Tuesday, June 21, 2011

RATIBA YA LIGI KUU UINGEREZA YAIKABA ARSENAL MAPEMA.

LONDON, Uingereza
BAADA ya ratiba ya ligi kuu ya soka nchini humo kuwekwa hadharani, washika bunduku wa Ashburton Grove Arsenal waliopania kufanya vyema msimu ujao, wanaonekana kuwa na michezo mikali zaidi katika siku za mwanzoni.

Arsenal ambao wana kiu ya kutwaa ubingwa wa nchini Uingereza ambao kwa mara ya mwisho waliupelekea Highbury katika msimu wa mwaka 2003-04, wamepangwa kuanza kusaka taji hilo msimu ujao kwa kucheza na Newcastle United ugenini na kisha watafuata na Liverpool huko Emirates Stadium.

Mchezo wa tatu kwa washika bunduki hao utawakutanisha na mashetani wekundu Manchester United huko Old Traffrod kabla ya kukutana na klabu iliyopanda daraja ya Swansea City katika uwanja wa Emirates.

Kufuatia muonekanano huo wa ratiba ambao unachukuliwa kama changamoto kwa meneja wa Arsenal Arsene Wenger pamoja na kikosi chake kwa ujumla, beki wa zamani wa klabu hiyo pamoja na timu ya taifa ya Uingerezea Sol Campbell amesema kuna ulazima kwa The Gunners kufanya jitihada za kushinda michezo mitatu ya mwanzo.

Sol Campbell ambae ameitumikia Arsenal kuanzia mwaka 2001–2006 na kisha kurejea tena klabuni hapo mwaka 2010 amesema endapo The Gunners watapata ushindi katika michezo hiyo mitatu ya mwanzo wachezaji watajijengea mazingira ya kujiamini na hatua hiyo itawasaidia kutengeneza mipango ya kuzifunga timu nyingine huko mbele ya safari.

No comments:

Post a Comment