Monday, November 29, 2010

BAADA YA KUPIGWA 5-0, MOURINHO ANYOOSHA MIKONO KWA BARCELONA.

BARCELONA, Hispania.
KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amekiri kuwa kikosi cha Barcelona kilikuwa bora baada ya kuifunga timu hiyo mabao 5-0 katika Uwanja Camp Nou.

Barcelona walitoka kifua mbele kwa mabao 2-0 wakati timu hizo zilipokwenda mapumziko na kuongeza mabao mengine katika kipindi cha pili na kjuihakikishia timu hiyo uongozi wa Ligi Kuu ya Hispania numa ya wapinzani wao Madrid.

"Timu moja ilicheza vizuri na nyingine vibaya," alikaririwa Mourinho akiwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo huo. " Moja listahili kushinda na nyingine ilistahili kushindwa.

"Tumedhalilishwa? Hapana. Ni rahisi kukubali tulivyoshindwa, kwakuwa hatucheza vizuri."

Barcelona sasa wanaongoza ligi kwa pointi mbili mbele ya Madrid, ambapo mabao ya timu hiyo yalifungwa na Xavi na Pedro katika kipindi cha kwanza, David Villa alifunga mawili na la mwisho alimalizia Jeffren alieingia badala ya Xavi.

Friday, November 26, 2010

RATIBA YA TUSKER CHALLENGE CUP 2010.

Full Broadcast Schedule – (all times in CAT)

TEAMS
DATE
START TIME
CHANNEL
EVENT TYPE
BURUNDI VS SOMALIA
27 November 2010
12:45:00
Super Sport Nine
LIVE
TANZANIA VS ZAMBIA
27 November 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
BURUNDI VS SOMALIA
27 November 2010
23:00:00
SuperSport Five Africa
DELAYED
BURUNDI VS SOMALIA
27 November 2010
23:00:00
SuperSport Five Nigeria
DELAYED
TANZANIA VS ZAMBIA
28 November 2010
01:00:00
SuperSport Five Africa
DELAYED
TANZANIA VS ZAMBIA
28 November 2010
01:00:00
SuperSport Five Nigeria
DELAYED
SUDAN VS ZANZIBAR
28 November 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
RWANDA VS IVORY COAST
28 November 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
BURUNDI VS SOMALIA
28 November 2010
08:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
TANZANIA VS ZAMBIA
28 November 2010
10:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
SUDAN VS ZANZIBAR
28 November 2010
22:00:00
SuperSport Seven
DELAYED
SUDAN VS ZANZIBAR
28 November 2010
22:00:00
SuperSport Seven Nigeria
DELAYED
RWANDA VS IVORY COAST
29 November 2010
00:00:00
SuperSport Seven
DELAYED
RWANDA VS IVORY COAST
29 November 2010
00:00:00
SuperSport Seven Nigeria
DELAYED
SUDAN VS ZANZIBAR
29 November 2010
04:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
RWANDA VS IVORY COAST
29 November 2010
06:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
ETHIOPIA VS UGANDA
29 November 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
MALAWI VS KENYA
29 November 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
ETHIOPIA VS UGANDA
29 November 2010
19:30:00
SuperSport Seven
DELAYED
MALAWI VS KENYA
29 November 2010
21:30:00
SuperSport Seven
DELAYED
ETHIOPIA VS UGANDA
29 November 2010
19:30:00
SuperSport Seven Nigeria
DELAYED
MALAWI VS KENYA
29 November 2010
21:30:00
SuperSport Seven Nigeria
DELAYED
ETHIOPIA VS UGANDA
29 November 2010
22:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
MALAWI VS KENYA
30 November 2010
00:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
ZAMBIA VS BURUNDI
30 November 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
SOMALIA VS TANZANIA
30 November 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
ZAMBIA VS BURUNDI
30 November 2010
22:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
SOMALIA VS TANZANIA
01 December 2010
00:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
SUDAN VS RWANDA
01 December 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
IVORY COAST VS ZANZIBAR
01 December 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
ZAMBIA VS BURUNDI
01 December 2010
00:00:00
SuperSport Seven
DELAYED
SOMALIA VS TANZANIA
01 December 2010
02:00:00
SuperSport Seven
DELAYED
ZAMBIA VS BURUNDI
01 December 2010
00:00:00
SuperSport Seven Nigeria
DELAYED
SOMALIA VS TANZANIA
01 December 2010
02:00:00
SuperSport Seven Nigeria
DELAYED
SUDAN VS RWANDA
01 December 2010
20:00:00
SuperSport Seven Nigeria
DELAYED
IVORY COAST VS ZANZIBAR
01 December 2010
22:00:00
SuperSport Seven Nigeria
DELAYED
UGANDA VS MALAWI
02 December 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
KENYA VS ETHIOPIA
02 December 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
UGANDA VS MALAWI
02 December 2010
22:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
UGANDA VS MALAWI
03 December 2010
00:30:00
SuperSport Five Africa
DELAYED
KENYA VS ETHIOPIA
03 December 2010
02:30:00
SuperSport Five Africa
DELAYED
UGANDA VS MALAWI
03 December 2010
00:30:00
SuperSport Five Nigeria
DELAYED
KENYA VS ETHIOPIA
03 December 2010
02:30:00
SuperSport Five Nigeria
DELAYED
KENYA VS ETHIOPIA
03 December 2010
00:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
SOMALIA VS ZAMBIA
03 December 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
ZANZIBAR VS RWANDA
03 December 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
SOMALIA VS ZAMBIA
03 December 2010
21:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
ZANZIBAR VS RWANDA
03 December 2010
23:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
UGANDA VS MALAWI
03 December 2010
06:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
KENYA VS ETHIOPIA
03 December 2010
08:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
SOMALIA VS ZAMBIA
04 December 2010
00:00:00
SuperSport Six Africa
DELAYED
ZANZIBAR VS RWANDA
04 December 2010
02:00:00
SuperSport Six Africa
DELAYED
MALAWI VS ETHIOPIA
04 December 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
TANZANIA VS BURUNDI
04 December 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
MALAWI VS ETHIOPIA
04 December 2010
22:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
TANZANIA VS BURUNDI
05 December 2010
00:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
MALAWI VS ETHIOPIA
05 December 2010
02:10:00
SuperSport Five Africa
DELAYED
TANZANIA VS BURUNDI
05 December 2010
04:00:00
SuperSport Five Africa
DELAYED
MALAWI VS ETHIOPIA
05 December 2010
02:10:00
SuperSport Five Nigeria
DELAYED
TANZANIA VS BURUNDI
05 December 2010
04:00:00
SuperSport Five Nigeria
DELAYED
IVORY COAST VS SUDAN
05 December 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
UGANDA VS KENYA
05 December 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
IVORY COAST VS SUDAN
05 December 2010
22:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
MALAWI VS ETHIOPIA
05 December 2010
06:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
TANZANIA VS BURUNDI
05 December 2010
08:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
UGANDA VS KENYA
06 December 2010
00:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
IVORY COAST VS SUDAN
06 December 2010
00:00:00
SuperSport Five Africa
DELAYED
UGANDA VS KENYA
06 December 2010
02:00:00
SuperSport Five Africa
DELAYED
IVORY COAST VS SUDAN
06 December 2010
00:00:00
SuperSport Five Nigeria
DELAYED
UGANDA VS KENYA
06 December 2010
02:00:00
SuperSport Five Nigeria
DELAYED
B1 VS C2
07 December 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
A1 VS Q2
07 December 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
A1 VS Q2
07 December 2010
22:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
A1 VS Q2
07 December 2010
23:00:00
SuperSport Six Africa
DELAYED
B1 VS C2
08 December 2010
00:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
B1 VS C2
08 December 2010
01:00:00
SuperSport Six Africa
DELAYED
C1 VS Q1
08 December 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
A2 VS B2
08 December 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
C1 VS Q1
08 December 2010
22:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
C1 VS Q1
08 December 2010
21:30:00
SuperSport Six Africa
DELAYED
A2 VS B2
08 December 2010
23:30:00
SuperSport Six Africa
DELAYED
A2 VS B2
09 December 2010
00:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
WINNER 19 VS WINNER 20
09 December 2010
13:45:00
SuperSport Nine
LIVE
WINNER 19 VS WINNER 20
09 December 2010
22:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
WINNER 19 VS WINNER 20
09 December 2010
23:00:00
SuperSport Seven
DELAYED
WINNER 19 VS WINNER 20
09 December 2010
23:00:00
SuperSport Seven Nigeria
DELAYED
WINNER 19 VS WINNER 20
09 December 2010
13:45:00
Supersport Four
LIVE
WINNER 21 VS WINNER 22
10 December 2010
13:45:00
SuperSport Nine
LIVE
WINNER 21 VS WINNER 22
10 December 2010
22:00:00
SuperSport Nine
DELAYED
WINNER 21 VS WINNER 22
10 December 2010
23:00:00
SuperSport Seven
DELAYED
WINNER 21 VS WINNER 22
10 December 2010
23:00:00
SuperSport Seven Nigeria
DELAYED
WINNER 21 VS WINNER 22
10 December 2010
13:45:00
Supersport Four
LIVE
3RD & 4TH PLACE PLAYOFF
12 December 2010
12:45:00
SuperSport Nine
LIVE
FINAL
12 December 2010
14:55:00
SuperSport Nine
LIVE
3RD & 4TH PLACE PLAYOFF
12 December 2010
22:30:00
SuperSport Nine
DELAYED
3RD & 4TH PLACE PLAYOFF
12 December 2010
21:30:00
SuperSport Five Africa
DELAYED
FINAL
12 December 2010
23:30:00
SuperSport Five Africa
DELAYED
3RD & 4TH PLACE PLAYOFF
12 December 2010
21:30:00
SuperSport Five Nigeria
DELAYED
FINAL
12 December 2010
23:30:00
SuperSport Five Nigeria
DELAYED
FINAL
12 December 2010
18:30:00
Supersport Four
DELAYED
3RD & 4TH PLACE PLAYOFF
12 December 2010
12:45:00
Supersport Four
LIVE
FINAL
13 December 2010
00:30:00
SuperSport Nine
DELAYED

FIFA YATOA ORODHA YA WACHEZAJI 55 WATAKAOTEULIWA KUUNDA KIKOSI CHA DUNIA.

ZURICH, Switzerland
UMOJA wa wachezaji Duniani (FIFPro) na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) limeteua majina ya wachezaji 55 kwa ajili ya uteuzi wa timu ya Dunia maarufu kama FIFA/FIFPro World XI 2010, kikosi ambacho kitatajwa Januari 10, 2011 Zurich, Uswis.

Wachezaji wakulipwa 50,000 ambao wapo katika umoja huo duniani na kuunda FIFPro walipatiwa fomu kwa ajili ya uteuzi wa kikosi wanachokiona kinafaa kuwa cha dunia wakichagua mabeki bora wanne, viungo watatu, washambuliaji watatu na mlinda mlango mmoja kwa mwaka 2010.

Mabingwa wa Dunia Hispania ndio yenye wachezaji wengi zaidi katika orodha hiyo ikiwakilishwa na wachezaji kumi, Brazil ndio wanaofuatia ikiwa na wachezaji tisa, wachezaji nane kutoka Argentina, sita kutoka Uingereza, wanne kutoka ujerumani, Uholanzi na Italia inawakilishwa na wachezaji watatu kila nchi, wawili kutoka Ureno na mchezaji mmoja kutoka nchi za Uruguay, Wales, France, Bulgaria, Serbia, Czech Republic, Sweden, Ghana, Ivory Coast na Cameroon.

Ifuatayo chini ni orodha kamili ya wachezaji 55 walioteuliwa na nchi pamoja na timu wanazocheza katika mabano;

MAKIPA: Gianluigi Buffon (Italy, Juventus FC), Iker Casillas (Spain, Real Madrid C.F.), Petr Cech (Czech Republic, Chelsea FC), Julio Cesar (Brazil, F.C. Internazionale), Edwin van der Sar (Netherlands, Manchester United FC)

MABEKI: Daniel Alves (Brazil, FC Barcelona), Gareth Bale (Wales, Tottenham Hotspur), Michel Bastos (Brazil, Olympique Lyonnais), Ashley Cole (England, Chelsea FC), Patrice Evra (France, Manchester United FC), Rio Ferdinand (England, Manchester United FC), Philipp Lahm (Germany, FC Bayern Munchen), Lucio (Brazil, F.C. Internazionale), Maicon (Brazil, F.C. Internazionale), Marcelo (Brazil, Real Madrid C.F.), Alessandro Nesta (Italy, AC Milan), Pepe (Portugal, Real Madrid C.F.), Gerard Pique (Spain, FC Barcelona), Carles Puyol (Spain, FC Barcelona), Sergio Ramos (Spain, Real Madrid C.F.), Walter Samuel (Argentina, F.C. Internazionale), John Terry (England, Chelsea FC), Thiago Silva (Brazil, AC Milan), Nemanja Vidic (Serbia, Manchester United FC), Javier Zanetti (Argentina, F.C. Internazionale)

VIUNGO: Esteban Cambiasso (Argentina, F.C. Internazionale), Michael Essien (Ghana, Chelsea FC), Cesc Fabregas (Spain, Arsenal FC), Steven Gerrard (England, Liverpool FC), Andres Iniesta (Spain, FC Barcelona), Ricardo Kaka (Brazil, Real Madrid C.F.), Frank Lampard (England, Chelsea FC), Javier Mascherano (Argentina, FC Barcelona), Thomas Muller (Germany, FC Bayern Munchen), Mesut Oezil (Germany, Real Madrid C.F.), Andrea Pirlo (Italy, AC Milan), Bastian Schweinsteiger (Germany, FC Bayern Munchen), Wesley Sneijder (Netherlands, F.C. Internazionale), Xabi Alonso (Spain, Real Madrid C.F.), Xavi (Spain, FC Barcelona)

Wednesday, November 24, 2010

PICHA CHINI ZINAONYESHA MATUKIO MBALIMBALI YA HAFLA FUPI YA UZINDUZI WA MICHUANO YA TUSKER CHALLENGE 2010.

KUTOKA kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) Nicholas Msonye, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo nchini (BMT) Kanali Mstaafu Alhaji Iddi Kipingu, Mkurugenzi wa Mauzo wa Serengeti Breweries Caroline Ndungu na Mkurugenzi wa Mahusiano Teddy Mapunda wakionyesha Kombe la CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP kwa waandishi wa habari katika hafla fupi ya uzinduzi iliyofanyika katika Hotel ya New Africa.

 
Mkurugenzi wa Mahusiano SBL Bi. Teddy Mapunda akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa Kombe la TUSKER CHALLENGE CUP 2010 leo mchana katika Hotel ya New Africa.



 
Meneja wa Kampeni United Against Malaria David Kyne(kulia) akizungumza leo mchana muda mfupi baada ya kuzindua Kombe la TUSKER CHALLENGE CUP 2010 wa pili toka kulia ni Mkurugenzi wa Mauzo SBL Caroline Ndungu akifuatiwa na Bi. Teddy Mapunda, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT) Kanali mstaafu Alhaji Idd Kipingu,pamoja na Katibu Mkuu wa Shirikisho la mpira wa Miguu Afrika Mashariki (CECAFA) Nicholas Msonye.


WAANDISHI kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini wakifuatilia kwa karibu hafla fupi ya uzinduzi wa Kombe la CECAFA TUSKER CHALLENGE CUP 2010.

FABREGAS NJE WIKI TATU.

LONDON, England
KAMARI aliyocheza Kocha wa Arsenal Arsene Wenger kwa kumchezesha nahodha wake Cesc Fabrigas jana usiku ilimrudia baada ya mchezaji huyo baada ya mchezaji huyo kutolewa nje baada ya kujitonesha msuli wa nyuma ya paja katika mchezo ambao timu hiyo ilifungwa mabao 2-0 na Braga.

Mchezaji anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa wiki tatu, na atakosa michezo ya Ligi Kuu wakati timu yake itakapocheza na Aston Villa, Fulham na Manchester United Desemba 13.

Arsenal pia itamkosa mchezaji wake Emmanuel Eboue ambaye ameumia kifundo cha mguu baada ya kukwatuliwa kwa nyuma na Matheus ambaye alifunga mabao yote mawili ya Braga.

"Nimesikitika sana kwasababu nilisita kumchezesha," alikiri Wenger.

"Nilicheza kamari na imenirudia. inaonekana ni kama msuli wa nyuma ya paja kwa hiyo anaweza kuwa nje kwa wiki mbili au tatu."

Wenger aliwabwatukia wachezaji wa Braga kwa mchezo mbaya waliokuwa wakicheza na mwamuzi wa mchezo huo Viktor Kassai kutoka Hungary kwa kumpa kadi ya njano mchezaji Carlos Vela kwa kujiangusha wakati alitakiwa kutoa penati.

Wenger pia alichukizwa na bao la kwanza Braga lilivyopatikana wakati Arsenal ikiwa na watu kumi baada ya Eboue kutolewa nje baada ya kuumia.

"Ni vigumu kuelewa kwanini hatukupata penati," alisema.

Waamuzi watano sio suluhisho la tatizo.

"Tulifungwa wakati Eboue akiwa ameumizwa baada ya kuchezewa vibaya kitndo ambacho hakichukuliwa hatua yoyote na mwamuzi.

""Sehemu ya kurudi mchezoni ni ile penati bado sijaelewa jinsi Carlos Vela alipopewa kadi ya njano. imebakia kuwa kitu kisichoeleweka.

'Mwamuzi alifanya maamuzi ya ajabu usiku huu. Tulicheza na timu ambayo hawakutaka kucheza badala walikuwa wakitumia mipira mirefu ya kushtukiza (counter attack).

"Walifanya kila waliloweza ili kupooza mchezo."

Ingawa Wenger alikiri kuwa timu yake haikutengeneza nafasi nzuri, alidai pia kipigo walichopata dhidi ya Tottenham hakiwaathiri.

BRAGA WASHEHEREKEA KUIFUNGA ARSENAL.

KOCHA wa timu ya soka ya Braga Domingos Paciencia amefurahishwa na timu hiyo baada ya kutoka kifua mbele dhidi ya Arsenal katika mchezo wa Champions League baada ya kushinda mabao 2-0.

Paciencia alishuhudia timu yake ikihangaika kipindi cha kwanza, lakini walijirekebisha na kucheza vizuri kipindi cha pili.

"Niolihisi kama wanashindwa kukaa na mpira katika kipindi cha kwanza," alisema kocha huyo akiuambia mtandao wa UEFA.com. "Tulijua kwamba sio rahisi kucheza na timu kama Arsenal, kwani walikuwa wanataka kumiliki mchezo na tulijitahidi kutafuta nafasi wakati tulipomiliki sisi, ulikuwa mchezo mgumu.

"Mambo yote yalibadilika kipindi cha pili. Timu yangu ilicheza kwa kutulia, walisahau woga wao na kuongeza mashambulizi, kitu ambacho tulikimudu vizuri. Hiyo ndio siri ya ushindi wetu.

Wote sisi pamoja na mashabiki wetu tulistahili ushindi huu. Niloikuwa nategemea usiku huu utakuwa tofauti na nyingine na ilikuwa hivyo kweli.

"Tutaona nini kinaendelea sasa. Chochote kinaweza kutokea. Tunajua kwamba tulianza vibaya, dhidi ya Arsenal na hapa dhidi ya Shakhtar, lakini ni vizuri kuwaonyesha ubora wetu usiku huu." aliongeza Paciencia.

WAAMUZI SCOTLAND WAJIANDAA KUGOMA.

RATIBA za mechi mbalimbali nchini Scotland zinakabiliwa na hatari ya kuvurugika wiki ijayo baada ya waamuzi wa daraja la kwanza kupiga kura kuidhinisha mgomo wao.

Waamuzi hao wa Scotland wamekatishwa tamaa na jinsi wanavyoandamwa msimu huu na hata kutishiwa maisha.

BBC nchini Scotland imegundua kuwa waamuzi wana wasiwasi na pia kushushwa heshima yao na baadhi ya vilabu na hata watu binafsi.

Kumekuwa na ongezeko la vitisho kwa usalama wao kutokana na kuchukiwa na jamii.

Uamuzi wa kugoma ulifikiwa na katika mkutano wa chama cha waamuzi uliofanyika siku ya Jumapili mchana, wengi wakiunga mkono.

Kuna mechi sita za Ligi Kuu ya Scotland zilizopangwa kuchezwa mwishoni mwa wiki ijayo.

STAILI YA ZIDADE YAMSABABISHIA ETO'O KUFUNGIWA MECHI TATU.

MILAN, Italia
MSHAMBULIAJI wa Inter Milan Samuel Eto’o amefungiwa kucheza michezo mitatu ya Ligi ya Italia maarufu Serie A, baada ya kumtwanga kichwa mchezaji wa klabu ya Chievo, Bostjan Cesar.

Wachezaji hao wawili walikumbana katika dakika ya 38 ya mchezo ambapo Inter walilazwa mabao Inter 2-1 na Chievo siku ya Jumapili, baada ya Cesar kurusha ngumi hafifu iliyompata Eto’o usoni.

Eto’o, ambaye tayari ameshafunga mabao 17 msimu huu, aliondoka katika eneo alilorushiwa ngumi, lakini baadae akamgeukia mgomvi wake na kumtwanga kichwa kifuani.

Mwamuzi hakuchukua hatua yoyote kutokana na tukio hilo, lakini Shirikisho la Soka la Italia, limemfungia Eto’o baada ya kupitia ushahidi wa mkanda wa video.

Ligi ya Italia ilishawahi kutumia ushahidi wa video siku za nyuma na walimfungia mshambuliaji wa Fiorentina Alberto Gilardino kucheza michezo miwili baada ya kufunga bao kwa mkono.

Taarifa iliyotolewa na Ligi hiyo ya Italia, Serie A, imesema kichwa alichorusha Eto’o’s ambacho waamuzi hawakukiona, ni shambulio la aibu na ni utovu wa nidhamu usiokubalika.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Cmeroon, ambaye amepigwa faini ya euro 30,000, ataweza kucheza siku ya Jumatano katika mechi ya Ligi ya Ubingwa wa Ulaya dhidi ya FC Twente.

Lakini kufungiwa kucheza mechi tatu za ligi ya Italia, ni pigo kubwa kwa kocha wake Rafael Benitez, ambaye hivi sasa anakabiliwa na wachezaji wengi majeruhi, akiwemo mpachika mabao hatari Diego Milito.

Mabingwa hao watetezi wa Italia, msimu huu wamebanwa baada ya kupoteza mechi kadha na kwa sasa wanashikilia nafasi ya sita ya msimamo wa ligi, pointi tisa nyuma ya mahasimu wao wakubwa , AC Milan.

Taarifa za vyombo vya habari zimekuwa zikidai huenda kocha Rafael Benitez akafutwa kazi ikiwa Inter Milan ambao ni mabingwa watetezi, watapoteza mechi na FC Twente.

Hata hivyo Rais wa klabu hiyo Massimo Moratti amekanusha madai hayo na kusema ataendelea kumuunga mkono Benitez.

Monday, November 15, 2010

"MNAMTWISHA MZIGO MKUBWA TEVEZ," - MANCINI

LONDON, England
KWA mara ya kwanza kocha wa Manchester City, Roberto Mancini, amesema nahodha, Carlos Tevez anabebweshwa mzigo mzito ndani ya kikosi hicho kulinganisha na wachezaji wengine Eastland.

Kocha huyo alimtolea mfano mshambuliaji mwenye miaka 23, Adam Johnson kuongeza kasi baada ya kinda huyo kushindwa kutamba katika mchezo dhidi ya Birmingham licha ya kucheza dakika 90 akichukuwa nafasi ya Tevez.

Mancini alisema, Johnson alishindwa kufunga mabao licha ya kupata nafasi nzuri na alionya Man City itapata ushindi wa kubahatisha ikiwa itamtegemea zaidi Tevez. Mtaliano alisema, Johnson na wachezaji wengine wa timu hiyo wanatakiwa kumsaidia Tevez kufunga mabao na siyo kubweteka.

"Adam Johnson siyo kiungo mkabaji, David Silva siyo kiungo wote ni washambuliaji. Lakini wana wana matatizo tangu kuanza msimu huu, ikiwa carlos hatafunga hakuna mchezaji yeyote anayeweza kufumania nyavu," alisema Mancini.

Mbali ya nyota, hao Man City ilimsajili mshambuliaji chipukizi wa Inter Milan, Mario Balotelli (20) aliyekuwa nje ya uwanja muda mrefu baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu. Man City ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 22 katika msimamo wa ligi.

Kocha huyo amekuwa akipata presha kubwa kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo na wachezaji wakikosoa mbinu zake za ufundishaji. Licha ya kumpa kitambaa cha unahodha Tevez, Mancini anapata shinikizo kwa wadau wa soka wanamtuhumu kutumia mabilioni ya fedha kusajili wachezaji nyota duniani lakini hapati mafanikio.

Mbali ya Balotelli na Silva, baadhi ya nyota waliotumia Eastland msimu huu ni kiungo wa Barcelona, Yaya Toure ambaye ni mdogo wa beki nguli na nahodha wa timu hiyo, Kolo Toure.

BLANC AKIPONDA KIKOSI CHAKE.

PARIS, Ufaransa
KOCHA wa Ufaransa, Laurent Blanc, amesema ni ndoto kwa timu hiyo kufanya maajabu katika mchezo wa soka duniani kwa kuwa kikosi hicho hakina wachezaji mahiri kama zamani.

Badala yake beki huyo wa zamani wa Manchester United alizitaka klabu za Ufaransa kuibua vipaji vipya kutoka mtaani. Blanc, alisema Ufaransa imepoteza mwelekeo baada ya wachezaji wake nguli kustaafu soka na haikuwa na msingi imara baada ya nyota hao kutundika daluga.

Blanc aliyechukua mikoba ya Roy Domenech, alionya Ufaransa inaweza kupoteza dira katika mchezo huo endapo hazitafanyika jitihada za kuibua wachezaji chipukizi wenye vipaji kutoka ngazi ya klabu.

Kocha huyo aliwataja wachezaji Florent Malouda na Franck Ribery hawatakuwa na muda mrefu kabla ya kustaafu soka na kuongeza kuwa anashangazwa kuona hadi sasa hakuna mrithi wa nyota hao. Malouda ni mshambuliaji tegemeo wa Chelsea na Ribery anacheza klabu ya Bayern Munich.

'Tuna wachezaji wachache wanaocheza klabu kubwa za Ulaya ambao bila shaka wanaweza kuibuka kuwa nyota siku za usoni. Lazima tuwe wakweli kama timu inakuwa na vijana watatu au wanne mahiri ni rahisi kupata mafanikio tofauti na ilivyo sasa, kimsingi tupo mbali sana," alisema Blanc.

Ufaransa iliwahi kutwaa Kombe la Dunia 1998 kabla ya mwaka 2000 kunyakuwa taji la Ulaya. Baadhi ya wachezaji waliounda kikosi hicho ni pamoja na nguli, Didier Deschamps, Zinedine Zidane (Juventus) Marcel Desailly (Chelsea), Patrick Vieira, Emmanuel Petit (Arsenal) na Youri Djorkaeff aliyekuwa Inter Milan.

KIBARUA CHA HODGSON MATATANI LIVERPOOL.

LONDON, England
MUDA Mfupi baada ya Liverpool kuchapwa mabao 2-0 na Stoke City, kocha Roy Hodgson amesema hatima ya klabu hiyo ipo nje ya uwezo wake kufuatia mashabiki kumzonga kutaka, Kenny Dalglish arudishwe kuinoa timu hiyo yenye makao makuu Anfield.

Mashabiki wa Liverpool, walichukizwa na kipigo hicho na muda mfupi baada ya mpira kumalizika, walitaka kocha wa zamani, Dalglish aliyeipa ubingwa wa England mara ya mwisho mwaka 1990 kuchukuwa mikoba ya Hodgson.

Mabao yaliyofungwa na Ricardo Fuller na Kenwyne Jones yalitosha kumpa homa Hodgson aliyechukuwa nafasi ya Rafael Benitez aliyetua Inter Milan. Kocha huyo wa zamani wa Fulham alisema anahisi kibarua chake kipo shakani baada ya mashabiki hao kumtaka Dalglish.

"Hakuna nililoweza kufanya hapa, nitaendelea kufanya kazi yangu lakini nitakuwa katika mazingira fulani. Kama klabu itakuwa tayari kumleta kocha mwingine nitakuwa tayari kumkabidhi kazi, mashabiki wananipa presha kubwa sijui nini la kufanya" alisema Hodgson.

Awali, beki wa Liverpool, Glen Johnson alitibuana na Hodgson wiki iliyopita baada ya kukosa mbinu za ufundishaji wa kocha huyo mwenye heshima England. Winga wa zamani wa timu hiyo aliyeitumikia Anfield miaka mitatu kabla ya kutua Stoke City, Jermaine Pennant alisema itakuwa ngumu kwa Liverpool kurejea kiwango cha zamani.

"Mashabiki wanataka kuiona Liverpool ya zamani, siyo jambo rahisi. Wachezaji hawana kiwango bora lakini kuna baadhi yao wanapigana kujilinganisha na wale wa zamani itachukuwa muda. Wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kufikia mafanikio kama ya Chelsea au Manchester United," alisema Pennant.

BALOTELLI AITWA ITALIA.

MILAN, Italia
CESARE Prandelli amemuita mshambuliaji chipukizi wa Chelsea, Mario Balotelli (20) kwa ajili ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Romania uliopangwa kuchezwa kesho nchini Austria.

Balotelli amerejea uwanjani akitokea kwenye maumivu ya upasuaji wa kifundo cha mguu alichoumia muda mfupi baada ya kujiunga na klabu ya Manchester City.

Winga wa Brescia, Alessandro Diamanti, mabeki Andrea Ranocchia wa Genoa, Federico Balzaretti anayecheza Palermo na kiungo nyota wa Lazio, Cristian Ledesma, wameitwa kwa ajili ya mchezo huo. Wachezaji hao walikosa mchezo uliopita dhidi ya Serbia uliochezwa Oktoba 12.

Makipa: Antonio Mirante (Parma), Salvatore Sirigu (Palermo) na Emanuele Viviano kutoka Bologna. Mabeki: Davide Astori (Cagliari), Federico Balzaretti (Palermo), Leonardo Bonucci (Juventus), Mattia Cassani (Palermo), Domenico Criscito (Genoa), Daniele Gastaldello (Sampdoria), Andrea Ranocchia (Genoa) na Davide Santon wa Inter Milan.

Viungo: Alberto Aquilani (Juventus), Daniele De Rossi (AS Roma), Alessandro Diamanti (Brescia), Cristian Ledesma (Lazio), Claudio Marchisio (Juventus), Stefano Mauri (Lazio) na mchezaji mkongwe, Andrea Pirlo anayecheza AC Milan.

Washambuliaji: Mario Balotelli (Manchester City), Alberto Gilardino (Fiorentina), Giampaolo Pazzini (Sampdoria), Fabio Quagliarella (Juventus) na Giuseppe Rossi kutoka Villarreal.

AC MILAN YAICHAKACHUA INTER.

R0ME, Italia
ZLATAN Ibrahimovic amesifu kiwango cha AC Milan ilichoonyesha katika mchezo wa Ligi Kuu Italia ambao timu hiyo ilishinda bao 1-0 dhidi ya mahasimu wao Inter Milan kwenye Uwanja wa San Siro.

Mshambuliaji huyo alifunga bao pekee katika mchezo kwa mkwaju wa penalti dakika 50 ambapo ilishuhudia Inter Milan ikicheza pungufu na wachezaji 10 baada ya beki, Ignazio Abate kulimwa kadi nyekundu.

Ibrahimovic aliyekuwa mfungaji bora alipokuwa Inter Milan kabla ya kutua Barcelona msimu uliopita, alisema walicheza soka ya kiwango bora ili kudhihirisha viwango vya wachezaji wa kikosi hicho ni bora kulinganisha na wapinzani wao.

Mshambuliaji huyo wa Sweden, alisema AC Milan ilicheza soka ya kiwango dakika 45 za mwisho na kuifanya ngome ya Inter Milan kupotea na kuruhusu timu hiyo kuvuna pointi tatu katika mchezo huo uliokuwa na upinzani mkali.

"Ilikuwa mechi ya kihistoria kwangu, hasa kipindi cha pili tulicheza kwa kiwango bora na kila mmoja alitimiza wajibu wake. AC Milan ni timu inayocheza kwa umoja na hilo tumelionyesha katika mchezo huu," alitamba Ibrahimovic.

Mshambuliaji huyo alitumia fursa kumwomba radhi beki mkongwe wa Inter Milan, Marco Materazzi aliyetolewa kwa machela baada ya kuumia akidai tukio hilo lilikuwa bahati mbaya na kuongeza katika mchezo wa soka lolote linaweza kutokea uwanjani.

TERRY HATIHATI KUIVAA UFARANSA

LONDON, England
KOCHA wa England, Fabio Capello atawakosa wachezaji wawili mahiri, Ashley Cole na Gabriel Agbonlahor katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Ufaransa uliopangwa kuchezwa kesho.

Mbali ya wachezaji hao, Capello ana hatihati ya kumtumia nahodha wa zamani wa kikosi hicho, John Terry ambaye kocha, Carlo Ancelotti wa Chelsea amedokeza ana maumivu.

Cole, anayecheza Chelsea na Agbonlahor anayeng'ara Aston Villa, watakuwa jukwaani na nafasi zao zitajazwa na Stephen Warnock wa Aston Villa na Gary Cahill kutoka Bolton.

Licha ya kuzitumikia klabu zao katika mechi za ligi mwishoni mwa wiki, madaktari wameshauri wachezaji hao wasicheze mchezo dhidi ya Ufaransa ili kuepuka majeraha zaidi. Cole, anakabiliwa na maumivu ya kifundo cha mguu na alianza mazoezi siku 10 zilizopita.

Cahill alishituka kuitwa kikosi cha England. Beki huyo wa kati, alimkuna Capello baada ya kuonyesha kiwango bora katika mchezo England ilishinda mabao 4-0 akichukuwa nafasi ya Michael Dawson dhidi ya Bulgaria, Septemba.

ANCELOTTI ABWATUKA.

LONDON, England
CARLO Ancelotti amesema wachezaji wake walicheza ovyo na kuchangia kipigo cha mabao 3-0 ilichopata kwa Sunderland katika mchezo wa Ligi Kuu England uliochezwa juzi usiku Uwanja wa Stamford Bridge.

Mabao yaliyofungwa na Danny Welbeck but Nedum Onuoha dakika 45, Asamoah Gyan (52) na Danny Welbeck, yalizima ndoto za Chelsea kuvuna pointi tatu kwenye Uwanja wake. Licha ya kufungwa, Chelsea imebaki kileleni kwa pointi 28 ikifuatiwa na Arsenal yenye pointi 26.

Ancelotti, alifura kwa hasira na kutamka kuwa wachezaji walicheza kwa kiwango cha chini na kuruhusu wapinzani wao kutawala mchezo huo. Hii ni mara ya kwanza kwa Chelsea kupoteza mchezo kwenye uwanja wake tangu Aprili, 2002.

Kipigo hicho kimetokea wakati Chelsea imemtimua kocha msaidizi, Ray Wilkins. "Hiki ni kiwango cha chini kabisa kuwahi kukiona tangu nilipofika hapa, kila kitu kilikwenda ovyo, hakuna mchezaji yeyote aliyecheza kwa kiwango bora. Sunderland ilicheza soka ya kuvutia na sikutarajia," alisema Ancelotti.

Kocha huyo aliyetua Chelsea mwaka 2009, alisema hakushangazwa Chelsea kupoteza mchezo na alitarajia kipigo hicho kutokana na mchezo wa ovyo walioonyesha vijana wake. Ancelotti, alidokeza hakuwa mkali ndani ya vyumba vya kuvalia nguo kwasababu alitaka kuzungumza na kila mchezaji akiwa kwenye utulivu.

Kocha huyo alisema baada ya kupoteza pointi tatu, atarejea uwanjani kuwapa wachezaji wake mafunzo kwa ajili ya kujiandaa na mchezo unaofuata ambao alidai hataki kuona Chelsea ikivurunda.

Sunday, November 14, 2010

ARSENAL MWENDO MDUNDO, CHELSEA, LIVER ZACHAPWA, MAN UNITED YAKABWA, CHINI NI BAADHI YA MATUKIO YA MECHI ZILIZOCHEZWA WIKIENDI HII.

MCHEZAJI wa timu ya Arsenal Bakari Sagna akishangilia baada ya kuipatia timu yake bao la kuongoza dhidi Everton katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza uliofanyika Jumapili, Arsenal ilishinda mabao 2-1.


KIUNGO wa Arsenal Cesc Fabrigas akifunga bao la ushindi huku mabeki wa Everton wakiokoa bila mafanikio katika mchezo baina ya timu hizo uliochezwa Jumapili.


MCHEZAJI wa timu ya Sunderland maarufu kama Paka Weusi Nedum Onuoha akifunga bao la kuongoza dhidi ya Chelsea huku beki wa timu hiyo Ramires akiangalia katika mchezo wa Ligi Kuu Uingereza uliochezwa Jumapili, Sunderland walifanikiwa kuvunja daraja kwa kushinda mabao 3-0.


MSHAMBULIAJI wa Sunderland Mghana Asamoah Gyan akishangilia baada ya kuipatia timu yake bao la pili dhidi ya Chelsea katika mchezo ulifanyika Jumapili katika Uwanja wa Stamford Bridge.


KOCHA wa timu ya Chelsea Carlo Ancelotti akiangalia huku akiwa hana la kufanya baada ya timu yake ikipoteza mchezo kwa mara ya kwanza nyumbani toka April, 2002 dhidi ya Everton kwa mabao 3-0.


MCHEZAJI wa Aston Villa Marc Albrighton akishangilia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Manchester United, katika Uwanja wa Villa Park, timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.


BEKI wa timu ya Manchester United (aliyelala) akifunga bao la kusawazisha dakika za mwisho na kuikoa timu yake kukosa pointi katika Uwanja wa Villa Park.