LONDON, England
HATIMAYE Fernando Torres amejiunga na Chelsea dakika za mwisho kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa baada ya Liverpool kukubali ofa kabambe ya Euro milioni 50.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania sasa atajiunga Chelsea baada ya uhamisho wake kuvunja rekodi Uingereza. Liverpool tayari wamekubali kulipa Euro milioni 35 kwa ajili ya mchezaji wa Newcastle Andy Carroll ili kuziba pengo la Torres.
Taarifa kutoka katika mtandao wa klabu ya Liverpool ilisomeka kama ifuatavyo, 'Liverpool Football Club tonight confirmed they have agreed a fee with Chelsea for the sale of Fernando Torres. The player has now been given permission to speak to the London club.'
Torres atapewa mkataba wa miaka mitano akiwa Stamford Bridge na atakuwa akilipwa kiasi cha Euro 175,000 kwa wiki.
PICHANI. Mashabiki wa Liverpool wakichoma jezi ya Torres katika uwanja wa mazoezi wa klabu muda mfupi kabla ya kutangazwa kuuzwa kwa mchezaji huyo.
Mchezaji huyo alikuwa akilipwa kiasi cha Euro 110,000 wakati akiwa Liverpool ambapo mkataba wake ulikuwa ukiisha 2013, kabla ya kuomba kuhama katika klabu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita, na klabu hizo mbili zimekuwa katika mazungumzo wikiendi hii.
Liverpool ilimsajili mchezaji huyo kwa kiasi cha Euro milioni 21 Julai mwaka 2007, na walikuwa na nia ya kumzuia mchezaji huyo mpaka dirisha litakapofungwa bila kupokea ofa yoyote, lakini waliogopa kwani ingeleta picha mbaya sio kwa Tirres tu bali na kwa wachezaji wengine pia.
Monday, January 31, 2011
LIVERPOOL YAPATA MBADALA WA TORRES.
LONDON,England
KLABU ya Liverpool ya Uingereza imekubali kutoa ada ya uhamisho ya Paundi milioni 23 ili kumsajili mshambuliaji Luis Suarez kutoka klabu ya uholanzi ya Ajax Amsterdam.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uruguay mwenye umri wa miaka 24 amefaulu majaribio ya afya, huku kukamilika kwa uhamisho wake kukitarajiwa kukamilika hivi leo.
Hapo awali Liverpool ilitoa ofa ya paundi milioni 12.7 kwa ajili ya Suarez, lakini klabu ya Ajax ikawataka kuongeza ofa hiyo ili kuwashawishi wadachi hao kuumuza mshambuliaji huyo.

LEE AFURAHIA BAO ALILOFUNGA KATIKA MCHEZO WA FAINALI DHIDI YA AUSTRALIA.
DOHA, Qatar
SHUJAA wa Japan katika mchezo wa fainali wa Kombe la Bara la Asia dhidi ya Australia, Tadanari Lee amefurahishwa kwea kushinda bao lake la kwanza akiwa na Blue Samurai katika mchezo muhimu katika mashindano hayo.
Akiwa pia amekwisha ichezea timu ya Korea Kusini ya chini ya miaka 20 mwaka 2004, Lee (25) anafurahia kuifungia Japan kwa staili ya aina yake.
"Nimekulia katika utamaduni wa kijapan na napenda nchi zote yaani Korea na Japan. Nimefurahi kuifungia bao Japan," alisema Lee.
SHUJAA wa Japan katika mchezo wa fainali wa Kombe la Bara la Asia dhidi ya Australia, Tadanari Lee amefurahishwa kwea kushinda bao lake la kwanza akiwa na Blue Samurai katika mchezo muhimu katika mashindano hayo.
Ilimchukua dakika sita toka lipoingia uwanjani kufunga bao hilo la ushindi, ambalo liliiongoza timu hiyo kutawazwa mabingwa wapya wa michuano ya hiyo katika bara la Asia.
"Nilikuwa nataka kwenda upande wa karibu lakini nilimuona beki wao akienda upande ule. Hivyo nilisimama na Nagamoto akanipa mpira mzuri. Wakati mpira uliponifikia nilifikiria kuwa nahitaji kuupiga," alisema Lee akihijiwa na mtandao goal.comAkiwa pia amekwisha ichezea timu ya Korea Kusini ya chini ya miaka 20 mwaka 2004, Lee (25) anafurahia kuifungia Japan kwa staili ya aina yake.
KILI MARATHON YAPAMBA MOTO.
Picha inawaonyesha wakimbiaji wakianza mbio za mashindano hayo mwaka jana.
MOSHI, Kilimanjaro
MITAA ya mji wa Moshi inatarajiwa kufurika watu watakajitokeza kushuhudia mbio kubwa barani Afrika hapo siku ya Jumapili tarehe 27 Februari 2011, wakati maelfu ya wakimbiaji watakaposhiriki mbio za mwaka huu za Kilimanjaro Marathon.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Francis John alisema mbio hizo zitashirikisha wanariadha nyota barani Afrika waliowahi kuvuma kitaifa na kimataifa.
Mlima Kilimanjaro.
Amewataja baadhi ya wanariadha hao kuwa ni pamoja na Patrick Nyangero, Andrea Silvini, Daudi Joseph, Sarah Majah, Sarah Kavina na Banuelia Brighton.

Thursday, January 20, 2011
DONDOO ZA DIRISHA DOGO UINGEREZA.
LONDON, England
Wakati dirisha dogo la usajili likiwa wazi katika ligi kuu ya Uingereza, klabu za Arsenal na Manchester United zimesemekana kumuwania mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos.
Beki huyo wa kimataifa wa Hispania anawaniwa kwa kitita cha paundi milioni 25.
Wakati huo huo wachezaji wawili wa klabu ya Everton wenye umri wa miaka 22 Victor Anichebe na Seamus Coleman kwa pamoja wametia saini mikataba mipya ya miaka minne na nusu kila mmoja kuendelea kusaka kabumbu katika klabu hiyo.
Naye Bosi wa klabu ya Sunderland Steve Bruce anatazamiwa kuzungumza na meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson kuhusiana na suala la kumsajili nyota wa Manchester United Michael Owen mwezi huu.
Bosi huyo wa ‘The Black Cats’ anafanya jitihada za kumchukua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kuziba nafasi ya Darren Bent aliyetimka na kujiunga na Aston Villa.

ARSENAL YAIRARUA LEEDS FA.
LEEDS, England
MAGOLI yaliyofungwa na Samir Nasri, Bacary Sagna na Robin van Persie yalitosha kuipa ushindi Arsenal wa mabao 3-1 dhidi ya Leeds United katika mchezo wa raundi ya tatu ya Kombe la FA uliochezwa jana usiku.
Leeds, ambao walilazimisha sare ya 1-1 jijini London Jan 8 na kusabisha mchezo huo kurudiwa jana. Leeds walipata bao la kufutia machozi kupitia kwa mchezaji wake Bradley Johnson ambaye ameshawahi kufanya mazoezi na Arsenal kipindi cha nyuma kwa shuti la umbali wa mita 25 lililomwacha kipa Wojciech Szczesny akiwa hana la kufanya.
Kwa ushindi huo Arsenal wataikaribisha Huddesfield katika raundi ya nne Januari 30 mwaka huu.

Wednesday, January 19, 2011
CANTONA APATA KIBARUA MAREKANI.
LONDON, England
Timu ya New York Cosmos imemuajiri mchezaji mahiri wa zamani wa kimataifa wa Manchester United na Ufaransa Erick Cantona kama Mkurugenzi wa timu hiyo.
Cosmos walinunua jina hilo kutoka klabu ya zamani iliyokuwa ikicheza katika ligi hiyo ya Marekani na wanategemea kuwa moja ya klabu ya 20 katika Major League Soccer (MLS). Timu hiyo bado haijapata uwanja wake yenyewe katika maeneo ya New York.
Taarifa ya klabu ilisema Cantona (44), ambaye alishafu kucheza soka mwaka 1997, atakuwa na majukumu katika kuchagua kikosi cha kwanza. Cantona alisema kuwa "Cosmos ni klabu ngumu na imetengenezwa vizuri, ikiwa na hitoria bora. Ni mchanganyiko kati ya soka na sanaa."
Cantona atafanya kazi na kiungo wa zamani wa Marekani Cobi Jones, ambaye ni Mkurugenzi Msaidizi wa michezo wa klabu hiyo.

BAADA YA KULA ZA USO MCHEZO WA YANGA NA ATLETICO YA BRAZIL, WAAMUA KUFUTA VIINGILIO KATIKA MCHEZO WA PILI DHIDI YA SIMBA.
DAR ES SALAAM, Tanzania
KUTOKANA na muitikio mdogo wa mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia mchezo wakirafiki baina ya Yanga ya Dar es Salaam na Atletico Paranaense ya Brazil kwenye Uwanja wa Taifa jana ambapo Yanga iligaragazwa kwa mabao 3-2, Rais wa Kampuni ya RPB Oil, Rahma Al Kharoous, amesema kuwa mchezo wa kesho jioni kati ya Simba na timu hiyo kiingilio itakuwa ni bure.
Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Rahma, ambaye ndiye mratibu wa michezo hiyo ya kirafiki, alisema kuwa ameamua kufanya kiingilio kuwa bure ili mashabiki wengi waweze kujitokeza kushuhudia mchezo huo na kuishangilia timu ya Simba ili kuwapa morari waweze kushinda.
Aidha alisema kuwa iwapo Simba itaweza kuibuka na ushindi basi ataigharamia timu hiyo ya Simba kuisafirisha hadi nchini Brazil kwa ajili ya mchezo wa marudiano na kuwataka mashabiki wengi kujitokeza kushuhudia mchezo huo.

RUUD GULLIT AIBUKIA URUSI.
MOSCOW, Russia
RUUD GULLIT ameteuliwa kuwa kocha mkuu wa klabu ya Terek Grozny ya Russia kwa mkataba wa miezi 18.
Gullit mwenye umri wa miaka 48 ambaye ni bosi wa zamani wa klabu za Chelsea, Newcastle na Feyenoord amekuwa nje ya utawala na uongozi tangu alipoondoka katika klabu ya Los Angeles Galaxy mwezi Agosti 2008.
Gullit raia wa uholanzi kwa kuanzia ametia saini mkataba wa mwaka mmoja na nusu, huku kukiwa na uwezekano wa kuongeza muda huo.
Klabu hiyo ya Terek Grozny ya Jamhuri ya Chechen imemaliza msimu wa ligi ikiwa katika nafasi ya 12 kati ya vilabu 16 vilivyoshiriki Russian Premier Liga mwaka jana.

JERMAINE JONES ATUA KWA MKOPO BLACKBURN
LONDON, England
KLABU ya Blackburn ya Uingereza imemsajili kiungo Jermaine Jones kwa mkopo katika mkataba wa miezi sita kutoka klabu ya Schalke 04 inayoshiriki ligi ya Bundesliga.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani mwenye umri wa miaka 29 ameungana na mshambuliaji Roque Santa Cruz baada ya dirisha dogo la usajili la Januari kufunguliwa Ewood park.
Bosi wa klabu ya Blackburn Steve Kean amesema usajili huo ni wa manufaa kwa klabu hiyo, na kwa yeyote anayemfahamu Jones atakubali kuwa ni mchezaji mwenye kujituma.

Monday, January 17, 2011
MISRI YATWAA MICHUANO YA NILE BASIN.
CAIRO, Misri
WENYEJI na wadhamini wa michuano ya Nile Basin Misri wameigaragaza Uganda kwa mabao 3-1 katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo uliochezwa jana jioni jijini Cairo, Misri.
Sayed Hamdi ndio aliyefungua ukurasa wa mabao kwa kuipatia timu yake bao la kuongoza dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika na kuongeza la pili sekunde 18 kabla kipenga cha mapumziko hakijapulizwa na kumfanya kuwa na magoli sita katika michuano hiyo. Geddo aliipatia Pharaohs bao la tatu dakika ya 82.
Mchezaji wa Uganda Ceasar Okuhti aliipatia timu yake bao la kufutia machozi dakika za majeruhi kabla ya mtanange huo kumalizika. Katika hatua ya makundi, Misri waliwafunga Uganda bao 1-0.
Katika mchezo wa awali wa kutafuta mshindi watatu, DR Congo iliifunga Kenya kwa ushindi mwembamba wa bao 1-0 na kuchukua nafasi ya tatu. Timu pia zilikutana katika hatua za makundi na Kenya ilifungwa kwa matokeo kama hayo. Jumapili Sudan iliifunga Tanzania mabao 2-0 na kujinyakulia nafasi ya tano.
Mabingwa Misri walinyakua kitita cha dola 173,000 na Uganda dola 123,000. Mshindi wa tatu DR Congo walipata dola 104,000. Mshindi wa nne na wa tano, Kenya na Sudan nao pia watapata zawadi ya fedha.
Michuano hiyo iliandaliwa na Shirikisho la Soka la Misri na ilishirikisha nchi zilizopitiwa na Mto Nile.

BABEL ATOZWA FAINI
Picha ya mwamuzi Howard Webb akiwa amevaa jezi ya Man United ambayo imemtia matatani Babel.
LONDON, England
Winga machachari wa Liverpool Ryan Babel amepigwa faini ya dola 16,000 na Shrikisho la Soka la Uingereza kwa kutoa comment za kuponda marefa wanaochezesha Ligi Kuu ya Uingereza katika mtandao wa Twitter.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Uholanzi alituma picha katika mtandao huo ya mwamuzi Howard Webb akiwa amevaa jezi ya Manchester United baada ya kuchukizwa na maauzi aliyiyafanya katika mchezo ambao timu hiyo ilipoteza kwa United kwa kufungwa bao 1-0 katika Uwanja wa Old Traford Jan 9, 2011.

Thursday, January 13, 2011
JINSI RONALDINHO ALIVYOPOKEWA KISHUJAA BRAZIL.
Ronaldinho akiwa na Rais Flamengo Patricia Amorim wakati akimtambulisha rasmi mbele ya maelfu ya watu jijini Rio.
Shabiki wa Ronaldinho akiwa na sanamu ya mchezaji huyo katika hafla ya kumtambulisha mchezaji huyo.
Picha juu inaonesha maelfu ya mashabiki wanaokadiriwa kufikia 20,000 walihudhiria hafla ya kutambulishwa mchezaji huyo katika timu ya Flamengo.

Monday, January 10, 2011
GAUCHO ARUDI NYUMBANI KUICHEZEA FLAMENGO
BRAZIL
KLABU ya soka ya Flamengo ya Brazil imeweka wazi katika mtandao wake kwamba imemsajili kiungo nyota Ronaldinho kwa mkataba wa miaka mitatu na nusu.
AC Milan klabu ya zamani ya Ronaldinho itakuwa italipwa kiasi cha Euro milioni 3 kwa uhamisho wa mchezaji huyo kutoka Rossoneri kwenda Mengao, na atakuwa akilipwa kiasi cha Euro 130,000 kwa wiki, kiasi ambacho kitakuwa kikilipwa na na wawekezaji wa timu hiyo Traffic na Olympikus.
Mchezaji huyo wa zamani wa mwaka wa FIFA anatarajiwa kutangazwa rasmi katika vyombo vya habari Alhamisi.

MESSI AIKWAA KWA MARA PILI MFULULIZO TUZO YA MCHEZAJI BORA WA DUNIA.
ZURICH, Uswis
Lionel Messi ameshinda tuzo ya pili ya mchezaji bora wa dunia, na amekuwa mchezaji wa kwanza kupata tuzo hiyo mfululizo toka aliposhinda Ronaldinho mwaka 2004-2005.
Mshambuliaji huyo wa Argentina amewashinda wachezaji wenzake anaocheza nao katika timu ya Barcelona Xavi Hernandez na Adres Iniesta katika tuzo hizo.
Mchezaji mwanamama Marta ameshinda tuzo kama hiyo kwa upande wa kina mama kwa mwaka wa tano sasa.
Jose Mourinho Kocha wa Real Madrid amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka baada ya kuingoza Inter Milan kushinda taji la Champions League.
Messi (23) ameisaidia Barcelona kutetea taji lake la ligi ambapo mpaka sasa pia wwanaongoza ligi ya Hispania.
Mourinho ameisaidia Inter kushinda mataji matatu mfululizo kabla ya kujiunga na Real Madrid.

BECKHAM AFANYIWA VIPIMO TOTTENHAM LEO.
LONDON, England
David Beckham amefanyiwa vipimo katika klabu ya Tottenham Jumatatu hii kabla ya kuanza mazoezi na klabu hiyo.
Pamoja na mchezaji huyo kupata ruksa ya kuchezea klabu hiyo kwa miezi miwili kwa mkopo kutokea Los Angeles Galax, kiungo huyo na Spurs wanaamini kwamba wataweza kuongeza mkataba huo.
Baada ya kufanyiwa vipimo katika Uwanja wa mazoezi wa Spurs Mashariki mwa London, Beckham aliondoka ndani ya masaa mawili akkiwa amevaa traki-suti ya klabu hiyo.
Beckham (35) ana matumaini ya kuichezea Tottenham ili kufufua matumaini yake ya kuitwa katika timu ya taifa ya Uingereza, ambapo mpaka sasa ameshaitwa mara 115 akiwa ndiye mchezaji aliyechezea mechi nyingi timu hiyo ya taifa.

HENRY AFANYA MAZOEZI NA ARSENAL.
LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa New York Red Bulls Thierry Henry ameanza mazoezi katika klabu ya zamani ya Arsenal ili kujiweka fiti katika kipindi hiki ambacho Ligi ya Marekani imemaliza msimu wake.
Henry (33) aliondoka Arsenal mwaka 2007 na kuhamia Barcelona baada ya kuweka rekodi katika klabu hiyo kwa kufunga magoli 226 katika kipindi cha mwaka 1999 na 2007.
Klabu ya Arsenal ilisema katika kipindi kifupin atachofanya mazoezi hapo kitamsaidia kumuweka fiti kabla ya kurudi tena katika timu yake ya NY Red Bulls.
Henry ataanza msimu wa pili na Red Bulls Machi 19 kwa mchezo dhidi ya Seatle Sounders nyumbani.

Tuesday, January 4, 2011
TAIFA STARS KUIVAA MISRI KATIKA NILE BASIN FRIENDLY TOURNAMENT.
CAIRO, Misri
TIMU ya Taifa ya Misri itacheza mchezo wake ufunguzi na timu ya Taifa ya Tanzania katika michuano ya kirafiki ya Nile Basin Januari 5 mwaka huu. Michuano hiyo imeandaliwa na Misri kuanzia Januari 5 mpaka 7 na inatarajiwa kushirikisha nchi 7 za Afrika. Nchi zinazoshiriki michuano hiyo ni pamoja na Sudan, Tanzania, Uganda, Burundi, Kenya, Congo DR na wenyeji Misri. Lengo kubwa la michuano hiyo ni kuunda umoja na kulinda vyanzo vya Mto Nile kwa ajili ya kizazi kijacho ambapo nchi zote hizo zinazoshiriki zinatumia mto huo.
Nchi nne, Misri, Tanzania, Uganda na Burundi zitacheza katika kundi A, wakati kundi B zitakuwepo nchi za Sudan, Kenya na Congo DR.
Katika droo iliyochezeshwa iliiweka Uganda na Sudan tofauti baada ya Sudan kuomba wasichezeshwe kundi moja na Uganda ambao wanakutana nao katika kundi moja katika michuano ya CHAN 2011 mwezi ujao.
Timu mbili kutoka katika kila kundi ndizo zitafuzu hatua ya nusu fainali. Ambapo timu itakayoongoza katika kundi A itacheza na timu itayoshika nafasi ya pili ya kundi B, wakati timu itakayoongoza kundi B itacheza na timu itayoshika nafsi ya pili katika kundi A.
Timu zitakazoshika nafasi ya tatu katika makundi hayo mawili zitashindania nafasi ya tano.

Monday, January 3, 2011
MMOJA WA ALIYESHAMBULIA MSAFARA WA TIMU YA TAIFA YA TOGO AENDA JELA MIAKA 24.
Pichani hapo ni Obilale golikipa wa Togo akiwa amelala kitandani akikimbizwa hospitalini mara baada ya kutua nchini Afrika Kusini.
LUANDA, Angola
MAHAKAMA nchini Angola imemhukumu mtu mmoja miaka 24 jela kufuatia tukio la kushambulia msafara wa timu ya Taifa ya Togo mapema mwaka jana shambulio ambalo lilipelekea watu wawili kupoteza maisha na wengine nane kujeruhiwa, akiwemo golikipa namba moja wa timu hiyo.
Jean Antuan Pwaty (42) raia wa Congo DRC alihukumiwa kwa makosa matatu la kuuwa, kumilikisilaha kinyume cha sheria na shambulio la mauaji iliripoti redio moja nchini Angola. Mwanasheria wake amesema atakata rufani kufuatia adhabu aliyopewa mteja wake huyo.
Obilale akiwa katika baiskeli ya magurudumu nchini Ufaransa akitibiwa ili aweze kutembea tena, lakini ndoto za kucheza tena soka hazipo kwa mchezaji huyo.
Timu ya Taifa ya Togo kutoka upande wa Magharibi mwa Afrika ilikuwa ikisafiri kwa barabara kuelekea kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yalifanyika Angola Januari mwaka jana wakati basi lao walilokuwa wakisafiria kushambuliwa kwa risasi katika mji wa Cabinda uliopo mpakani mwa Angola.
Kocha wa timu ya Togo na mwandishi wa habari waliuawa katika tukio hilo. mmoja ya walijeruhiwa golikipa Kodjovi Obilale, ambaye alipata majeraha kiunoni alisema hategemei kucheza mpira tena kwa majeraha aliyopata lakini ana matumaini ya kutembea siku kwani mpaka hivi sasa bado hawezi kutembea.

BAADHI YA MATUKIO KATIKA PICHA YALIYOTOKEA KATIKA LIGI KUU YA UINGEREZA WIKIENDI YA KWANZA YA MWAKA MPYA 2011.
ILIKUWA siku nyingine ya kusononesha kwa timu ya Chelsea baada ya kutoka suluhu nyumbani na timu ya Aston Villa na kuzidi kupeperusha matumaini ya kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza, pichani anaonekana golikipa Petr Cech akiangalia huku akiwa hana la kufanya wakati mchezaji Ciaran Clark akiipatia timu yake bao la kusawazisha dakika za majeruhi na kupelekea timu hizo kutoka sare ya mabao 3-3.
Mchezaji wa Manchester United Javier Hernandez akipiga kichwa na kuifungia timu yake bao la kuongoza dhidi ya West Brom.
Hatimaye Rooney naye aliona mwezi baada ya ukame wa mabao kwa muda mrefu, pichani akishangilia bao lake baada ya kufunga na kupelekea timu yake kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya West Brom katika uwanja wa Old Traford.
Arsenal walianza mwaka kwa staili ya aina yake baada ya kuwabamiza bila ya huruma Birmigham katika Uwanja wao wa nyumbani, pichani hapo juu mshambuliaji wa Gunners Robin van Persie akiifungia bao la kuongoza timu yake, katika mchezo huo Arsenal ilishinda mabao 3-0.
Liverpool nao walianza mwaka vizuri baada ya kuifunga Bolton mabao 2-1 pichani wachezaji wa Liver wakishangilia moja ya mabao hayo.
Sunderland nao walianza 2011 kwa staili ya kipekee baada ya kuishindilia bila ya huruma Blackburn mabao 3-0 picha ni mshambuliaji wa Sunderland akishangilia moja ya mabao hayo.
Mshambuliaji mwenye kasi zaidi katika Ligi Kuu ya Uingereza Gareth Balle akishangilia bao lake wakatika timu ilipocheza na Fulham bao hilo ndilo pekee lilifungwa katika mchezo huo.

Subscribe to:
Posts (Atom)