Tuesday, May 3, 2011

"WEST HAM BADO INA NAFASI." GRANT.

LONDON, England
KOCHA wa Westham United Avram Grant anaamini bado kikosi chake kina nafasi ya kusalia katika ligi kuu ya soka nchini Uingereza kwa ajili ya msimu ujao licha ya kupoteza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Manchester City.

Grant ametoa mtazamo huo mara baada ya mtanange kumalizika huko City Of Manchester ambapo alikishuhudia kikosi cha kikipoteza point tatu muhimu kwa kubamizwa mabao mawili kwa moja.

Alisema kutokana na matokeo hayo kikosi chake kimahesabu kinahitaji point saba ili kiweze kusalia katika michuano ya ligi msimu ujao, hatua ambayo anaamini inaweza kukamilishwa kufuatia kuwa wachezaji wenye njaa ya mafanikio.

Nae Kocha wa Man City Roberto Mancini alisema pamoja na ushindi mabao 2-1 walioupata jana bado kikosi chake kina kazi ya ziada ya kuhakikisha kinashinda michezo iliyosalia endapo wanahitaji kucheza ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao.

Alisema tayari wameshamalizana na West ham utd ambao amekiri walikua wanawahofia kutokana na nafasi yao katika msimamo wa ligi na sasa wanageuzia macho yao katika mchezo ujao wa ligi dhidi ya Everton.

Katika mchezo wa jana mabao ya Man city yalipachikwa wavuni na kiungo wa kimataifa toka nchini Uholanzi Nigel de Jong pamoja na beki wa Argentina Pablo Zabaleta huku bao la kufutia machozi kwa upande wa West Ham utd liikifungwa na na Demba Ba.

No comments:

Post a Comment