Tuesday, May 3, 2011

HOFU YATANDA BARCA.

BARCELONA, Hispania
KLABU ya soka nchini Hispania FC Barcelona wameingia hofu kubwa kufuatia safu yao ya ulinzi kukabiliwa na majeruhi ambao hawatoweza kujumuishwa katika mchezo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya Real Madrid hapo kesho.

Hofu kwa mabingwa hao imeshamiri kufuatia kuumia kwa beki wa kimataifa toka nchini Argentina Gabriel Milito ambae sasa itamlazimu kuwa nje ya uwanja kwa muda wa majuma manne kufuatia maumivu ya paja yanayomkabili.

Mchezaji mwingine alieongeza hofu hiyo ni beki wa pembeni Martin Montoya ambae ameripotiwa kuvunjika mfupa wa bega ambapo hatua hiyo inakadiriwa huenda ikamuweka nje ya uwnaja kwa kipindi kirefu zaidi.

Wachezaji hao wawili walipatwa na maumivu hayo katika mchezo wa ligi wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Real Sociedad ambao walifanikiwa kuwachapa Barcelona mabao mawili kwa moja.

Kuumia kwa wachezaji hao kunamfanya meneja wa klabu ya Barcelona Pep Guardiola Isala kuendelea kuwa na idadi kubwa ya wachezaji majeruhi ambao wanacheza nafasi ya ulinzi kama Eric Abidal, Maxwell Andrade pamoja na Adriano Correia.

Hata hivyo meneja huyo amepokea taarifa njema za kupona kwa kiungo Andrés Iniesta aliekua anasumbuliwa na maumivu ya kiazi cha mguu ambayo yamsababishia kuukosa mchezo wa kwanza wa hatua ya nusu fainali uliochezwa mjini Madrid juma lililopita.

No comments:

Post a Comment