MUSTAKABALI wa kiungo wa kimataifa toka nchini Italia pamoja na klabu ya AC Milan Andrea Pirlo wa kuendelea kubakia San Siro kwa ajili ya msimu ujao bado umeendelea kuwa katika hali ya sintofahamu huku uongozi wa klabu ya Juventus ukitangaza hadharani kuwa tayari kumsajili kiungo huyo.
Mustakabali wa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 31 upo shakani kufuatia mkataba wake na klabu ya AC Milan kutarajia kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu, huku kukiwa hakutn taarifa iliyo rasmi kama atasaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo ama la.
Kocha wa klabu ya AC Milan Massimiliano Allegri usiku wa kuamkia hii leo aliulizwa na waandishi wa habari juu ya sakata hilo, ambapo alijibu kwamba anachofahamu Andrea Pirlo bado ni mchezaji halali wa klabu yake na ataendelea kuwepo katika himaya ya The Rossonelli.
Hata hivyo taarifa zinazoendelea kutolewa katika magazeti karibu ya kila ya nchini Italia zinatanabaisha kwamba kiungo huyo ana asilimia ndogo sana ya kupewa mkataba mpya ambao utamuwezesha kuendelea kuitumikia AC Milan na hii inatokana na majeraha yanayomkabili kila kukicha.
Wakati huo huo rafiki wa karibu wa Andrea Pirlo ambae alishawahi kuwa mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Napoli Pierpaolo Marino amenukuliwa na moja ya chombo cha habari mjini Milan akisema kwamba anachofahamu yeye ni kwamba rafiki yake yu mbioni kujiunga na Juventus kwa ajili ya msimu ujao wa ligi.
1995–1998 Brescia 47 (6)
1998–2001 Internazionale 22 (0)
1999–2000 → Reggina (loan) 29 (6)
2001 → Brescia (loan) 10 (0)
2001– Milan 283 (32)
No comments:
Post a Comment