MUNICH, German
CHAMA cha Soka nchini Ujerumani (DFB) msimu ujao kitaingiza timu nne kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, kufuatia nchi hiyo kupanda katika viwango vya soka barani Ulaya mbavyo hutolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka barani humo (UEFA) kwa vigezo vya michuano iliyo chini ya UEFA.
Ujerumani wamefikia hatua hiyo baada ya kukamata nafasi ya tatu kwenye viwango vya ubora barani Ulaya sifa ambayo inaifanya nchi hiyo kutoa fursa kwa mshindi wa kwanza wa pili na watatu wa ligi kuingia moja kwa moja katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Ulaya huku mshindi wa nne akianzia katika hatua ya mtoano.
Mshindi wa tano na wa sita katika ligi ya Ujerumani pia watacheza moja kwa moja katika hatua ya makundi la michuano ya ligi ya barani Ulaya ambayo huzishirikisha klabu 64 toka msimu uliopita baada ya utaratibu wa uendeshaji wa michuano hiyo kubadilishwa.
Sababu ya Ujerumani kuingia katika utaratibu huo na kushika nafasi ya tatu katika viwango vya ubora wa soka barani ulaya, ni kufutia ushindi wa klabu za nchi hiyo uliopatikana juma hili ambapo Bayern Munich walifanikiwa kuwachapa Inter Milan bao moja kwa sifuri, Schalke 04 nao wakalazimisha sare ya bao moja kwa moja na Valencia katika mchezo wa ligi ya mabingwa huku Bayer Leverkusen wakifanikiwa kuiondosha Metalist Kharkiv ya nchini Ukraine kwenye michuano ya ligi ya barani ulaya na VfB Stuttgart wakabamizwa na Benfica toka nchini ureno.
Mtendaji mkuu wa DFB Reinhard Rauball amesema wamefurahishwa na hatua hiyo na sasa wanachokitazama mbele ni kukwea zaidi kutoka katika nafasi ya tatu hadi nafasi ya pili na ikiwezekana kuikamata nafasi ya kwanza.
Wakati Ujerumani wakishika nafasi ya tatu, nchi ya Italia yenyewe imeporomoka nafasi moja chini kutoka nafasi ya tatu hadi ya nne kwenye viwango vya ubora duniani, ambapo sasa nchi hiyo itawakilishwa na klabu tatu kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Sababu ya kuporomoka ni kupoteza kwa vilabu vya nchi hiyo katika michuano ya kimataifa ambapo Inter Milan walikubali kisago cha bao moja kwa sifuri kutoka kwa Bayern Munich, Ac Milan nayo ilipoteza kwa Tottenham Hotspurs kwa kukubalia kichapo cha bao moja kwa sifuri huku AS Roma wakachapwa mabao manne kwa matatu Shakhtar Donetsk.
Kama itakumbukwa vyema pia klabu ya Sampdoria ilitolewa na Werder Bremen ya nchini ujerumani katika hatua ya mtoano ili hali katika michuano ya ligi ya barani ulaya klabu ya Napoli, imetolewa baada ya kutandiskwa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Villarreal ya nchini Hispania.
Hii inakua ni mara ya kwanza kwa nchi ya Italia kuporomoka kwa viwango vya ubora wa soka barani ulaya baada ya miaka 12 kupita ambapo kwa mara ya mwisho Italia waliingia katika nchi tatu bora zinazofanya vyema mwaka 1999 kufuatia vilabu vya soka vya nchini humo kutwaa vikombe 13 vya barani ulaya kuanzia mwaka 1990.
Monday, February 28, 2011
NDOTO ZA MAN CITY KUNYAKUWA UBINGWA WA LIGI KUU ZAZIDI KUPEPERUKA BAADA YA KUKUBALI SARE YA 1-1 NA FULHAM.
![]() |
Mchezaji wa Man City Jerome Boateng akichuana vikali na mchezaji wa Fulham Clint Dempsey katika mchezo baina ya timu hizo ulichezwa katika Uwanja wa City of Manchester jana usiku. |
![]() |
Beki wa Fulham Moussa Dembele akijaribu kumdhibiti mshambuliaji wa Man City Edin Dzeko katika mchezo baina ya timu hizo. |
![]() |
Mshambualiaji wa Fulham Damien Duff akishabgilia na Dembele mara baada ya kuipatia timu hiyo bao la kuongoza. |
ARSENAL YAENDELEZA UKAME WA VIKOMBE KWA KUKUBALI KIPIGO CHA 2-1 NA BIRMIGHAM KATIKA FAINALI YA CARLING CUP.
![]() |
Mshambuliaji wa Arsenal Robin van Persie akishangilia sambamba na Samir Nasri na Jack Wilshere mara baada ya mchezaji huyo kuisawazishia bao katika mchezo huo. |
![]() |
Maelfu ya watu wakimiminika katika Uwanja wa Wembley kushuhudia mchezo wa huo wa fainali kati ya Arsenal na Birmigham. |
![]() |
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger akizungumza na kipa wake Szczesny mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo. |
![]() |
Wachezaji wa Arsenal wakishuka mara baada ya kuchukua zawadi zao za ushindi wa pili katika michuano hiyo. |
![]() |
Wachezaji wa birmigham wakishangilia mara baada ya kukabidhiwa Kombe la Carling. |
Saturday, February 26, 2011
MAN UNITED YAICHAKACHUA WIGAN MABAO 4-0 NA KUENDELEA KUJIKITA KILELENI.
BONGO FLEVA WAIRARUA BONGO MOVIE 2-0 KATIKA MCHEZO WA HISANI KUCHANGIA WAHANGA WA MABOMU GONGO LA MBOTO.
![]() |
Kamati ya ufundi ya timu ya Bongo Movie wakifanya vitu vyao kabla ya kuanza kwa mchezo baina ya timu hizo. |
![]() |
Mlinda mlango wa timu ya Bongo Fleva Tunda Man akijaribu kumtoka mshambuliaji wa Bongo Movie Joti katika mchezo baina ya timu hizo ulichezwa katika Uwanja wa Taifa. |
![]() |
Mshambuliaji wa timu ya Bongo Fleva H-Baba akiifungia bao la kuongoza timu yake katika mchezo huo. |
![]() |
Mchezaji mahiri wa Bongo Fleva ambaye ndio alikuwa nyota wa mchezo huo Alikiba akimtoka mchezaji wa Bongo Movie. |
![]() |
Mshambuliaji wa Bongo Movie Ben Kinyaia akipiga tuta ambalo alipaisha juu. |
![]() |
Kikosi kamili cha Bongo Movie. |
![]() |
Kikosi kamili cha Bongo Fleva. |
![]() |
Maelfu ya mashabiki waliojitokeza katika mchezo huo wa hisani kusaidia wahanga wa mabomu Gongo la Mboto. |
Friday, February 25, 2011
HASHEEM THABEET AJIUNGA NA HOUSTON ROCKETS.
HABARI ambazo zimetufikia muda si mrefu uliopita zinapasha kwamba mtanzania wa kwanza kucheza katika ligi ya NBA,Hasheem Thabeet aliyekuwa akichezea timu ya Memphis Grizzlies, ameuzwa kwenda timu ya Houston Rockets ya jijini Houston,Texas katika mabadilishano maalumu baina ya timu hizo mbili.
Katika mabadilishano hayo,mchezaji Shane Battier aliyekuwa akichezea timu anayokwenda Hasheem(Houston Rockets) anajiunga na Memphis Grizzlies.
Maendeleo ya Hasheem katika ligi hiyo ya NBA yamekuwa hayaridhishi.
Read more: HASHEEM THABEET KUJIUNGA NA HOUSTON ROCKETS! - BongoCelebrity

MATOKEO YA UEFA EUROPA LEAGUE HATUA YA 32 BORA AMBAYO IMEKAMILIKA JANA.
Manchester City 3-0 Aris Salonika
Ajax 2-0 Anderlecht (Jumla 5-0)
Bayer Leverkusen 2-0 FC Metalist Kharkiv (Jumla 6-0)
Braga 2-0 Lech Poznan (Jumla 2-1)
Dynamo Kiev 4-0 Besiktas (Jumla 8-1)
FC Twente 2-2 Rubin Kazan (Jumla 4-2)
Liverpool 1-0 Sparta Prague (Jumla 1-0)
Man City 3-0 Aris Salonika (Jumla 3-0)
Paris SG 0-0 BATE Borisov (Jumla 2-2) (PSG ameshindwa kwa golio la ugenini)
PSV Eindhoven 3-1 Lille (Jumla 5-3)
Spartak Moscow 1-1 Basle (Jumla 4-3)
Sporting 2-2 Rangers (Jumla 3-3) (Rangers ameshinda kwa goli la ugenini)
VfB Stuttgart 0-2 Benfica (Jumla 1-4)
Villarreal 2-1 Napoli (Jumla 2-1)
Zenit St Petersburg 3-1 Young Boys (Jumla 4-3)

Thursday, February 24, 2011
FABREGAS, WALCOTT KUKOSA FAINALI CARLING CUP.
LONDON, England
NAHODHA wa Arsenal Cesc Fabregas hatacheza katika mchezo wa fainali ya Carling Cup Jumapili dhidi ya Birmigham kufuatia kuumia nyuma ya kifundo cha mguu katika mchezo dhidi ya Stoke City Jumatano iliyopita.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alithibitisha kukosekana kwa mchezaji huyo kwenye fainali hiyo katika luninga ya timu hiyo Alhamisi jioni, ingawa alisema hadhani kama maumivu hayo yatakuwa ya muda mrefu.
“Ameumia kidogo lakini atakosa mchezo wa Jumapili,” alisema Mfaransa huyo. “Ni kwa muda gani atapumzika kujiuguza sijui lakini nadhani itakuwa kwa Jumapili tu.
“Amehuzunika. Wote tumesikitika juu ya hilo. Njia pekee ya kumsaidia ni kuhakikisha tunashinda hilo taji kwani ametoa mchango mkubwa katika mashindano hayo.
Pamoja na Fabregas kukosa fainali ya Jumapili, Wenger hawezi kutoa chochote kwa kuheshimu nahodha huyo kuwa fiti kwa ajili ya kupambana na Barcelona Machi 8.
“Ni vigumu kutoa tarehe ya mwisho,” alisema Wenger. “Haiwezekani.”
Theo Walcott pia anatarajiwa kukosa mchezo wa Jumapili baada ya kuumia kifundo cha mguu katika mchezo na Stoke, lakini Kocha huyo anaamini kuwa mchezaji huyo hakuumia sana.
“Nilimuona asubuhi hii,” alisema Wenger. “Alipata maumivu ya kifundo cha mguu yasiyo makubwa sana.
Hatufikiri kama kuna lingine zaidi ya hilo. Naye pia tunamsikitikia. Hatakuwepo katika mchezo wa Jumapili na labda wiki moja au mbili mbele.”
"WEMBLEY UKO TAYARI KWA AJILI YA FAINALI KOMBE LA LIGI." MKURUGENZI.
![]() |
Wembley Stadium |
LONDON, England
MKURUGENZI Mtendaji wa Uwanja wa Wembley, Roger Maslin amezihakikishia timu za Arsenal na Birmigham kuwa nyasi katika uwanja huo ziko katika hali nzuri kwa ajili ya mchezo wa fainali wa Kombe la Ligi baina ya timu hizo.
Kumekuwa na minong'ono kuhusiana na ubora wa nyasi, baada ya Kocha wa Man United Sir Alex Ferguson kusema kuwa mchezaji wake Michael Owen aliumia katika Uwanja huo msimu uliopita kutokana na nyasi hizo kuwa chini ya kiwango, wakati Kocha wa Tottenham Harry Redknapp pia alilalamikia suala kama hilo wakati timu yake ilipofungwa na Portsmouth katika Kombe la FA.
![]() |
Wembley kwa ndani. |
"Hakutakuwa na tatizo la kupoteza mipira wala kuteleza kwakuwa kuna mabadiliko yalifanywa katika nyasi hizo." alisema Maslin akiambia BBC Sport.
"CR7 NI WINGA NA MSHAMBULIAJI." MOURINHO.
MADRID, Hispania
KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amekiri kuwa hana uhakika kuwa mchezaji wake Cristiano Ronaldo kama ni winga au mshambuliaji, akiamini kuwa anaweza kumudu nafasi zote vizuri.
Kocha huyo raia wa Ureno aliongea hivyo katika maahojiano na kituo cha Sky Sport, ambapo walikuwa wakiongelea uwepo wa CR7 katika mipango yake, na pia kuhusiana na kuifunga Barcelona nje na ndani.
Akiongea kwa mara ya kwanza kuhusiana na mchezaji huyo, Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Inter alisema, " Tumejaribu kutafuta nafasi inaweza kumfaa Cristiano, na siku zote kunakuwa na mdahalo katika hilo. Ni mshambuliaji? Sidhani. Nafikiri ni mchezaji aneyeweza kupamba na moja kwa moja na adui.
"Ni Winga? Hapana, kwasababu pia mfungaji na kama ni winga ni magoli mangapi unaweza kufunga katika msimu? nafikiri ni mchanganyiko wa vitu vyote hivyo viwili. Yuko fiti na amekomaa kama mchezaji. Ana kila kitu."
Kocha huyo pia aliongelea jinsi wachezaji wake walivyochulia kipigo cha mabao 5-0 na barcelona, na alikiri kuwa ingawa ilikuwa ni vigumu kuondoa kichwani tukio lile lakin i wachezaji wake walifanikiwa kuliondoa tukio lile vichwani mwao.
"Kila mtu alikuwa amepagawa, nakumbuka katika mchezo uliofuata dhidi ya Valencia, siwezi kusema kwamba watu walikuwa wanaogopa, lakini walikuwa hawajiamini. Ni jambo la kawaida baada ya kipigo kama kile, lakini wachezaji walifanikiwa kushinda hilo.
"Tunahitaji kuendelea kushinda kama tunavyofanya hivi sasa. Msimu huu tuna kundi la vijana wadogo katika historia ya klabu hii, na naamini kuwa tunafanya vizuri ingawa tunahitaji kushinda chochote."
Mwisho, wakati akiulizwa kama atamaliza mkataba wa miaka minne akiwa Santiago Bernabeu hakuwa na majibu kuhusu hilo, alisema "Sijui. Niliipenda Chelsea, na wakati nikiwa London nilikuwa nafuraha. Nilifikiri nitakuwa pale kwa maisha yangu yote, na miiezi michache nikaondoka. Hivyo siwezi kujua. kama kila kitu kitakwenda sawa nitabaki.
KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amekiri kuwa hana uhakika kuwa mchezaji wake Cristiano Ronaldo kama ni winga au mshambuliaji, akiamini kuwa anaweza kumudu nafasi zote vizuri.
Kocha huyo raia wa Ureno aliongea hivyo katika maahojiano na kituo cha Sky Sport, ambapo walikuwa wakiongelea uwepo wa CR7 katika mipango yake, na pia kuhusiana na kuifunga Barcelona nje na ndani.
Akiongea kwa mara ya kwanza kuhusiana na mchezaji huyo, Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Inter alisema, " Tumejaribu kutafuta nafasi inaweza kumfaa Cristiano, na siku zote kunakuwa na mdahalo katika hilo. Ni mshambuliaji? Sidhani. Nafikiri ni mchezaji aneyeweza kupamba na moja kwa moja na adui.
"Ni Winga? Hapana, kwasababu pia mfungaji na kama ni winga ni magoli mangapi unaweza kufunga katika msimu? nafikiri ni mchanganyiko wa vitu vyote hivyo viwili. Yuko fiti na amekomaa kama mchezaji. Ana kila kitu."
![]() |
CR7 |
"Kila mtu alikuwa amepagawa, nakumbuka katika mchezo uliofuata dhidi ya Valencia, siwezi kusema kwamba watu walikuwa wanaogopa, lakini walikuwa hawajiamini. Ni jambo la kawaida baada ya kipigo kama kile, lakini wachezaji walifanikiwa kushinda hilo.
"Tunahitaji kuendelea kushinda kama tunavyofanya hivi sasa. Msimu huu tuna kundi la vijana wadogo katika historia ya klabu hii, na naamini kuwa tunafanya vizuri ingawa tunahitaji kushinda chochote."
Mwisho, wakati akiulizwa kama atamaliza mkataba wa miaka minne akiwa Santiago Bernabeu hakuwa na majibu kuhusu hilo, alisema "Sijui. Niliipenda Chelsea, na wakati nikiwa London nilikuwa nafuraha. Nilifikiri nitakuwa pale kwa maisha yangu yote, na miiezi michache nikaondoka. Hivyo siwezi kujua. kama kila kitu kitakwenda sawa nitabaki.
"TIMU INA NAFASI YA KUTINGA ROBO FAINALI CHAMPIONS LEAGUE PAMOJA NA KUTOA SULUHU NYUMBANI." DESCHAMPS.
MARCEILLE, Ufaransa
KOCHA wa Marceille Didier Deschamps amesema kuwa Man United bado itakuwa timu inayopigiwa chepuo la kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Champions league hata baada ya kutoa suluhu katika mchezo wa kwanza uliochezwa Stade Velodrome.
Pamoja na kwamba United ilishindwa kupata bao la ugenini katika mchezo huo, Deschamps alieleza wasiwasi wake huo kuwa anadhani timu hiyo ndio inayopigiwa chapuo la kusonga mbele lakini alisisitiza suluhu hiyo sio matokeo mabaya kwa timu yake.
Wakati akihojiwa na Luninga ya ITV Sport kuhusiana na timu gani anadhani inapewa nafasi ya kusonga mbele kufuatia matokeo hayo ya suluhu alisema, "Nafikiri ni Man United. Sio matokeo mabaya kwetu, lakini ni matokeo mazuri kwa Man United.
Kocha huyo pia alisisitiza kuwa anajivunia kikosi chake na anaamini kuwa hakitatoa nafasi kwa United kupata bao kama wanataka kuwatoa katika michuano hiyo.
"Nimefurahishwa na wachezaji wangu kwasababu nafikiri walicheza vizuri," alisema Deschamps.
"Itakuwa ni muhimu katika marudiano Old Traford kutokubali kufungwa tena na labda tukipata nafasi ya kufunga tuitumie."

Monday, February 21, 2011
GATUSSO AFUNGIWA MECHI NNE UEFA.
MILAN, Italia
SHIRIKISHO la Soka Barani Ulaya (UEFA) limemfungia mchezaji wa AC Milan Gennaro Gatusso mechi nne baada ya kufanya vurugu katika mchezo wa Champions League dhidi ya Tottenham Hotspurs wiki iliyopita katika Uwanja wa San Siro.
Gatusso alikutwa na kosa baada ya kumsukuma Kocha Msaidizi wa Spurs mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo wa hatua ya mtoano.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 33 tayari alikuwa amepewa kadi nyekundu na alitakuwa akose mchezo wa marudiano katika Uwanja wa White Hart Lane, kwa maana hiyo atakosa michezo mitano ya Ulaya.
Mchezaji huyo hataweza kucheza katika mashindano hayo tena msimu huu labda kama timu yake hiyo itafikia hatua ya fainali. Kama haitakuwa hivyo adhabu itaendelea katika msimu ujao wa 2011-2012.
KALUSHA BWALYA AJIPIGIA DEBE KATIKA UCHAGUZI CAF.
LONDON, England
HOFU kubwa imetanda kwenye kambi Kalusha Bwalya ambae anawania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya shirikisho la soka barani Afrika CAF katika ukanda wa kusini mwa bara la Afrika.
Hofu hiyo imezuka huku zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya kufanyika kwa uchaguzi huko mjini Khartoum nchini Sudan ambapo Bwalya ametoa angalizo kwa wapiga kura kwa kuwaeleza kwamba wanatakia kutazama namna ya kuendeleza soka ndani ya ukanda huo.
Bwalya ambae alikua mchezaji bora wa barani Afrika mwaka 1988 amesema endapo wajumbe watashindwa kumchagua mtu sahihi kuna uwezekano mkubwa wa soka la ukanda wa kusini mwa bara la Afrika likaendelea kudumaa kama ilivyo sasa ambapo hali hiyo inasababishwa na utawala mbovu ambao hautakiwi kuvumiliwa hata kidogo.
Amesema kimtazamo ukanda wa kusini mwa bara la Afrika ndio kuna wagombea wengi kuliko ukanda wowote wa barani humo hivyo busara na maamuzi ya haki ndio vinavyotakiwa siku ya upigaji wa kura.
Wanaowania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji wa CAF katika ukanda wa kusini mwa bara la Afrika ni Adam Mthetwa (Swaziland), John Muinjo (Namibia), Justino Fernandes (Angola), Walter Nyamilandu (Malawi) Suketu Patel (Sheli sheli) pamoja na Kalusha Bwalya (Zambia)
Kalusha Bwalya pia anawania nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji ya FIFA kutoka ukanda huo ambapo katika sehemu hii atapambana na Danny Jordaan (Afrika Kusini) pamoja na Suketu Patel (Sheli sheli).
Katika ukanda wa magharibi mwa Afrika upande B, nafasi ya kamati ya ujumbe ya CAF inawaniwa na Kwesi Nyantakyi (Ghana), Anjorin Moucharafou (Benin) pamoja na Hima Souley (Niger).
Ukanda wa kaskazini mwa bara la Afrika nafasi hiyo inawaniwa na Tarek Bouchamaoui (Tunisia) huku Almamy Kabele Camara akiwania nafasi hiyo kwenye ukanda wa Afrika ya Magharibi upande A.
Katika ukanda wa Afrika ya kati Omari Selemani (Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo) yeye anajiandaa kumrithi Thierry Kamach (Jamuhuri ya Afrika ya kati) huku ukanda wa Afrika ya mashariki nafasi hiyo inawaniwa na Leodegar Tenga (Tanzania ) pamoja na Celestin Musabyimana ( Rwanda).

"SIJIUZULU NG,O." ANCELOTTI.
LONDON, England
KOCHA wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti amekataa kujiuzulu na badala yake ametangaza kuiweka hatma yake mikononi mwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.
Ancelotti amegoma kujiuzulu nafasi ya umeneja klabuni hapo kufuatia mambo kuendelea kuwa mabaya kwa upande wake huku mashabiki wakimtaka awaachie klabu yao na kurejea nyumbani nchini Italia.
Msimamo wa kutokua tayari kujiuzulu, umetolewa na meneja huyo kwenye mkutano na waandishi wa habari ambapo amesema hafikirii kufanya hivyo kwani bado anaona kuna nafasi ya kuiwezesha Chelsea kufanya vyema katika michuano waliyosalia.
Shinikizo kwa Ancelotti la kuondoka klabuni hapo kutoka kwa mashabiki limejitokeza mara baada ta kikosi chao kushindwa kusonga mbele katika michuano ya kombe la FA baada ya kukubalia kisago kutoka kwa Everton kupitia changamoto ya mikwaju ya penati 4 dhidi ya 3.

AS ROMA YAMTENGEA NAFASI ANCELOTTI.
![]() |
Aliyekuwa Kocha wa AS Roma Claudio Ranieri ambaye kibarua chake kimeota nyasi hivi karibuni. |
ROMA, Italia
UONGOZI wa klabu ya AS Roma umemuingiza meneja wa sasa wa klabu ya Chelsea Carlo Ancelotti kwenye mipango ya kukirihthi kiti kilicho wazi klabuni hapo.
Uongozi wa klabu ya AS Roma umemuweka Carlo Ancelotti kwenye mikakati hiyo kufuatia hali mbaya inayomkabili kwa sasa huko Stamford Bridge baada ya kikosi chake kusalia na ndoto za kutwaa ubingwa wa michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya pekee msimu huu.
Katika kuhakikisha utaratibu huo hauharibu mipango ya Anceloti kwenye maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya, Uongozi wa AS Roma tayari umeshamteua Vincenzo Montella kuwa meneja wa muda, ambapo kibarua hicho atakishikilia hadi mwishoni mwa msimu huu, huku shughuli yake ya kwanza ikitarajiwa kuwa siku ya jumatano katika mchezo wa ligi dhidi ya Bologna huko Stadio Dall'Ara.
Wakati mipango hiyo ikipangwa huko mjini Roma nchini Italia, huko London nchini Uingereza mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich hii leo alitarajiwa kufanya mazungumza na John Terry pamoja na Branislav Ivanovic kwa ajili ya kufahamu nini kinachopelekea mwenendo mbovu ndani ya kikosi chao.
Kama itakumbukwa vyema mapema hii leo meneja wa klabu ya Chelsea Ancelotti amekataa kujiuzulu na badala yake akatangaza kuiweka hatma yake mikononi mwa mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich.
Msimamo huo wa kutokua tayari kujiuzulu, ameutoa akiwa safarini kuelekea mjini Copenhagen nchini Denmark tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya 16 bora dhidi ya FC Copenhagen ya nchini Denmark.

"MODRIC IS NOT FOR SALE," REDKNAPP.
![]() |
Luka Modric |
KOCHA wa klabu ya Tottenham Hotspurs Harry Redknapp amesema hatomuuza kiungo Luka Modric ambaye kwa sasa anahusishwa na taarifa za kuwa mbioni kusajiliwa na klabu ya Man Utd.
Harry Redknapp amekataa kuingia kwenye biashara ya kumuuza kiungo huyo kufuatia uvumi unaomuhusu yeye kuwa tayari kufanya hivyo kuendelea kushamiri kwenye vyombo mbali mbali vya habari ambapo amesema uvumi huo ni mzushi mtupu.
Alisema hata yeye amekua akizisikia taarifa hizo za Luka Midric kuwa mbioni kuuzwa na klabu yake huku ikielezwa tayari dau la paund million 35 limeshatengwa kwa ajili ya safari yake ya kuelekea huko Old Trafford yalipo makao makuu ya klabu ya Man Utd.
Alisema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 amekua na maendeleo mazuri ndani ya kikosi chake toka aliposajiliwa huko White Hart Lane mwaka 2008 akitiea kwenye klabu ya Dynamo Zagreb hivyo haoni sababu ya kulazimika kumuondoa kwa sasa wakati bado Spurs inamuhitaji.
Redknapp akaendelea kumsifia mchezaji huyo kwa kusema ni msikivu na wala hapendi makuu, zaidi ya kutaka kucheza soka wakati wote hali ambayo inamfanya apendwe na wachezaji wenzake kila kukicha klabuni hapo.
Taarifa zinazoelezwa kwenyo vyombo mbali mbali vya habari huko nchini Uingereza ni kwamba Luca Modric anapigiwa upatu wa kusajiliwa na klabu ya Man Utd kwa lengo la kuziba nafasi itakayoachwa wazi na Paul Scholes.
"TUMEJIONGEZEA MCHEZO USIO WA LAZIMA." WENGER.
LONDON, England
SIKU moja baada ya kung’ang’aniwa na klabu ya Leyton Orient kwa kulazimishwa sare ya bao moja kwa moja kwenye mchezo wa michuano ya kuwania ubingwa wa kombe la chama cha soka nchini Uingereza FA, meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Charles Ernest Wenger amesema matokeo hayo yamewalazimisha kujiongezea mchezo ambao ulikua hauna ulazima wa kuwepo.
Wenger amesema mchezo huo umewaongezea michezo zaidi ya ile wanayoifikiria kwa sasa kutokana na sheria ya michuano ya kombe la FA kuwalazimisha kucheza tena dhidi ya Leyton Orient huko Emirates kwa lengo la kumsaka mshindi atakaetinga kwenye hatua ya robo fainali.
mzee huyo pia amebainisha kwamba kiujumla kikosi chake kilicheza kwa kujituma wakati wote lakini makosa madogo madogo waliyoyafanya dakika za lala salama yaliwagharimu na kutoa nafasi kwa wapinzani wao kusawazisha kupitia kwa Jonathan Kahne Téhoué.
Hata hivyo Arsene wenger amekimwagia sifa kede kede kikosi cha Leyton Orient kufuatia kuonyesha soka safi na lenye kutokatisha tamaa licha ya upande wa Arsenal kupata bao katika dakika za mwanzo za kipindi cha pili lililofungwa na Thomas Rosicky.

GUARDIOLA KUONGEZEWA MKATABA BARCA.
![]() |
Pep Guardiola |
LONDON,England
”KOCHA wa Barcelona Pep Guardiola anatarajiwa kuongeza mkataba wa mwaka mmoja na klabu hiyo Jumatano alisema mmoja wa viongozi wa klabu hiyo.
Ilitangazwa mapema mwezi huu kuwa Guardiola atasaini mkataba mpya Jumanne lakini sasa imerudishwa nyuma kwa masaa 24.
“Mapema ilitangazwa kuwa kocha huwa natakiwa kusaini mkataba wake mpya Jumanne Februari 22, lakini sasa imeamualiwa kuwa atasaini mkataba huo Jumatano Februari 23, baada ya mazoezi ya timu hiyo,” ilisema taarifa katika mtandao wa klabu hiyo.
“Guardiola atasaini mkataba mwingine wa mwaka mmoja mpaka Juni 30,2012, ilitangazwa Februari 8.”
Guardiola (40) alichukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo mwaka 2008 na tayari ameiwezesha klabu hiyo kushinda mataji 8. Ambapo alieleza nia yake ya kuendelea kuinoa klabu hiyo mwezi Januari, na uongozi wa Barca ulitoa taarifa ya kumuongeza mkataba mapema Februari.
“Kwa kocha, baada ya kipindi fulani mambo kama hayo yanakuwa ya kawaida kwake na wakati huo ukifika lazima ujue jinsi ya kuepukana nayo,” alisema Guardiola. “Lakini bado muda mwingi umebakia katika mkataba wangu na klabu inajua siwezi kuwaacha, hivyo naomba nifanhye kazi yangu kwa amani.”
VILLA SQUARD YAFANIKIWA KUREJEA KATIKA LIGI KUU BARA.
TIMU ya Villa squad yenye makazi yake jijini Dar es Salaam imefanikiwa kurejea katika Ligi kuu ya soka Tanzania baada ya kutoka suluhu na timu ya Prisons ya Mbeya katika mchezo wa Ligi ya Daraja la Kwanza uliofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Villa Squad imefikisha pointi 12 sambamba na Polisi Morogoro, lakini timu hiyo ya Magomeni iliyoshuka daraja mwaka 2009, inafaida ya tofauti ya magoli, ambapo ina magoli 12 ya kufunga dhidi ya magoli 8 ya Polisi Moro.
PATRICE EVRA AONGEZEWA MKATABA MAN UNITED.
LONDON,England
The 29-year-old has already helped United land three Premier League titles, a Champions League, plus three League Cups - the last of which he lifted after skippering the team to victory over Aston Villa last year.
And, with his future now secure, Evra is adamant his desire for silverware has not been satisfied yet.
"Ever since I arrived at United, it's been a dream come true playing here," he said.
"The fans, the players, the manager and the staff all work hard to make this club the best in the world.
"I have won a lot in the last five years, but I want to win more and I know that's the mentality of everyone her
is links to Monaco will make him a target amongst the Marseille support when United head to the south of France for Wednesday's Champions League encounter with Didier Deschamps' men.
But Sir Alex Ferguson has no fears about Evra handling the abuse and, at a time when the most experienced members of his squad are beginning to end their careers, reckons the defender's influence will become more apparent.
"Patrice is unquestionably one of the world's best left-backs," said the Scot.
"He has developed into a key character in the dressing room and it is great that he has committed himself to the club.
FA CUP REVIEW - SUN 20TH FEB.
LONDON, England
Two headers either side of half-time from Manchester City midfielder Patrick Vieira and late efforts from Carlos Tevez, Edin Dzeko and Micah Richards disposed of Notts County in their FA Cup fourth-round replay at Eastlands.
Vieira, a four-time FA Cup winner with Arsenal, struck in the 37th and 58th minutes before substitute Tevez, Dzeko and Richards finished things off in the final six minutes.
County had dominated early on, hitting a post through Karl Howley, but the Barclays Premier League side upped their game to run out comfortable winners.
VOLLEY HOME
Ivan Klasnic's second FA Cup goal in four days secured Bolton Wanderers a 1-0 victory over Fulham and a quarter final trip to Birmingham City.
The Croatian striker scored the winner in Wednesday's fourth-round replay against Wigan Athletic and he was on hand again here to volley home from 12 yards.
Fulham welcomed Bobby Zamora back into action after five months out with a broken leg but they could not find a breakthrough in a fractious encounter at Craven Cottage.
LATE RALLY
Leyton Orient handed Arsenal a reality check as the League One side battled to a famous 1-1 draw in their FA Cup fifth-round tie at Brisbane Road.
The Gunners made 10 changes from the side which had beaten Barcelona in midweek, but lacked a cutting edge in attack before they eventually made the breakthrough when Tomas Rosicky headed in on 53 minutes.
However, Orient produced a late rally and earned themselves a replay when substitute Jonathan Tehoue drilled home with a minute left to keep alive the dream of a quarter-final at Manchester United.
SUNDAY'S FA CUP RESULTS
Manchester City 5-0 Notts County
Fulham 0-1 Bolton Wanderers
Leyton Orient 1-1 Arsenal
Fulham 0-1 Bolton Wanderers
Leyton Orient 1-1 Arsenal
Wednesday, February 16, 2011
DAVIES MOSHA ATUA UINGEREZA KUJARIBU KUWASHAWISHI SOL CAMPBELL NA JOHN CAREW KUICHEZEA YANGA.
TOTTENHAM HOTSPURS YAICHAPA AC MILAN CHAMPIONS LEAGUE.
![]() |
Peter Crouch akifunga bao la ushindi dhidi ya AC Milan jana usiku katika Uwanja wa San Siro, Milan. |
![]() |
Wachezaji wa Tottenham wakishangilia bao pekee lilifungwa na Crouch dhidi ya AC Milan jana usiku. |
![]() |
Mchezaji wa Tottenham Corluka akigaragara chini baada ya kuchezewa vibaya na Flamini wa AC Milan jana usiku. |
![]() |
Mchezaji wa AC Milan Gattuso akigombana na kocha msaidizi wa Tottenham Joe Jordan wakati timu hizo zilipokutana jana usiku. |
RONALDO LUIS NAZARIO DE LIMA ATUNDIKA DARUGA.
LONDON, England
Mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Ronaldo Luis Nazario de Lima hii leo ametangaza rasmi kustahafu soka baada ya kuutumikia mchezo huo kwa muda wa miaka 24 iliyopita.
Mshambuliaji huyo anaeshikilia rekodi ya kupachika mabao mengi kuliko mchezaji yoyote aliewahi kucheza fainali za kombe la dunia toka ziazishwe mwaka 1930, amefikia maamuzi ya kustahafu soka kwa sababu mbili tofauti ambapo sababu ya kwanza ni kutaka kupata muda wa kufanya shughuli nyingine za kimaisha ambazo amedhamiria kuzifanya.
Amesema muda mrefu amekua akiutumikia mchezo wa soka pasipo kujishughulisha na shughuli za kimaisha ambazo kwa kipindi kirefu amekua akizifanya kwa kujiibia muda wake na kwa sasa ameona muda umefika kuingia katika utaratibu huo moja kwa moja.
Sababu ya pili amedai ni kuzidiwa na mwili ambao kwa sasa ni mkubwa zaidi ya alivyokua siku za nyuma.
Hata hivyo ameeleza kwamba bado ana mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu yake ya sasa ya Corinthians ya nchini Brazil ambayo ilimsajili kutoka Ac Milan ya nchini Italia mwaka 2009 lakini ameona ni bora akae pembeni na kutoa nafasi kwa wachezaji wengine kuonyesha uwezo wao.
Ronaldo Luis Nazario de Lima ambae amepachikwa majina mengi kama R9, The Phenomenon pamoja na The Big ataendelea kukumbukwa kwa uwezo wake binafsi wakati alipokua akivitumikia vilabu kama Cruzeiro, PSV, Barcelona ,Inter Milan, Real Madrid, AC Milan na Corinthians ambao ulimuwezeshwa kutwaa tuzo ya uchezaji bora dunia mara tatu ambapo hiyo ilikua mwaka 1996, 1997, 2002.
Akiwa na timu ya taifa ya Brazil kuanzia mwaka 1994–2006 alifanikiwa kucheza michezo 97 na kupachika mabao 62 huku akitwaa ubingwa wa dunia mara mbili mwaka 1994 na mwaka 2002.
HIZI NDIO TUZO ALIZOFANIKIWA KUTWAA WAKATI WA UCHEZAJI WAKE.
* Supercopa Libertadores Top Scorer: 1993–94
* Campeonato Mineiro Top Scorer: 1993–94
* Campeonato Mineiro Team of The Year: 1994
* Eredivisie Top Scorer: 1994–95
* La Liga Top Scorer: 1996–97,2003–2004
* European Golden Boot: 1996–97
* Don Balón Award La Liga Foreign Player of the Year: 1996–97
* Copa América Final Most Valuable Player: 1997
* Copa América Most Valuable Player: 1997
* Confederations Cup All-Star Team: 1997
* Cup Winners Cup Final Most Valuable Player: 1997
* Cup Winners Cup Top Goal Scorer: 1996–1997
* IFFHS World's Top Goal Scorer of the Year: 1997
* UEFA Most Valuable Player: 1997–98
* Serie A Footballer of the Year: 1997–98
* Serie A Foreign Footballer of the Year: 1997–98
* UEFA Best Forward: 1997–98
* Bravo Award : 1995, 1997, 1998
* FIFA World Cup Golden Ball: 1998
* UEFA Cup Final Most Valuable Player: 1998
* Copa América Top Scorer: 1999
* Copa América All-Star Team: 1997, 1999
* FIFA World Player of the Year: 1996, 1997, 2002
* Ballon D'or: 1997, 2002
* World Soccer Magazine World Player of The Year: 1996,1997.2002
* Onze d'Or: 1997, 2002
* FIFA World Cup Silver Ball: 2002
* FIFA 100
* FIFA World Cup All-Star Team: 1998, 2002
* FIFA World Cup Final Most Valuable Player: 2002
* FIFA World Cup Top Scorer: 2002
* Intercontinental Cup Most Valuable Player: 2002
* UEFA Team of The Year: 2002
* Laureus Comeback of the Year: 2002
* Strogaldo De Legendary Award 2002
* BBC Sports Personality of the Year Overseas Personality: 2002
* La Liga South American Player of the Year: 1996–97, 2002–03
* Golden Foot award: 2006
* Brazilian National Hall of Fame: Class of 2006
* Serie A Player of the Decade: 1997–2007
* France Football Magazine: Starting eleven of all-time (2007)
* FIFA World Cup: All-Time Leading Scorer
* Campeonato Paulista: Best Player, 2009
* Goal.com : Player of a decade: Winner 2000–2010[27]
Subscribe to:
Posts (Atom)