farouk Mohamed atakayepuliza filimbi wakati wasaidizi wake ni
Mohamed Waleed na Hassan Sherif. Mwamuzi wa mezani (fourth official) ni Omar
Fahim wakati Kamishna wa mchezo huo ni Magdy Shams El Din kutoka Sudan.

Mshindi atacheza kundi B pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, Esperance ya
Tunisia na Moloudia Club d’Alger ya Algeria. Timu itakayoshindwa itaingia katika
hatua ya 16 bora ya michuano ya Kombe la Shirikisho ambapo itacheza mechi ya
kwanza nyumbani dhidi ya Daring Club Motema Pembe ya DRC kati ya Juni 10, 11 na
12 mwaka huu.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),
Muhsin Balhabou ndiye atakayeongoza msafara wa timu ya Simba kwenda Cairo kwa
ajili ya mechi hiyo.

ADEBAYOR ATAMANI KUBAKIA MADRID.

MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Adebayor bado anaamini huenda uongozi wa klabu hiyo ukamsajili moja kwa moja baada ya kumsajili kwa mkopo akitokea Man City mwezi januari mwaka huu.

Emmanuel Adebayor ameonyesha kuwa na imani hiyo alipohojiwa na kituo kimoja cha televisheni cha mjini Madrid ambapo amekiri anaipenda klabu hiyo na tayari ameshatengeneza mazingira mazuri ya kuwa na marafiki wa kila aina mjini humo kufuatia uwezo wake anapokua uwanjani.

Toka alipojiunga na Real Madrid mwezi Januari, mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, amecheza michezo 21 na kupachika mabao matano.

UFARANSA WATAJA VIWANJA VYA EURO 2016.

PARIS, Ufaransa
WAKATI nchi za Poland pamoja na Ukraine zikiendelea na maandalizi ya fainali za mataifa ya barani Ulaya zitakazoanza kutimua vumbi lake June 8 – July Mosi mwaka ujao, wenyeji wa fainali hizo kwa mwaka 2016 Ufaransa hii leo wametaja viwanja vitakavyotumika.

Ufaransa waliofanikiwa kushinda harakati za kuwa mwenyeji wa fainali za mataifa ya bara la Ulaya kwa mwaka 2016 baada ya kuzishinda nchi za Italia pamoja na Uturuki wametangaza viwanja tisa vilivyopo katika miji minane tofauti.

Taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa shirikisho la soka la nchi hiyo imefafanua kwamba viwanja viwili kati ya hivyo vipo mjini Paris ambvyo ni Stade de France pamoja na Parc des Princes huku vingine vikiwa katika mji wa Marseille ambacho ni Stade Velodrome, mji wa Nancy ni Stade Marcel Picot, mji wa Lille ni Grand Stade Lille Métropole, mji wa Lyon ni Stade des Lumières, , mji wa Lens ni Stade Felix-Bollaert, pamoja na mji wa Nice ni Grand Stade Nice huku mji wa Bordeaux uwanja wake bado unatengenezwa kwa hivi sasa.

Katika fainali za mataifa ya barani ulaya kwa mwaka huo historia mpya itaandikwa kufuatia timu shiriki kutarajia kuongezea kutoka 16 hadi 24.

PIRLO KUTIMKIA JUVENTUS.

MILAN, Italia
MCHEZAJI wa kimataifa toka nchini humo pamoja na klabu bingwa ya “Sirie A” msimu huu AC Milan Andrea Pirlo imeeleza kwamba yu mbioni kujiunga na klabu ya Juventus yenye maskani yake makuu huko Stadio Olimpico di Torino.

Taarifa za harakati za kiungo huyo kuelekea Juventus kwa ajili ya msimu mpya wa ligi, zimeelezawa wazi na rafiki yake wa karibun aitwae Tullio Tinti baada ya kukaririwa na gazeti la kila siku la michezo la nchini Italia liitwalo "Gazzetta dello Sport " ambapo amesema mipango ya Andrea Pirlo ni kutaka kuichezea klabu hiyo kongwe.

Tullio Tinti amesema siku kadhaa zilizopita Andrea Pirlo alimueleza wazi kwamba angetamani sana kujiunga na meneja wake wa zamani Carlo Ancelotti huko nchini Uingereza katika klabu ya Chelsea lakini hali ya sintofahamu iliyotanda kwa meneja huyo imemkwamisha kutimiza ndoto yake.

Wakati huo huo kiungo wa kimataifa toka nchini Italia pamoja na klabu ya AC Milan Massimo Ambrosini amekubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambao utafikia kikomo mwezi June mwaka 2012.

Hata hivyo uongozi wa klabu ya AC Milan bado umeripotiwa kuendelea na mazungumzo ya kumbembeleza kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi Clarence Seedorf ili aweze kukubali kusaini mkataba wa mwaka mmoja kufuatia mkataba wake wa sasa kuwa mbioni kufikia kikomo.

Thursday, May 19, 2011

PORTO YANYAKUWA UBINGWA WA EUROPA LEAGUE KWA KUIFUNGA BRAGA BAO 1-0.








TFF YAPATA KOCHA MPYA WA UNDER 17 (SERENGETI BOYS) NA UNDER 20 (NGORONGORO HEROES).

Kim Poulsen.

DAR ES SALAAM, Tanzania
KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemwajiri Kim Poulsen, raia wa Denmark kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) na chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kuanzia Mei 15 mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema, Poulsen mwenye leseni ya kulipwa ya ukocha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA) katika ngazi ya diploma, na mkufunzi wa makocha wa kiwango cha juu anayetambuliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU) amesaini mkataba wa miaka miwili.

Alisema kabla ya kujiunga na TFF, Poulsen alikuwa kocha wa timu ya FC Hjorring inayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Denmark kuanzia Julai mwaka jana hadi Mei Mosi mwaka huu.

Mwaka 1989 alikuwa kocha bora wa mwaka nchini Denmark. Tuzo hiyo pia aliipata mwaka 2004 na 2005 nchini Singapore ambapo alikuwa kocha wa timu ya Taifa chini ya umri wa miaka 23. Mwaka 2002 hadi 2003 alikuwa kocha wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 18 ya Singapore.

Mbali ya sifa za ukocha, uteuzi wake pia umezingatia utaratibu wa TFF wa kuwa na makocha wenye falsafa moja ya mpira, hali ambayo inawajengea misingi mizuri wachezaji wa timu za vijana wanaopata fursa ya kuchezea timu ya wakubwa (Taifa Stars).

Utaratibu huo tuliuanzisha toka wakati wa Marcio Maximo akiinoa Stars ambapo makocha wa vijana nao walikuwa wakitoka Brazil. Kocha wa sasa wa Taifa Stars,Jan Poulsen naye anatoka Denmark, na hana uhusiano wowote wa damu na Kim.