Wednesday, October 27, 2010

GOLIKIPA WA MAN CITY JOE HART AKIJIACHIA BAADA KIPIGO WALICHPATA KUTOKA KWA ARSENAL.

PWEZA PAUL AFARIKI DUNIA.

PWEZA maarufu aliyekuwa akitabiri mechi za michuano ya Kombe la Dunia, ajulikanaye kama Paul amefariki dunia.


Mbali na kutabiri kwamba Hispania itaifunga Uholanzi katika mchezo wa fainali, Paul pia alitabiri kwa usahihi michezo saba ambayo timu ya Ujerumani ilicheza katika michuano hiyo. Kiwango ambacho kiliongezeka ikilinganishwa na rekodi yake ya kawaida, ambayo alitabiri matokeo yaliyo sahihi manne ya michuano ya Ulaya 2008.


Baada ya michuano hiyo iliyofanyika Afrika Kusini, Pweza huyo alitabiri Uingereza itakuwa nchi ambayo itandaa michuano ya Kombe la Dunia 2018, kabla ya kurudia katika kazi yake ya kawaida katika kituo cha Sea Life Oberhausen Aquariuam, Ujerumani.


"Uongozi na wafanyakazi wa kituo cha Oberhausen Sea Life walishtushwa baada ya kugundua Pweza Paul ambaye alijizolea umaarufu mkubwa duniani katika KOmbe la Dunia, kwamba alifariki dunia usiku," ilisema taarifa ya aquarium.

Tuesday, October 26, 2010

FIFA YATEUA MAJINA YA WATAKAOGOMBEA TUZO YA MCHEZAJI BORA.

ZURICH, Switzerland
SHIRIKISHO la Soka la Dunia (FIFA) limetangaza majina ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa dunia na makocha watakaowania tuzo kama hiyo pamoja na tuzo zingine ambazo zitakabidhiwa kwa mashujaa hao wa michezo kwa mchango wao.

Washindi watatangazwa Januari 10, 2011 mjini Zurich. Tuzo hizo zitajumuisha kwa mara ya pili tuzo ya FIFA ya Puskas kwa goli zuri na tuzo ya FIFA Fair Play itakuwa mojawapo kwa timu na mchezaji mmoja mmoja.

Orodha ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Dunia imejumuisha wale waliofanya vizuri katika Kombe la Dunia lilifanyika Afrika Kusini. Majina ya Mabingwa wa kombe hilo Hispania na Germany ambao walifika nusu fainali ndio yako mengi katika orodha hiyo.

Majina ya wachezaji hao na nchi zao katika mabano ni pamoja na
 
 

Xabi Alonso
(Spain)
 Dani Alves
(Brazil)
Iker Casillas
(Spain)
 Cristiano Ronaldo
(Portugal)
Didier Drogba
(Ivory Coast)
 Samuel Eto'o
(Cameroon)
Cesc Fabregas
(Spain)
 Asamoah Gyan
(Ghana)
Julio Cesar
(Brazil)
 Miroslav Klose
(Germany)
Philipp Lahm
(Germany)
 Maicon
(Brazil)
Thomas Mueller
(Germany)
 Arjen Robben
(Netherlands)
Bastian Schweinsteiger
(Germany)
 David Villa
(Spain)
Xavi
(Spain)
 Carles Puyol
(Spain)
Andres Iniesta
(Spain)
 Diego Forlan
(Uruguay)
Lionel Messi
(Argentina)
 Mesut Oezil
(Germany)
Wesley Sneijder
(Netherlands)
  

 

Majina ya makocha kumi na vilabu wanavyofundisha ni pamoja na

Carlo Ancelotti
(Chelsea)
 Vicente del Bosque
(Spain)
Alex Ferguson
(Manchester United)
 Pep Guardiola
(Barcelona)
Joachim Loew
(Germany)
 Jose Mourinho
(Inter & Real Madrid)
Oscar Tabarez
(Uruguay)
 Louis van Gaal
(Bayern Munich)
Bert van Marwijk
(Netherlands)
 Arsene Wenger
(Arsenal)

Monday, October 25, 2010

GUARDIOLA AMVULIA KOFIA MOURINHO.

BARCELONA, Hispania
KOCHA wa Barcelona Pep Guardiola amedai kuwa mpinzani wake Jose Mourinho anaweza kuwa kocha bora katika dunia, na kwamba Real Madrid "wana timu nzuri".

Kocha huyo alikuwa akijibu maswali leo kuhusu mechi inayowakabili ya Copa del Rey utakaochezwa Jumanne jioni dhidi ya AS Ceuta wakati alipoulizwa maoni yake kuhusu Mourinho, na jinsi gani alivyoitengeneza timu yake.

Guardiola alisema: "Pengine ni kocha bora duniani. Mara nyingi ni vigumu kuamua katika kesi hizi kwamba ni nani bora, lakini kazi yake katika nchi kadhaa ni safi. Real Madrid wana timu nzuri, na mimi nilijua kuwa ligi ya msimu huu itakuwa na ushindani kutoka mchezo wa kwanza. Tunatarajia tutajitahidi kuwa juu. "

Bosi huyo baada ya hapo alihamishia maongezi katika mchezo wao huo unaokuja dhidi ya timu hiyo ya daraja la pili ambayo imepakana na pwani ya Afrika Kaskazini, na kuwa na waiswasi jinsi gani mchezo huo unavyoweza kuwa mgumu kama wachezaji wake wasipokuwa makini.

Aliendelea: "Hatutakiwi kuwa wavivu. Nina imani kubwa katika timu, na tuna nia ya kushindana. Kuna wachezaji katika kikosi wenye sifa kamilifu kwa ajili ya mchezo huu. Tunahitaji miguu safi na kuna wachezaji ambao wana desturi ya kucheza mechi dhidi ya timu za Sirie B na kushuka chini. Unaweza kuwa sio mchezo muhimu kwao, lakini ni mchezo hatari kwetu.

"Timu yetu kamwe huwa hatuwadharau wapinzani wetu, na hatuwezi kufanya hivyo kwa Ceuta, ambapo kuna mashabiki wengi wa Barcelona. Naelewa kwamba wanataka kuwaona Xavi [Andres] Iniesta au Leo [Messi], lakini hii timu ina wachezaji wengi wazuri. "

PELLEGRINI: ULIKUWA NI UAMUZI MGUMU KUMUACHA RAUL.

VALPARAISO SANTIAGO, Chile
KOCHA wa zamani wa Real Madrid Manuel Pellegrini amezungumzia magumu aliyokutana kuhusu kumwanzisha mshambuliaji mkongwe katika kikosi chake katika kipindi alichukuwa akifundisha klabu hiyo.

Kocha huyo raia wa Chile alikuwa na wakati mgumu msimu uliopita wakati timu ilipomaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Barcelona kwa mwaka wa pili, na kuchukua majukumu ya kumuacha mchezaji huyo katika kikosi hicho, zaidi kwa ajili ya maendeleo ya klabu hiyo.

Hatahivyo, katika mahijiano yake na gazeti moja la Chile, bosi huyo wa zamani wa Villareal alisema kwamba ilikuwa ni lazima kumuacha ingawa kulikuwa na mawazo tofauti, na pia alifurahia kufanya kazi na Cristiano Ronaldo.

"Ilikuwa ni vigumu kwangu kumwacha Raul, na maamuzi niliyochukua yalikwenda kinyume na baadhi ya viongozi. Ingawa mchezaji siku zote alielewa.

Cristiano anajali shughuli yake. Anapenda mpira, na pia anapenda vyombo vya habari. Tulikuwa na kundi la wachezaji wazuri, lakini Madrid sio klabu am,bayo iko tayari kwa mipango. Kama ningeendelea mwaka huu tungekuwa tuko vizuri."

Pellegrini pia alisema bado anaendelea kuwa na mahusiano mazuri na Mkuregenzi Mkuu Jorge Valdano na anamatumaini kocha wa sasa Jose Mourinho atapatiwa kila kitu kinahitajika ili afanikiwe.

Aliongeza: "Huwa naongea mara kwa mara na Jorge Valdano, na tuna mahusiano mazuri, sitaki nichambue kazi anayofanya Mourinho, lakini napenda nimtakie kila la heri."

Cesc Fabregas post Manchester City match interview (24/10/2010)

Saturday, October 23, 2010

RORBETO CARLOS: ZIDANE NI MCHEZAJI BORA NILIYEPATA KUMUONA KATIKA MAISHA YANGU.

MADRID, Hispania
BEKI wa zamani wa Real Madrid Roberto Carlos amekiri katika mahojiano yake na gazeti la L'Equipe kuwa Zinedine Zidane ni mchezaji aliyepata kumuona katika maisha yake.

Akijulikana zaidi kwa staili yake ya kwenda kushambulia akitokea nyuma upande wa kushoto na mashuti aliyokuwa akipiga katika mipira ya adhabu (free kicks), Mbrazil huyo alimtaja mchezaji mwenzake huyo kuwa ni bora katika kipindi chake chake cha uchezaji soka na hata baadae, akifafanua kuwa ni bahati kwamba walicheza pamoja katika kikosi cha Madrid.

"Ni mchezaji bora niliyepata kumuona," alisema Rorbeto Carlos. "Ronaldo alimkuwa mzuri, lakini Zizou alikuwa na kitu cha ziada. kucheza pamoja naye ilikuwa ni kitu cha kufurahisha! Mashabiki walikuwa wakiwasili mapema Bernabeu ili kumuona akipasha misuli!"

Zidane alianza kujulikana katika ulimwengu wa soka baada kuonyesha kiwango bora katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Ufaransa 1998 katika mchezo dhidi ya Brazil, ambapo alifunga mabai mawili, na Champions League, wakati alipofunga bao la kukumbukwa na kuisaidia Mdrid kunyakuwa taji la tisa.

Kwa sasa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 38 ni mmoja wa viongozi wa klabu hiyo.

Wednesday, October 20, 2010

ROONEY ATHIBITISHA KUONDOKA OLD TRAFORD.

LONDON, England
MSHAMBULIAJI wa Manchester United Wayne Rooney ametoa taarifa ya kuthibitisha nia yake ya kuondoka Old Traford.

Mchezaji huyo wa zamani wa Everton alielekeza kuwa maamuzi yake yametokana na ukweli kwamba bodi ya klabu hiyo imeshindwa kumuhakikishia kama wanampango wowote wa kununua wachezaji zaidi ili kuboresha kikosi hicho.

"Nilikutana na David Gill wiki iliyopita na hakunihakikishia chochote kuhusu kuboresha kikosi siku zijazo," alisema Rooney.

"Ndio nilipomwambia kuwa sitasaini mkataba mpya."

Rooney pia amekiri kuvutiwa na kushangazwa na kauli ya Sir Alex Ferguson aliyosema Jumanne alipoongea na vyombo vya habari, ambapo Mscotland huyo alisema "ameshtushwa" na 'ameangushwa" na uamuzi aliochukua Rooney (24), lakini atabakia kuwa mchezaji anayempenda .

"Nilivutiwa kumsikiliza kitu gani atasema Ferguson jana na nilishangazwa na baadhi ya vitu alivyosema," aliendelea Ferguson.

"Ni ukweli mtupu aliosema, kuwa wakala wangu na mimi tulifanya mikutano mingi kuhusiana na mkataba mpya. Katika kipindi hicho tulipokutana nilitaka kuhakikishiwa kuhusu mwenendo wa klabu katika kuwavutia wachezaji nyota duniani.

"Sijawahi kuwa na chochote zaidi ya kuiheshimu MUFC. kwanini nisiiheshimu kwani imekuwa na historia ya kipikee na haswa miaka sita iliyopita ambayo nimekuwa na bahati ya kuwa nayo?

"Kwa mimi hakuna kingine zaidi ya kushinda vikombe kama klabu ilivyofanya chini ya Sir Alex. kwasababu ya hilo nadhani swali niliulizwa litakuwa limejibiwa."

RIJKAARD ATUPIWA VIRAGO GALATASARAY.

UONGOZI wa Galatasaray ya Uturuki umeamua kumtupia virago kocha wake Frank Rijkaard baada ya klabu kuanza vibaya ligi ya msimu wa 2010-11.

Taarifa ya katika tovuti ya klabu ilisema kuwa mkataba wa kocha huyo wa zamani wa Barcelona umesitishwa, pamoja na msaidizi wake Johan Neekens naye ameiacha klabu hiyo.

Kwa sasa klabu hiyo inashikilia nafasi ya tisa katia msimamo wa ligi kuu ya nchi hiyo katika mechi nane ilizocheza wakiwa wamejikusanyia pointi 12 mpaka sasa na wakiwa nyuma ya pointi nae dhidi ya vinara wanaoongoza ligi hiyo Bursaspor.

Rijkaard (48) alichukua kibarua cha kuinoa klabu hiyo 2009, lakini alishindwa kuipa mafanikio klabu hiyo kwani walimaliza ligi msimu uliopita wakiwa nafasi ya tatu.

INTER YAPIGA NNE, LYON, MANCHESTER UNITED, BARCELONA NAZO ZAPETA.

MILAN, Italia
TIMU ya Inter Milan jana iliendeleza ubabe katika kundi A baada ya kupata ushindi wa tatu katika kundi hilo kwa kuidhibu bila ya huruma Tottenham Hotspurs kwa mabao 4-3.

Inter ambao katika mchezo wao wa kwanza walifanikiwa kuwafunga Werder Bremen nyumbani kwa mabao 4-0, walifanikiwa kuwadhibiti Spurs katika kipindi cha kwanza ambapo mpaka kinamalizika walikuwa tayari wameshashinda mabao 4-0 mabao yaliyofungwa na Javier Zanetti, Samuel Eto'o na Dejan Stankovic huku mabao ya Tottenham yote yakifungwa na Gareth Bale katika kipindi cha pili na kuifanya timu hiyo iendelee kubaki nafasi ya pili wakiwa wamezidiwa pointi na Inter wanaoongoza kundi hilo na pointi mbili zaidi ya FC Twente na Bremen ambao walitoka sare ya bao 1-1.

Jumanne usiku tulishuhudia FC Bayern Munich, Chelsea, Real Madrid na Arsenal wote wakijizolea pointi katika makundi yao na kufikisha tisa, jana likuwa ni zamu ya Olympique Lyon, ambao walishinda mabao 2-0 dhidi ya Benfica ukiwa ni mchezo wao wa tatu kushinda katika Kundi B, Schalke 04 wanakamata nafasi ya pili baada ya kuifunga timu ambayo haina pointi ya Hapoel Tel Aviv kwa ambao 3-1.

FC Kobenhavn haijapoteza pointi katika kundi D kabla ya jana usiku kwani walipoteza baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 kutoka kwa Barcelona mabao yaliyofungwa na Lionel Messi. FCK inazidiwa na barcelona kwa pointi moja lakini inawazidi kwa pointi tano na nne Rubin Kazan na Panathiniakos baada ya jana timu hizo kutoshana nguvu kwa kutofungana.

Uwezo binafsi uliofanywa na Nani dakika ya saba ulitosha kuifanya Manchester United kuibuka kidedea kwa kuifunga timu ya Bursaspor bao 1-0 katika uwanja wa Old Trafordna kuifanya iongoze kundi D kwa tofauti ya pointi mbili dhidi ya Rangers ambayo ndio inayofuatia baada ya kulazimishwa suluhu na ya bao 1-1 dhidi ya Valencia.

Monday, October 18, 2010

MAJINA YA WATAKAOWANIA TUZO ZA MCHEZAJI BORA AFRIKA KUTANGAZWA NOVEMBA.

CAIRO, Misri
KATIBU MKUU wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Hicham El Amrani amesema kuwa majina ya watakaowania tuzo za mchezaji bora wa shiriki hilo kwa mwaka huu yanatarajiwa kutangazwa katika wiki ya kwanza ya Novemba.

"Orodha yoyote iliyotoka hivi haijatoka kwetu," alisema Amrani. "Tunakwenda kwa mujibu wa ratiba. Tunachukua mashindano yote yaliyofanyika 2010 kuanzia ngazi vilabu na timu za Taifa ikijumuisha michuano ya Mataifa ya Afrika yaliyofanyika Angola na Kombe la Dunia la South Afrika."

El Amrani alisema kuwa tayari majina ambayo yatakuwa yamegawanjika katika sehemu mbili yaani majina ya wachezaji wa mwaka ambao wanacheza Ulaya na majina wachezaji wa mwaka ambao wanacheza katika ligi za hapahapa Afrika yameshawasilishwa katika kamati ya ufundi na maendeleo pamoja kamati ya habari ya CAF kwa ajili ya uhakiki. Kamati hizo zinatarajiwa kufikisha kuchuja majina hayo na kubakia kumi kwa ajili ya tuzo za wachezaji wa nyumbani na matano kwa ajili ya wachezaji wa nje.

Alisema majina hayo yatapunguzwa zaidi na kufikia matatu kila upande, baada ya vyama vya soka 53 vya Afrika watapopiga kura kwa ajili ya uteuzi wa mwisho.

Sherehe hizo zinatarajiwa kufanyika wiki ya tatu ya mwezi Desemba lakini mahala itakapofanyika bado hapajaamuliwa.

EDUARDO: KUVUNJIKA MGUU KULICHANGIA KUPOROMOSHA KIWANGO CHANGU.

SHAKHTAR, Ukraine
MSHAMBULIAJI wa Shakhtar Donetsk Eduardo amesema kuwa kitendo cha kuvunjika mguu kilichangia kutokurudi katika kiwango chake wakati alipokuwa Arsenal.

Eduardo (27) aliumia mwaka 2008 baada ya kuchezewa vibaya na mchezaji wa Birmingham City Martin Taylor. Baada ya kupigania kiwango chake na afya yake, aliruhusiwa kuhamia kwa mabingwa wa Ukraine katika kipindi cha majira ya kiangazi.

Akiongea na Skysports.com, Eduardo alifafanua kuwa anachotilia maanani ni kupata matokeo mazuri Jumanne usiku katika mchezo wao wa Champions League kuliko kuchukuliwa na hisia zangu.

"Sikukusudia kuvunja mguu wangu, lakini ni kweli naweza kusema kuwa tukio lilitia doa soka langu," alisema Eduardo.

"Siwezi kujua ni kitu gani kingenitokea kama nisingeumia, lakini pengine ningeendelea ningekuwa bado katika timu.

"Kama nitacheza nitakuwa na hisia kali, lakini nitajaribu kutilia maanani mchezo huo na nitakuwa nimetulia katika mechi hiyo.

"Shakhtar Donetsk inakuja London kwa utulivu kwa ajili ya mchezo wao mgumu.

"Tumeshinda michezo miwili iliyopita na hatuna wasiwasi. Haitakuwa rahisi, lakini tunataka kuwashangaza."
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia aliongeza: "Nahitaji kukumbukwa kwa kuwa mchezaji mzuri uwanjani na sio mambo yaliyopita wakati niko Arsenal, Ingawa naenda katika mchezo huu nikiwa sina cha kulipiza.

"Mashabiki siku zote wako nyuma yangu na wako katika moyo wangu na bado nawasiliana na Denilson, Cesc Fabrigas na Robin [van Persie]."

MORATTI: KUMSAJILI MESSI NI NGUMU.

MILAN, Italia
RAIS wa Inter Milan Massimo Moratti amelirudia suala la Lionel Messi, lakini akisema kuwa hawezi kuvunja benki kumsajili mchezaji huyo.

"Messi? ni waandishi ndio wanaendelea kulikuza suala lake," alisema Moratti akiliambia gazeti la Sky Sport la Italia.

"Messi ni mchezaji anayehitajiwa na klabu yoyote, lakini nadhani ni zoezi gumu sana.

"Huko mbele? Nani anaweza kujua..."

Moratti alihamishia maongezi hayo ya kuhusiana na na kumsajili Messi, kwa kuelezea ushindi mwembamba waliopata dhidi ya Cagliari Jumapili.

"Nimependa kikosi kilichocheza dhidi ya Cagliari, walionyesha morali ambao huku unahitajika katika mchezi kama hizo," alisema Moratti.

"Sidhani kama tunamtegemea Eto'o, walisema hivyo wakati tuko na Zlatan Ibrahimovic, lakini tumeshinda mataji mawili ya ligi.

Sunday, October 17, 2010

WILSHERE: NILISTAHILI KUTOLEWA.

LONDON, England
KIUNGO wa Arsenal Jack Wilshere amekiri kuwa alistahili kutolewa nje katika mchezo dhidi ya Birmigham Jumamosi lakini ameapa kuwa amejifunza kutokana na kosa hilo.

Kiungo huyo mchezeshaji alisema alikumbwa na dhahama hiyo dakika za majeruhi kabla ya mpira kumalizika katika Uwanja wa Emirates baada kumuinmgilia vibaya mshambuliaji wa Birmingham Nikola Zigic.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye miaka 19 amekuwa mkweli kwa tukio alilofanya.
"Nataka kusema kuwa nilidhamiria kumuingilia kwa nguvu Zigic na nakubali kuwa nilistahili kutolewa nje," alisema Wilshere akiuambia mtandao wa klabu hiyo.

"Sina chochote cha kupinga kuhusu kadi nyekundu niliyopewa na nitajifunza kutokana na hili. Nitakosa mechi tatu sasa kitu ambapo kinanisononesha, lakini nahitaji kusema nilistahili kadi nyekundu."

Wilshere sasa atakosa mechi tatu za nyumba kuanzia mchezo dhidi ya Manchenster City mwishoni mwa wiki inayokuja.

WENGER KUMPA KIBARUA VIERA.

LONDON, England
ARSENE Wenger yuko tayari kumpa kibarua nahodha wa zamani wa Arsenal katika benchi lake la ufundi kama mmoja wa makocha kama nguli huyo atatundika daluga mwishoni mwa msimu huu.

Kiungo huyo anayechezea Manchester City kwa sasa alishakiri kuwa anaweza kutundika daruga zake mwishoni mwa msimu huu na Wenger atajaribu kwa mara ya pili kumchukua mchezaji huyo kama kocha, ilisema taarifa ya gazeti la The People.

Alijaribu kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 34 kama kocha mchezaji katika majira ya kiangazi 2009 lakini kiungo huyo alionekana kuvutiwa zaidi na Manchester City, akiamini kuwa atapata muda kucheza zaidi ili aweze kuitwa katika fainali za Kombe la Dunia 2010.

Hatahivyo Viera hakuweza kuitwa katika kikosi cha Ufaransa na amechezeshwa kidogo tu katika msimu huu huku akianza katika mchezo mmoja tu.

Hili limepelekea kufikia hatua hiyo wiki iliyopita kwamba kipindi chake cha kucheza soka kitakuwa kimefikia tamati.

MANCHESTER, CHELSEA ZANG'ANG'ANIWA, ARSENAL, TOTTENHAM, BOLTON ZAPETA.

MANCHESTER, Uingereza
MANCHESTER United jana iliendelea kuwaduwaza mashabiki wake nyumbani, baada ya kukubali sare ya mabao 2-2 dhidi ya West Bromwich Albion, katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Mchezo huo ambao ulichezwa kwenye uwanja wa Old Trafold ulishuhudia Mashetani Wekundu wakilazimika kupigana kulinda heshima na wageni wao ambao walionyesha soka safi kipindi cha pili.

Hadi kipindi cha kwanza kilipomalizika, Manchester United ndio waliokuwa wakiongoza kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Javier Hernandez na Louis Nani katika dakika za tano na 25 za mchezo.

Hata hivyo, West Bromwich Albion ambao wana rekodi ya kupanda na kushuka katika ligi hiyo walikuja juu na kulisaka lango la wapinzani wao na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya 50.

Mpira huo uliotokana na adhabu iliyopigwa na mlinzi Chris Brunt, ulimgonga Patrice Evra na kujaa kimiani, ukimuacha mlinda mlango Edwin Van Der Sar akichupa bila mafanikio.

Wageni walifanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 55 kupitia kwa mshambuliaji
Somen Tchoyi ambaye alitumia makosa yaliyofanywa na Van Der Sar kuuweka mpira wavuni.

Saturday, October 16, 2010

JOHN W. HENRY: TUTAFANYA KILA TUNALOWEZA KUHAKIKISHA MASHABIKI WANAJIVUNIA KLABU YAO.

LONDON, England
MMILIKI wa kampuni wa New England Sports Venture (NESV) John W. Henry ameeleza hamasa aliyonayo baada ya kuinunua klabu ya Liverpool kwa paundi milioni 300.

Henry (61), ambaye pia anamiliki timu ya Baseball ya Boston Red Sox ya Marekani, alijitokeza wiki iliyopita, ambapo kulikuwa na vita ya kisheria baada ya wamiliki wa zamani wa kimarekani Tom Hicks na George Gillett kutaka kuing'ang'ania klabu hiyo.

"Zimekuwa ni siku za matukio, ya hapa na pale, zilikuwa zinachosha lakini hatimaye tumefanikiwa malengo na matarajio yetu," alisema Henry akiuambia mtandao wa klabu hiyo. "Najivunia timu ya watu ambao wamefanikisha mpango huu.

"Tumefurahi sana. Nikiwaongelea wote ninaoshirikiana nao huko Marekani, wote wamefurahi."
Hatimaye mpango huo ulikamilika rasmi Ijumaa mchana, hatahivyo kwa mujibu wa madai ya kisheria yaliyofunguliwa na Hicks na Gillett, Henry hakuwa na uhakika wa moja kwa moja kwamba kila kitu kitakwenda sawa na alikiri hilo katika kipindi cha mvutano kwamba alikuwa na wasiwasi kwamba NESV itanyimwa nafasi ya kuinunua klabu hiyo.

"Kuna siku nyingi nilikuwa nafikiria kama tutarudi nyumbani au hatutarudi mikono mitupu. Kwa ukweli, hata leo nilikuwa sina uhakika wa asilimia mia moja," alisema Henry.

"Kuna siku ambazo nilikuwa na uhakika lakini kulikuwa na vitu vingi vya hapa na pale hapa. Nilikuwa na watu makini ambao walifanya kazi nzuri ya katika kushughulikia hili na nina furaha limekwisha kwa mafanikio."

Mfanyabiashara huyo mzaliwa wa Illinois alifafanuwa kuwa kufanana kwa klabu hizo mbili ya Boston Red Sox na Liverpool ndiko kulikompelekea kufikia hatua ya kuinunua klabu hiyo ya kihistoria.

"Kuna vitu vingi vinavyofanana na ni kitu aambacho tumekuwa tukikijadili kabla ya kuanza harakati hizi. Tumegundua kuna mengi na mengi yanayofanana kati ya Liverpool 2010 na Red Sox ya 2001 walipoinunua.

"Kwa mfano tatizo la uwanja lilikuwa ni tatizo kubwa Boston mwaka 2001 na tulienda kule tukiwa hatujui la kufanya, kama tujenge uwanja mwingine au kuufanyia matengenezo uliokuwepo. Tuna tatizo kama hilo hapa.

"Tunatakiwa tusikilize, tujifunze, tuongee na jamii ya hapa, tuongee na baraza, tuongee na wanachama, lakini tatizo kubwa kuliko yote ni jinsi gani tutaifanya Liverpool iwe katika kipindi kirefu kijacho."

Kllabu ilipo hivi sasa ndani na nje ya uwanja, limekuwa tatizo na Henry anajua kwamba haitakuwa kazi rahisi kuiridisha timu hiyo kuendeleza ushindi kama ilivyokuwa zamani.

Aliendelea: "Kuna kazi kubwa ya kufanya kuirudisha klabu katika hadhi yake. Kiukweli kutokana na kazi tuliyofanya katika miezi miwili iliyopita, tumeona changamoto na matatizo yalijitokeza, na tutayafanyia kazi ili kuwaonyesha.

"Kuna vitu vikubwa vyenye umuhimu hapa nje na ndani ya uwanja na tunadhani tunaweza kuanzia kutoka hapo, lakini haiwezi kuwa rahisi. Tuna changamoto kubwa."

Wakati mashabiki wa Liverpool wakimkaribisha mmiliki mpya, hawakusita pia kuonyesha wasiwasi wao kwa mmiliki huyo mwingine wa kimarekani.

Kipindi Hicks na Gillet walipoinunua klabu hiyo 2007, ahadi walizotoa wamiliki hao hazikuwahi kutimizwa.

"Ilikuwa ni miaka mitatu migumu na kulikuwa na matarajio makubwa yaliyowekwa, hivyo kitu ambacho sitajaribu kufanya ni kuweka matarajio mengi," alikiri Henry

"Nataka kujenga matumaini kuliko kutimiza ahadi, Nikisema mimi, namaanisha 'New England Sports Ventures (NESV).

"Tuna kampuni yenye nguvu kifedha na vinginevyo tuna malengo mazuri ya kufikirika na tutaanza kuyafanya kazi kuanzi kesho."

"Tunachoweza kusema tutafanya kazi kwa bidii kwa ajili ya mashabiki wa Liverpool kwa kadri tunavyoweza na hatuna mashaka kuhusu hilo, kwani mnastahili," aliendelea Henry akiwaambia mashabiki wa Liverpool.

"Mmekuwa pamoja na klabu hii katika kipindi chote kigumu na tutafanya yote tunaweza kwa uwezo wetu wote kuwafanya mashabiki kujivunia klabu yao pamoja na sisi. Ni cgangamoto kubwa lakini nafikri tuko tayari kukabiliana nayo."

TOURE AWAOMBA WANASIASA NCHINI KWAO KUWA WATULIVU KATIKA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI.

LONDON, England
BEKI wa Manchester City Kolo Toure mzaliwa wa Ivory Coast ametuma ujumbe wa maneno kwa wanasiasa wa nchi yake katika kipindi cha kuelekea uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Octoba 31, kuwaomba kuwa maslahi yao makubwa yawe kwa ajili ya watu wengi.

Katika mahojiano na gazeti la France Football Alhamisi, mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal alisema anatarajia na haswa wanasiasa wa nchi yake siku zote kutoa kipaumbele kwa wananchi wakawaida.
"Bara letu la Afrika linakabiliwa na wakati mgumu hivi sasa. Nchi yangu Ivory Coast inakabiliwa na hekaheka uchaguzi wa Rais Octoba 31," alisema.

"lakini tunahitaji kuwapa watu pumzi ya hewa nzuri, na hilo linatakiwa kuanzia kwa wanasiasa ambao siku zote wana wajibu wa kufukiria uwingi wa watu wa kawaida kuliko kitu chochote. Ni muhimu kufanya hili kwa kizazi kijacho ambao wanatuona kama mifano, ukiwa kama mwanamichezo au mwanasiasa."

Kampeni za Urais zinaanza rasmi Ivory Coast Ijumaa, kampeni ambazo zitadumu kwa muda wa wiki mbili kabla ya uchaguzi wa kihistoria ambao labda unaweza kuliunganisha taifa hilo la Afrika Magharibi baada ya miaka mingi ya machafuko ya kisiasa.

Mchezaji wa Chelsea Didier Drogba, pia kutoka Ivory Coast, naye pia amewaomba wana siasa wa nchi hiyo kusaidia kurudisha amani ambayo ilikuwa imepotea kwa muda mrefu.

"BENDTNER KUANZA KUTUPA RAHA KARIBUNI," - WENGER.

LONDON, England
KOCHA wa Arsenal Arsene Wenger anaamini kuwa wapenzi wa Uwanja wa Emirates hivi karibuni wataanza kumuona Nicklas Bendtner akifanya vitu vyake.

Bendtner (22), bado hajaanza kuonekana katika kikosi cha timu hiyo msimu huu ambapo anauguza maumuvu ya nyonga ambayo anaamini aliyapata baada ya kupata ajali ya gari Septemba mwaka uliopita, na kujitonesha katika Kombe la Dunia Afrika Kusini.

Hatahivyo, mshambuliaji huyo anaweza kuonekana katika kikosi cha timu hiyo kwa mara ya kwanza msimu huu, zaidi akiwa benchi la akiba katika mchezo dhidi ya Bimighham City baadaye, huku akiamini kuwa kuwa mchezaji huyo atakuwa fiti baada ya maumivu ya nyonga yaliyokuwa yakimkabili kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita.

"Tusisahau kuwa toka Novemba mwaka uliopita Nicklas alitusaidia hapa na pale, lakini hakuweza kuonekana kutokana na maumivu," alisema Wenger.

"Tukiachilia ukweli kwamba alikwenda kwenye Kombe la Dunia hatujamuona Bendtner akiwa fiti katika kiwango chake kwa muda mrefu sana.

"Yuko karibu kurudi katika kiwango chake.

"Maumivu ya nyonga yalikuwa ni tatizo kwake, lakini sasa yameondoka."

"SINA MPANGO WA KUHAMA MADRID," - DIARRA.

MADRID, Hispania
KIUNGO wa Real Madrid Lassana Diarra ametupilia mbali tuhuma kwamba anataka kuondoka Bernabeu lakini alisisitiza anataka kucheza mara kwa mara kuliko anavyochezeshwa hivi sasa.

Kuna habari zinazosema kuwa Mfaransa huyo anataka kuwakimbia vigogo hao wa Hispania kwa ajili ya kutafuta timu atakayocheza mara kwa mara, huku Manchester United, Aston Villa na Liverpool ambazo zimeripotiwa kumnyemelea mchezaji huyo mwenye miaka 25.

Hatahivyo, Diarra ameondoa uvumi huo kwa kusema kwamba hana mpango wa kuikacha klabu hiyo na alikaririwa na Sky Sports akisema, "Nina furaha hapa Madrid, lakini nahitaji kucheza. Naamini nitachezeshwa zaidi chini ya kocha wangu huyu mpya ambaye kocha na binadamu mzuri."

Wednesday, October 13, 2010

UEFA YAANZA UCHUNGUZI WA MECHI ILIYOVURUGIKA KATI YA ITALIA NA SERBIA.

SHIRIKISHO la Soka Ulaya (UEFA) limethibitisha kuwa limeunda kamati maalumu ya uchunguzi wa tukio lilitokea jana kati ya Italia na Serbia na kusababisha mchezo huo wa kutafuta tiketi za kufuzu michuano ya Ulaya kuvunjika.

"Kutokana na tukio la jana la mechi baina ya Italia na Serbia katika Uwanja wa Luigi Ferraris, Genoa baada ya dakika sita za mchezo huo zilizochezwa, UEFA imeanza kufanya uchunguzi mara moja kupitia kamati yake ya nidhamu kwa tukio lilishuhudiwa na jana na mazingira yake," ilisema taarifa ya UEFA.

"Mara taarifa itakapokamilika, wakisaidiana na ripoti ya waamuzi na makamisaa, suala hilo litapelekwa kamati ya nidhamu ya UEFA ambao watalipitia na kulitolea maamuzi.

"TULISTAHILI USHINDI TULIOPATA." - CUPERLY.

KOCHA wa timu ya Morocco Dominique Cuperly ameuambia mtandao wa timu hiyo kwamba timu yake ilistahili ushindi wa bao 1-0 iliyoupata dhidi ya Tanzania mwishoni mwa wiki iliyopita Dar es Salaam. Alisema wachezaji wake ndio wanaostahili kupongezwa na pointi tatu walizochukua zinaonyesha ubora wao, haswa baada ya kikosi hicho kupoteza pointi mbili nyumbani katika mchezo wao wa kwanza dhidi ya Afrika ya Kati.

"Ushindi huu unawarudia wachezaji. kwani tumepata kitu tulichokuwa tunakitafuta. Pointi tatu hizi tulizopata ugenini zitakuwa na umuhimu katika mashindano yote. Tutauhifadhi ushindi huu na kuendelea kujiandaa kwa michezo ijayo. Tutacheza michezo miwili ya majaribio ili kukiandaa kikosi chetu na labda tunaweza kuita wachezaji wapya ili kuongeza nguvu," alisema.

Hivi sasa, Cuperly aliongeza kuwa ameridhishwa na mwenendo wa timu hiyo katika ukabaji lakini katika ushambuliaji bado kuna kazi ya kufanya.

"Tuliweza kuzuia vizuri na bao tulilopata lilikuwa zuri. Lile bao lilitokana kwa pamoja na Chamakh na El Hamdaoui. Inabidi tubaki katika kiwango cha juu katika mechi zote za kufuzu na kufanya kazi kwa bidii ili kuwaridhisha mashabiki wetu.

DUNGA AMSIHI NEYMAR KUHAMIA JUVE.

BRASILIA, Brazil
KOCHA wa zamani wa Brazil Dunga amemwambia Neymar kutojiunga na Chelsea na badala yake ajiunge na klabu ya Juventus pindi atapoondoka katika klabu yake ya Santos.

Kinda huyo mwenye miaka 18, kidogo ahamie Stamford Bridge katika kipindi cha majira ya kiangazi lakini vilabu hivyo vilishindwa kukubaliana ada ya uhamisho wa machezaji huyo. Juventus wamekuwa wakimnyemelea mchezaji huyo toka kipindi hicho na Dunga anaamini kuwa ili aweze kuendelea ni bora ahamie Serie A.

"Lazima tuwe na uvumilivu kwa watu wadogo," alikaririwa Dunga na gazeti la Daily Mail.

"Lakini Juventus ni klabu inayojua umuhimu wa kutunza vipaji. Neymar bado mdogo sana lakini tayari ameshaanza kuonekana katika timu ya Taifa."

INTER YAMTAMANI FABRIGAS.

MILAN, Italia
KLABU ya soka ya Inter Milan inataka kuvamia soko la Ligi Kuu ya Uingereza na mchezaji mahiri wa Arsenal Cesc Fabrigas ndio wa kwanza wanayemuhitaji katika kipindi cha dirisha dogo Januari mwakani, alidai Pierpaolo Marino.

Bosi huyo wa zamani wa Napoli amaamini kuwa Inter wa Nerazzuri wataongeza nguvu baada ya kushindwa kutengeneza kikosi imara katika majira ya kiangazi, na wanatarajia kuhamishia nguvu zao kwa Fabrigas.

Tatizo kubwa litakalowakabili ni kuwashawishi Arsenal kummuachia mchezaji huyo. Inter pia itapata upinzani kutoka Barcelona ambayo nayo inammezea mate mchezaji huyo.

"Kama Benitez angewashawishi wakurugenzi kumsikiliza katika kipindi hicho basi wangeweza kufanikiwa katika kipindi cha mwezi August," alisema Morino.

"Fabrigas na Dirk Kuyt wa Liverpool. Kama wataweza kukamilisha taratibu za kuwanyakuwa hawa hakuna yeyote anayeweza kusema katika klabu hiyo kwani wachezaji hao watyakamilisha kikosi kilicho bora kabisa."

Tuesday, October 12, 2010

"ULIKUWA NI UAMUZI MGUMU KUIHAMA BARCA." - TOURE YAYA.

LONDON, England
KIUNGO wa Manchester City Yaya Toure ameeleza nia yake ya kurudi katika klabu yake ya zamani ya Barcelona, baada ya kukiri kuwa kuhama Nou Camp "ni jambo gumu katika maisha yangu".

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast alihamia Eastlands katika kipindi cha majira ya kiangazi kwa ada ya euro milioni 24, ambapo klabu hiyo ilikuwa ikimuhitaji kwa kipindi kirefu msimu uliopita".

Toure (27) alisema wakati akihijiwa na Radio Catalunya kuwa atavaa jezi za mabingwa hao wa Hispania tena, akaongeza kuwa ujio wa Sergio Busquets katika kikosi hicho ndio uliochangia maamuzi yake ya kuondoka.

"Nitarudi Barcelona kucheza, sio kama mtalii. Nahitaji kurudi Barcelona, kwasababu kuondoka kwangu kilikuwa ni kitu kigumu katika maisha yangu. alisema Toure.

"Sergio Busquets ni mtu mzuri, na bila Busquets, nisingeweza kuondoka. Ni mchezaji bora na kitu nilichokuwa nahitaji ni kucheza, na sio kukaa benchi. nimeshinda kila kitu nikiwa na klabu ile na nahitaji changamoto tofauti.

"Kwa mimi, Manchester City ni changamoto nzuri. Hii ni timu ambayo haichezi Champions League, na haitawahi kushinda taji lolote hivi karibuni. Kwa hiyo, naona inanifaa."

Barcelona ilimnyakuwa mchezaji huyo kutoka Monaco kwa ada ya euro milioni 9, na ameitumikia klabu hiyo kwa misimu mitatu ya mafanikio ambapo ameshinda mataji mawili ya ligi na moja la Champions League.

"NAFASI YANGU INAWEZA KUZIBWA," - XAVI.


BARCELONA, Hispania
KIUNGO wa Barcelona Xavi amesisitiza kuwa nafasi yake inaweza kuzibwa katika kikosi hicho na kufafanua kuwa timu yake ya Taifa ya Hispania nayo pia inafuata mfumo huohuo na kutomtegemea mchezaji mmoja.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania ambaye kwa sasa anauguza majerahalakini anatarajiwa kurudi uwanjani mwishoni mwa wiki wakati timu yake itakapocheza dhidi ya Valencia katika Uwanja wa Nou Camp. Akiongea na Barca TV, Xavi alifafanua kuwa ingawa ni mchezaji wa kutegemewa katika kikosi cha Pep Guardiola, haimaanishi kuwa nafasi yake haiwezi kuzibwa.

"Hapana, hapana hapana," alisema Xavi. "Unaweza kuliona hilo siku moja. jinsi tunavyocheza ni sawasawa na haihitaji kitu au mchezaji fulani kuweza kufanyika. Ingawa, kama [Leonel] Messi hayupo huwa tunamkumbuka, kama ilivyo kwa [Andres] Iniesta, [David] Villa au [Carles] Puyol, kwasababu ni wachezaji muhimu, lakini hakuna hata mmoja mmoja wetu ambaye nafasi yake haiwezi kuzibwa."

Xavi (30) pia ameondoa minong'ono iliyopo kuhusu yeye kuwa mchezaji bora wa dunia na anaamini kuwa heshima hiyo anastahili mchezaji mwezake Messi.

"Sidanganyi, kuna mchezaji mmoja ambaye yuko katika nafasi ya juu. Naweza kusema kusema sijawahi kumuona mchezaji kama yeye katika maisha yangu.

"Ni mchezaji wa aina yake kama anavyosema Peps, anacheza sehemu zote, ana kasi, jasiri, nguvu ana kila kitu! Nadhani huwa wanakuwepo kama yeye katika kila miaka 50, kwahiyo ukitaka kuchagua aliye bora basi ni Messi.

"NAIPENDA LIGI KUU UINGEREZA." - MOURINHO.

MADRID, Hispania
BAADA ya kufafanua kuwa rafiki yake mkubwa katika mpira ni kocha Manchester United Sir Alex Ferguson, kocha Real Madrid Jose Mourinho aliwaambia waandishi wa habari sababu zake kwanini anaipenda Uingereza kuliko nchi zingine alizowahi kufundisha.

"Hakuna mahojiano yaliyofanyika bila kunitaja mimi hapa Hispania, fikiria kama najali hili. Bora Uingereza. Nafikiri kuwa Ureno, Italia na Hispania kuna baadhi ya mashabiki huwa wanachagua siku kabla na baada ya mchezo, kuliko mchezo wenyewe," alisema Mourinho.

Mourinho aliwahi kuongea kuhusu mapenzi aliyonayo na Ligi Kuu ya Uingereza wakati akifundisha Inter na ilimfanya kutengeneza uadui kwa baadhi ya waandishi na makocha kwa kuonyesha mapenzi yake na Uingereza.

"Furaha kubwa niliyonayo kuhusu kazi na shughuli yangu ni kuwa imeniwezesha kufundisha Ureno, Uingereza, Italia na sasa Hispania. Inanifanya kuwa kocha tajiri kuliko yule ambaye amefundisha sehemu zinazofanana na utamaduni unaofanana," alimalizia Mourinho.

VIINGILIO SIMBA NA YANGA CCM KIRUMBA HIVI HAPA.

SHIRIKISHO la Soka nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa watadi kati ya timu ya Simba na Yanga mchezo utakaochezwa Octoba 16 katika Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanaendelea ambapo wenyeji wa mchezo huo itakuwa ni klabu ya Simba.

Alisema katika mchezo huo kiingilio cha juu kabisa yaani viti maalumu au VIP kitakuwa ni shilingi 30,000, eneo la jukwaa kuu kiingilio kitakuwa shilingi 20,000 wakati kiingilio cha chini kitakuwa shilingi 5,000 upande wa mzunguko.

Alisema wamefikia hatua ya kuweka viwango vya chini ili kila mkazi wa Mwanza aweze kumudu kwenda kupata burudani ambayo muda mrefu walikuwa hawajaipata ya kushuhudia timu zao zikipambana katika uwanja huo.

Monday, October 11, 2010

MATOKEO YA MECHI MBALIMBALI ZA KUFUZU MICHUANO YA MATAIFA YA AFRIKA.

YAFUATAYO hapo chini ni matokeo pamoja na tarehe ya michezo mbalimbali liyochezwa ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika yanayoandaliwa kwa pamoja na Gabon na Equatorial Guinea 2012.

Kundi A


10/10/10 Zimbabwe 0-0 Cap Vert

Kundi B

10/10/10 Madagascar 0-1 Ethiopia
10/10/10 Guinea 1-0 Nigeria

Kundi C

10/10/10 Libya 1-0 Zambia
09/10/10 Comoros 0-1 Mozambique

Kundi D

9/10/10 Tanzania 0-1 Morocco
10/10/10 Central Africa 2-0 Algeria

Kundi E

9/10/10-18:30 Senegal 7-0 Mauritius
9/10/10 Cameroon 1-1 RD Congo

Kundi F

9/10/10-18:00 Burkina Faso 3-1 Gambia

Kundi G

10/10/10 Niger 1-0 Egypt
10/10/10 Sierra Leone 0-0 South Africa

Kundi H

09/10/10 Rwanda 0-3 Benin
09/10/10 Burundi 0-1 Côte d’Ivoire

Kundi I

10/10/10 Congo 3-1 Swaziland
10/10/10-17:00 Ghana 0-0 Sudan

Kundi J

09/10/10 Kenya 0-0 Uganda
09/10/10 Angola 1-0 Guinea Bissau

Kundi K

09/10/10 Malawi 6-2 Tchad
10/10/10 Togo 1-2 Tunisia
09/10/10 Mali 2-1 Liberia

"SIWEZI KUWA KAMA FERGUSON AU RIJKAARD," - LARSSON.

LANDSKRONA, Sweden
MCHEZAJI nyota wa Zamani wa Sweden, Celtic, Barcelona na Manchester United Henril Larsson ambaye siku zote alikuwa akidai kazi ya ukocha haimvutii baada ya kuacha kucheza mpira, lakini sasa mshambuliaji huyo wa zamani ameonyesha kufurahia nafasi yake ya ukocha katika klabu ya Landskrona.

"Ni kweli nilikuwa sitaki kuwa kocha kabisa, lakini wakati umri ukiwa mkubwa unagundua kuwa ni vizuri kuliko ulivyokuwa ukifikiri mwanzoni. Unaona picha yote kwa usahihi kuliko ulivyokuwa ukiona ulivyokuwa mdogo na napenda mpira," alisema Larsson akiuambia mtandao wa fifa.com.

"Kuwa kocha ni maamuzi magumu mwishini. Na nafurahia. Kuna kipindi kizuri na kibaya na inaweza kukuchanganya, lakini pia nilikuwa nikichanganyikiwa kipindi fulani nilipokuwa nacheza."

Larsson amefanya kazi na makocha wengi katika kipindi chake cha uchezaji, lakini hakuna kocha hata mmoja ambaye anafanana na jinsi Larsson anavyofundisha.

"Nikuwa na bahati sana kucheza chini ya makocha wengi wazuri na kitu kitu ambacho nimekuwa nikifanya ni kudokoa machache kutoka kwa wote hao walionifundisha ambayo yanaweza kunisaidia. Katika mpira hakuna jipya, ni vitu vinavyoendelea kwa miaka mingi, hivyo siwezi kusema nitafanya kitu ambacho hakijawahi kufanywa hapo kabla.

"Kitu unachoweza kufanya ni kuwa mwenyewe. Hata nikijaribu, siwezi kuwa kama [Sir Alex] Ferguson, siwezi kuwa kama [Martin] O'Neil na siwezi kuwa kama [Frank] Rijkaard. nataka niwe mimi mwenyewe, na wa aina ya peke yangu, na hicho ndicho nachojaribu kufanya."

"CRISTIANO NI BORA DUNIANI," - MOURINHO.

MADRID, Hispania
KOCHA wa Real Madrid Jose Mourinho amejibu maswali ya watu kuhusu ni mchezaji gani anayeona ni bora duniani, na kumchagua mchezaji wake Cristiano Ronaldo kuwa namba moja.

Bosi huyo Mreno alikuwa akihijiwa na Telemadrid kuhusu maendeleo ya mpango kwa klabu hiyo, na mawazo yake ya nani anamuona ni mchezaji bora kati ya Messi na Ronaldo.

Akiwalinganisha wote wawili, Mourinho alijibu, "Kuna machaguo mawili - Cristiano, and Messi. Kama ukimchagua Cristiano kuwa namba moja, basi Messi atakuwa wa pili. Lakini kwangu mimi Cristiano ni namba moja."

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea pia alisema kama kuna kitu chochote ambacho angependa kushinda katika msimu huu, angependa zaidi kuwa kocha wa kwanza kutetea ubingwa wa Champions League katika msimu huu baada ya kulichukua akiwa na Inter msimu uliopita.

"Champions League ni shindano la mashindano. Ni muhimu zaidi na makubwa kutokana na ubora wake.

"Sitaki nionekane kama mjinga, lakini nahitaji ubingwa wa Champions League kwa huu kwa sababu nahitaji kutetea ubingwa wangu, lakini pia kupeleka ubingwa huo Real Madrid ambapo unatakiwa uwe."

"KIMOMBO KINANIPA SHIDA." RAMIRES.

LONDON, England
MCHEZAJI mpya wa Chelsea Ramires amekiri kuwa tatizo kubwa linalomkumba kwasasa ni lugha ya Kiingereza.

Ramires (23), alisajiliwa kutoka Benfica katika msimu wa majira ya kiangazi na alianza katika mchezo wa wiki iliypita dhidi ya Arsenal ambapo timu hiyo ilishinda mabao 2-0. Baada kuhamia katika nchi ambazo zinaongea lugha ya kireno ambayo ndio lugha ya nyumbani, kiungo huyo alisema kuwa mawasiliano na wachezaji wenzake yalikuwa tatizo kubwa na wachezaji wenzake katika miezi ya mwanzo alipotua Stamford Bridge.

Akiongea na gazeti la Daily Star, Mbrazil huyo alisema: "Bado sijaweza kabisa lakini najaribu. Jambo kubwa gumu linalonikabili ni lugha.

"Wakati mwingine unahitaji kuongea na mtu unakuwa huwezi au huelewi lakini nadhani nitaweza baadae."

PH: VIDEO: Top 10 misses of the 2010/2011 season so far

PH: VIDEO: Top 10 misses of the 2010/2011 season so far - Goal.com

Friday, October 8, 2010

BRAZIL YAIADHIBU IRAN.

ABU DHABI, Falme za Kiarabu
DANIEL Alves, Alexandre Pato na Nilmar, juzi waliifungia Brazil mabao matatu katika mchezo wa kihistoria dhidi ya Iran ambapo kigogo hicho kilishinda 3-0.
 
Mchezo huo uliokuwa maalumu kwa ajili ya maonyesho, ulimpa raha kocha mpya wa Brazil,
Mano Menezes ukiwa ni ushindi wake wa pili mfululizo tangu alipochukuwa nafasi ya Carlos Dunga.
 
Dunga, nahodha wa zamani wa Brazil, alitupiwa virago muda mfupi baada ya kutolewa katika fainali za Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini.
 
Alves alianza kufunga bao dakika 14 kwa mpira wa adhabu kabla ya Pato kuongeza dakika 69. Nilmar alifunga bao la tatu dakika mbili kabla ya mchezo kumalizika.
 
Brazil itavaana na Ukraine Jumatatu ijayo katika mchezo wa kirafiki utakaopigwa mjini Derby, England, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya michuano ya Kombe la Amerika majira ya kiangazi.

APPIAH ATAMANI KUINOA GHANA.

ACCRA, Ghana
NAHODHA wa zamani wa Ghana, 'Black Stars', Stephen Appiah amesema anataka kuifundisha
timu ya taifa ya nchi hiyo baada ya kustaafu soka.
 
Kauli ya kiungo huyo wa kimataifa aliyewahi kung'ara na klabu za Ulaya, imekuja muda mfupi baada ya kustaafu kuitumikia Black Stars.
 
"Nina kiu ya kuinoa Ghana baada ya kustaafu soka, lakini sasa naelekeza nguvu katika klabu yangu ya Cesena. Tutaona siku za usoni nini kitatokea," alisema Appiah.
 
Kiungo huyo alidai siyo lazima kuinoa timu ya wakubwa lakini pia atakuwa radhi kuanza nafasi ya kocha msaidizi au yoyote atakayopewa na Shirikisho la Soka Ghana (GFF) muda wake ukifika.
 
Appiah (29), alisisitiza kamwe hatarejea kucheza soka ya kimataifa baada ya kutundika daluga Agosti, mwaka huu na kuongeza kuwa ameridhika kuiongoza Ghana katika fainali mbili za Kombe la Dunia.
 
Alisema amefikia uamuzi huo ili kutoa nafasi kwa wachezaji chipukizi kuitumikia Ghana katika michuano mbalimbali.
 
Baadhi ya wachezaji nguli waliowahi kuvuma na kikosi cha Black Stars ni Abedi Pele, Tony Yeboah, Gargo Mohammed, Osei Kufuor, Augustine Arhinful na Yaw Preko.

FERDINAND ROHO JUU.

LONDON, England
RIO Ferdinand siyo tu anahaha kulinda nafasi yake ya unahodha, lakini pia anapasua kichwa kuhakikisha anapata namba kikosi cha kwanza cha England.
 
Maumivu ya goti yamemuweka nguli huyo katika hali ngumu baada ya kukosa fainali za Kombe la Dunia 2010. Nafasi yake ilichukuliwa na msaidizi wake Steven Gerrard.
 
Nahodha huyo wa Liverpool, alisema atakuwa radhi kurudisha kitambaa cha unahodha kwa Ferdinand baada ya kupona.
 
Ferdinand amerejea uwanjani kwa kishindo baada ya kupona majeraha ya goti na tayari ameanza kuingiwa hofu ya kupokwa namba na kinda wa Everton, Phil Jagielka aliyecheza mechi mbili za kufuzu fainali za Kombe la Ulaya.
 
Jagielka alisimama 'mkoba' katika mechi ambazo England ilishinda mabao 4-0 dhidi ya Bulgaria kabla ya kuifumua Uswis mabao 3-1. Fabio Capello anaweza kumtumia chipukizi huyo katika mchezo wa Jumanne ijayo dhidi ya Montenegro.
 
Jagielka alikuwa mchezaji pekee aliyecheza dakikika zote 90 katika mechi hizo. Licha ya kurejea uwanjani, Capello ana hofu kama mkongwe huyo (31) yupo katika kiwango bora kwa ajili ya mechi za kufuzu Kombe la Ulaya.

BOSI MTARAJIWA LIVER KUKUTANA NA TORRES.

LONDON, England
MMILIKI mtarajiwa wa klabu ya Liverpool, John Henry amepanga kukutana uso kwa uso na mshambuliaji wa timu hiyo Fernando Torres.
 
Bilionea huyo anayemiliki klabu ya mchezo wa 'baseball' ya Red Sox huenda akawa bosi mpya wa Liverpool wiki ijao. Henry anataka kuinunua klabu hiyo ingawa anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mmiliki Tom Hicks.
 
Hicks amepeleka pingamizi mahakamani akipinga Liverpool kuuzwa kwa pauni milioni 300 (sh. bilioni 690), lakini Henry anayeungwa mkono na kundi la wachezaji anapewa nafasi kubwa kutua Anfield.
 
Henry amepanga kukutana na Torres haraka kuzungumzia mustakabali wake baada ya nyota huyo kuwa katika hali ngumu kufuatia majeraha ya korodani yanayomuandama muda mrefu tangu msimu uliopita.
 
Torres anatarajiwa kurejea uwanjani katika mchezo ambao Liverpool itavaana na Everton katika mchezo wa ligi uliopangwa kuchezwa kesho. Liverpool ipo nafasi ya 18 katika katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi sita.

Thursday, October 7, 2010

MASHABIKI WA TUNISIA JELA MISRI.

CAIRO, Misri
MASHABIKI wa soka 11 raia wa Tunisia wamefungwa jela baada ya kutokea vurugu katika mchezo ambao Esperance ilichapwa mabao 2-1 ilipovaana na Al Ahly ya Misri.
 
Katika mchezo huo wa nusu fainali kuwania Kombe la Orange, mashabiki wa Esperance walipata hasira baada ya mechi hiyo kumalizika ambapo walidai mabao ya Al Ahly hayakuwa halali.
 
Jaji wa mahakama wa jiji la Cairo, aliwahukumu jela mashabiki 11 kwa madai ya kufanya fujo baada ya pambano hilo kumalizika. Ilidaiwa mashabiki wa Tunisia walipigana na askari wa Cairo.
 
Polisi wa Cairo walishindwa kudhibiti hasira za mashabiki wa Tunisia ambao walipinga uamuzi katika mchezo huo. Hali ya uwanja ilikuwa mbaya zaidi kabla ya maofisa usalama kuingilia kati kuokoa jahazi.
 
Mashabiki wenye hasira waliwavamia polisi na kutoa kipigo. Polisi 11 walikimbizwa hospitali kwa ajili ya matibabu kabla ya kuruhusiwa. Mashabiki wawili wa Tunisia walipandishwa ndege kurudishwa nyumbani.
 
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) linafanya uchunguzi wa kuhusiana na tukio hilo ambalo litajadiliwa na Kamati ya Maadili kabla ya kutolewa uamuzi baada ya kupitia kwa kina vielelezo.

WACHEZAJI CAMEROON, KONGO KUPEWA CHANJO YA KIPINDUPINDU.

YAOUNDE, Cameroon
WACHEZAJI wa Cameroon na Kongo watapewa chanjo za kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu kabla ya timu hizo kuvaana kesho katika mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa Afrika 2012.
 
Mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka, unatarajiwa kuchezwa Kaskazini mwa Cameroon katika mji wa Garoua, uliokumbwa na maambukizi ya ugonjwa huo hatari kwa miezi kadhaa.
 
Chama cha Soka Cameroon (FA) kilisema kikosi cha Cameroon kiliwasili Garoua Jumanne iliyopita kiliondoka Jumatano asubuhi kwenye Hoteli ya Benoue na jana walipatiwa vidonge vya kuzuia maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu.
 
"Tuliambiwa na Wizara ya Afya hali ya ugonjwa wa kipindupindu ni kubwa, lakini tupo makini sana tumechukua tahadhari kwa wachezaji wote kupimwa na watakuwa sehemu moja maalumu kabla ya Jumamosi kucheza mchezo huo," alisema mmoja wa madaktari wa Cameroon.
 
Kwa mujibu wa FA, wachezaji wa Kongo watahusika na utaratibu huo. Kocha wa timu ya taifa ya Kongo, Robert Nouzaret alitaka mchezo huo uhamishwe kutoka jiji la Yaounde kwenda Garoua ombi ambalo lilikubaliwa.

SHEVCHENKO KUTIMIZA MECHI YA 100 UKRAINE.

NYOTA wa zamani wa klabu ya AC Milan na Chelsea Andriy Shevchenko anatarajiwa kuwa mchezaji wa kwanza wa Ukraine kucheza mechi 100 wakati timu hiyo itakapocheza na Canada, Ijumaa.

Mshambuliaji huyo alianza kuichezea timu hiyo miaka 15 iliyopita katika mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu michuano ya Ulaya 1996 dhidi ya Croatia na mchezaji huyo mzoefu bado hapendi kukumbuka mechi hiyo. Hatahivyo na hayo Chevchenko anazo kumbukumbu nyingi za kukumbukwa na timu hiyo.

Hakuna kitu kibaya kama tulivyofungwa mabao 4-0. Nataka nikumbuke mambo mazuri na nashukuru kwamba yapo mengi katika miaka 16 niliyochea timu hiyo," alikaririwa Chevchenko na tovuti ya uefa.com.

"Kampeni zetu za Kombe la Dunia mwaka 2006 bado ziko nazikumbuka, haswa pale Ukraine ilipopoteza michezo yake mitatu katika hatua za mwanzo katika kutafuta nafasi ya kuvuzu. Nakumbuka mchezo wetu dhidi ya Uturuki wakati mashabiki wa nyumbani walipotuzomea haya mambo huwa yanakatisha tamaa.

"Tulichemka kwenda katika Kombe la Dunia lililopita lakini sasa tunajiandaa na michuano ya Ulaya 2012 tukiwa na nguvu za ziada. Naamini nitakuwa fiti kwenye michuano hiyo na nitatumia nguvu zangu zote pamoja na uzoefu nilionao kuhakikisha timu inafanikiwa hapa nyumbani. kwasasa nitakosa baadhi ya mechi za kufuvu, hatahivyo tunawapa umuhimu marafiki zetu na tunajaribu kucheza kwa kiwango bora.

"Kufikisha michezo 100 ni safari ndefu, hata kwa wale, kama mimi, ambao huwa hawafuatilii mambo ya uwiano."

"HATUMTEGEMEI XAVI," - MARCHENA.

MADRID, Hispania
MCHEZAJI wa kimataifa wa Hispania Carlos Marchena amesisitiza kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo hakimtegemei kiungo mchezeshaji wa timu hiyo Xavi, wakati wakijiandaa kucheza na Lithuania na Scotland bila nyota huyo wa Barcelona.

Beki huyo mzoefu ambaye alikuwemo katika kikosi hicho wakati kilipobeba Kombe la Ulaya 2008 pamoja na Kombe la Dunia 2010, anaamini kuwa kuna wachezaji wengi ambao wanaweza kuziba pengo la mchezaji huyo wa katikati.

"Ni matarajio yetu kuwa hatutamtegemea mchezaji huyo. Ni mchezaji mzuri lakini wako wengine pia ambao wanaweza kucheza nafasi yake na wako tayari kuchukua nafasi yake," alisema Marchena.

"Ni lazima tuendeleze ushindi na kucheza mchezo wa kuvutia. Soka ndivyo lilivyo huwa inatokea, mnapoteza mchezo muda mwingine. Tunachotakiwa ni kugundua makosa yetu na kuhakikisha hayajirudii tena."

"NITAUA MTU." - FERGUSON.

LONDON, England
SIR Alex Ferguson amewaambia wachezaji wake 'ataua' mtu endapo mwenendo wao utakuwa wa kusuasua katika Ligi Kuu England msimu huu.
 
Kocha huyo mwenye msimamo, alitoa kauli hiyo juzi usiku akidai haridhishwi na kiwango cha United na ameonya mchezaji yeyote atakayezembea atakiona cha moto.
 
Ferguson alisema ni upuuzi United kuvuna pointi 13 katika mechi saba ilizocheza na kuwaacha wapinzani wake wakubwa Chelsea kukalia kiti cha uongozi kwa pointi 18.
 
Alisema hatakubali kuona upuuzi huo ukiendelea na amechukizwa baada ya kikosi hicho kutoka sare mara manne katika mechi saba. "Katika mchezo na Fulham tulikosa penalti kizembe, tulipocheza na Everton walipata mabao mawili dakika za majeruhi, sitakubali upuuzi huu tena," alisema Ferguson.
 
Kocha huyo alikiri safu ya ulinzi ina tatizo kulinganisha na ushambuliaji na alitaka mabeki kuongeza kasi. Ngome ya United inaundwa na nahodha Gary Neville, Rafael de Silva, Patrice Evra, Nemanja Vidic na Rio Ferdinand aliyekuwa nje ya uwanja muda mrefu akiuguza goti.
 
Ferguson aliwataka vijana wake kuiga mfano wa Chelsea ambayo ilianza vizuri ligi kwa kupata ushindi mnono mfululizo. Tangu kuanza msimu huu, timu hiyo ya Stamford Bridge imekuwa na kiwango bora.

Wednesday, October 6, 2010

RAIS TOGO AJIUZULU.

LOME, Togo
RAIS wa muda wa Shirikisho la Soka Togo (TFF), Seyi Memene amejiuzulu kufuatia Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kukataa ombi la bodi ya uchaguzi kutaka kuahirisha uchaguzi kwa wiki mbili.
 
Waziri wa Michezo wa Togo, Christophe Tchao alisema, Memene aliandika barua ya kujiuzulu nafasi hiyo Septemba 30. Kiongozi huyo wa zamani yupo Paris, Ufaransa alipopelekwa kwa ajili ya kuchunguzwa ugonjwa ambao haufahamiki.
 
Memene alitaka uchaguzi huo ufanyika Oktoba 16. Shirikisho la Soka Togo, lilikumbwa na kashfa ya kuipeleka timu ya taifa 'feki' kucheza na Bahrain, mkanganyiko huo ulisababisha maofisa wawili Antoine Folly na Doucoure Mamadou kuadhibiwa.
 
Folly kabla ya kuteuliwa mjumbe wa kamati ya maadili, alikuwa Waziri wa Michezo wa Togo na Mamadou alikuwa msaidizi maalumu wa rais wa Shirikisho hilo. "Nimepokea kopi ya barua ya kujiuzulu kutoka kwa Memene kwasababu anataka kufanyiwa upasuaji mjini Paris," alisema Tchao.
 
Bodi hiyo sasa imebakiwa na wajumbe sita wa bodi walioteuliwa kwa muda, baada ya jaji Sogoyou Powele na mwanasheria, Akakpo Martial kubwaga manyanga.
 
Timu ya taifa ya Togo ilipandikizwa majina 'feki' ya wachezaji ilichapwa mabao 3-0 na Bahrain kwenye Uwanja wa Riffa. Shirikisho hilo na Wizara ya Michezo, iliibuka na kudai timu hiyo haikupewa baraka ya kuiwakilisha nchi katika mechi hiyo. Kocha wa zamani wa Togo,Tchanile Bana aliyefungiwa, adhabu yake inaweza kuongezeka.

Mc CLAREN ATAJWA KUMRITHI CAPELLO.

LONDON, England
KOCHA wa zamani wa England, Steve Mc Claren, anatajwa kuwa ndiye mrithi wa Fabio Capello baada ya mkataba wa Mtaliano huyo kumalizika 2012.
 
Capello, ameweka bayana hataongeza mkataba baada ya kumalizika fainali za Kombe la Ulaya 2012.
 
England ilianza vizuri kampeni ya kufuzu fainali hizo kwa kuzichapa Bulgaria mabao 3-1 kabla ya kuifumua Uswis 4-0.
 
Mc Claren alishindwa kuipeleka England katika fainali za Kombe la Ulaya 2008, lakini Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Chama cha Soka England (FA), Trevor Brooking  alisema kocha huyo anastahili kutwaa nafasi ya Capello.
 
"Nina uhakika kama Steve ataendelea kupata mafanikio jina lake litarejea kuinoa England. Tumejifunza mengi, tumepata uzoefu wa kutosha, hatuwezi kumdharau kila mtu nadhani litakuwa siyo jambo zuri," alisema Brooking.
 
McClaren (49), alitupiwa virago England mwaka 2007 lakini nyota yake iling'aa baada ya kutua FC Twente ambapo aliipa ubingwa wa Ligi Kuu Uholanzi kabla ya kutimkia Ujerumani kujiunga na Wolfsburg miezi mitano iliyopita.
 
Baadhi ya makocha wanaopewa nafasi kuifundisha England ni Harry Redknapp, Sam Allardyce na Roy Hodgson. FA imeweka msimamo kuwa inataka mrithi wa Capello awe raia wa England.

"FERGI ANANITAKA UNITED," - BELLAMY.

LONDON, England
MSHAMBULIAJI mtukutu, Craig Bellamy, amesema kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson alimtupia ndoano kabla ya kutua Cardiff kwa mkopo Agosti, mwaka huu.
 
Mchezaji huyo wa Manchester City, alidokeza Roberto Mancini alimuwekea ngumu kuhamia Old Trafford kutokana na chuki binafsi. Bellay alisema kocha huyo hakupenda kumwona akijiunga na klabu kubwa kabla ya kumsukumia Cardiff kwa mkopo.
 
Nahodha huyo wa Wales, alisema baada ya kutokea mzozo kati yake na Mancini, alitaka kujiunga United baada ya Ferguson kumtaka lakini Mancini aligoma. Bellamy, alisema hakupenda kutua Tottenham Hotspurs kwasababu zilizokuwa nje ya uwezo wake kati ya klabu hizo.
 
"Maisha Manchester City yalikuwa magumu sana, kila kitu kilikuwa kigumu. Manchester United ilinitaka lakini klabu yangu iliweka ngumu na kunisukumia Cardiff haraka sana. Sikuwa na tatizo la kufanya mazoezi mara mbili kwa siku haikuwa tatizo, lakini mzozo wangu na Mancini ulianza baada ya kukosoa baadhi ya mbinu zake" alisema Bellamy.
 
Mkongwe huyo aliibua mzozo na Mancini muda mfupi baada ya kutua Eastaland kuchukuwa nafasi ya Mark Hughes aliyefukuzwa. Nguli huyo alitupiwa virago Liverpool kutokana na tabia ya ukorofi. Bellamy anatajwa mmoja wa washambuliaji wenye vipaji vya kufunga mabao.

VIGOGO WA LIVERPOOL WATOFAUTIANA.

LONDON, England
KLABU ya Liverpool imekumbwa na mpasuko mkubwa baada ya bodi ya wakurugenzi kutofautiana kuhusu ofa iliyowekwa mezani na mmiliki wa timu ya 'baseball' Boston Sox, John Henry.
 
Mkanganyiko huo ulitokea juzi usiku baada ya wamiliki wa Liverpool, Tom Hicks na George Gillett kujarabu kutaka kuwafukuza kazi Mkurugenzi Mtendaji, Christian Purslow na Mkurugenzi wa Fedha, Ian Ayre na nafasi zao kutaka kujazwa na raia wa Wamerakani.
 
Mzozo huo ulitokea muda mfupi baada ya ofa kuwekwa mezani, mbali ya Henry, bilionea mwingine kutoka Asia alijitokeza kutaka kuinunua klabu hiyo lakini siyo Kenny Huang raia wa China aliyejitoa mapema.
 
Mwenyekiti, Martin Broughton alitumia kura ya veto kuwalinda, Purslow na Ayre ambao walitakiwa kuondoka Anfield na nafasi zao kuchukuliwa na Mack Hicks, mtoto wa Tom Hicks na Lori Kay McCutcheon.
 
Purslow na Broughton wanapinga Hicks na Gillett kuwa wasemaji wa mwisho wa kutoa uamuzi kwenye bodi ya wakurugenzi kuhusu mchakato wa malipo katika benki ya Royal Bank ya Scotland ambapo wamekopa. Vigogo hao wanataka uamuzi wa mwisho ufanywe na wakurugenzi watano.
 
Hicks na Gillett walitangaza kuiuza Liverpool pauni milioni 800 kabla ya kupunguza bei hadi kufikia pauni milioni 600. Mzozo huo, umeibuka wakati klabu hiyo inadaiwa pauni milioni 237 na benki ya Royal ya Scotland. Matukio hayo, yamekuja siku chake baada ya Liverpool kutupwa nje na timu ya daraja la pili Northampton katika michuano ya Kombe la Carling.
 
Jumapili iliyopita, Liverpool ilichapwa mabao 2-1 na timu iliyopanda daraja la pili na kusababisha mashabiki wenye hasira kutaka Roy Hodgson atimuliwe na nafasi yake kujazwa na kocha wa zamani wa kikosi hicho, Kenny Dalglish.

Tuesday, October 5, 2010

VIINGILIO VYA STARS NA MOROCCO HIVI HAPA.

SHIRIKISHO la soka nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mechi baina ya timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars" na timu ya Taifa ya Morocco mchezo unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Florian Kaijage alisema katika mchezo huo kiingilio cha juu kwenye viti vya VIP A kitakuwa sh. 30,000, viti vya VIP B sh. 20,000 na viti vya VIP C sh. 15,000.

Kaijage alivitaja viingilio vingine ni sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya Bluu, viti vya rangi ya kijani sh. 7,000, wakati viti vya rangi ya machungwa nyuma ya magoli na mkabala na jukwaa kuu sh. 10,000.

Alisema tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zimepangwa kuanza kuuzwa kesho kwenye vituo mbalimbali, Dar es Salaam kuanzia saa 4.30 asubuhi.

"Viingilio hivyo vimepangwa kulingana na mahitaji ya kila mshabiki wa soka, ili aweze kufika uwanjani na kutoa mchango wake kwa kuishangilia Stars ili hatimaye iibuke na ushindi na kuzoa pointi zote tatu," alisema Kaijage.

Wakati huo huo Kaijage alisema Morocco wanatarajiwa kutua leo usiku kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), tayari kwa kuivaa Stars Jumamosi.

Mechi hiyo ya pili kwa Stars ya kusaka tiketi ya kucheza fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika, ambazo zimepangwa kuchezwa 2012, zitaandaliwa kwa pamoja na nchi za Gabon na Equatorial Guinea.

Kaijage alisema msafara wa timu hiyo utaundwa na watu 40 ambapo watakuwemo wachezaji, viongozi, makocha wa kikosi hicho pamoja na waandishi wa Habari 15.

"Wageni wetu (Morocco) wanatarajiwa kuwasili kesho usiku (leo), saa 4.30 usiku kwa kutumia ndege za Shirikka la Ndege la KLM. Baada ya kupokewa watapelekwa kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempisky," alisema Kaijage.
 
Kaijage alisema pambano hilo litachezeshwa na waamuzi kutoka Mauritius, ambapo alimtaja mwamuzi wa kati ni Sochurn Rajir ambaye atasaidiwa na waamuzi wasaidizi, Bootun Balkrishna na Vaay Vivian wakati mwamuzi wa akiba Mohammad Imteaz.

Alisema waamuzi hao na kamishna wa mchezo huo, Mohammed Aziz kutoka Kenya, alisema wanatarajia kuwasili nchini kesho usiku.

Kaijage akizungumzia maandalizi ya Stars chini ya kocha wake, Jan Poulsen, alisema maandalizi yanaendelea vizuri ikiwa ni pamoja na kuwasili kambini kwa wachezaji wote wakiwemo wanaocheza soka ya kulipwa nje ya nchi.

"Idadi yote ya wachezaji 22 wa Stars ambayo imesalia baada ya kuondolewa kikosi Mussa Hassan 'Mgosi', tayari wamesharipoti kambini na wameanza mazoezi. Hivyo tunasubiri tu programu za mwisho za kocha Poulsen kabla ya kuivaa Morocco," alisema.

Mbali ya Morocco na Stars kwenye kundi D, pia ziko timu zingine za taifa za Algeria na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

"WAAMUZI LAZIMA WATULINDE," - NASRI.

LONDON, England
MUDA mfupi baada ya Hatem Ben Arfa wa Newcastle United kuvujika mguu, kiungo wa Arsenal, Samir Nasri amewajia waamuzi wa mchezo wa soka England kuwapa ulinzi mkali.
 
Arfa alivunjika mguu baada ya kuchezewa rafu mbaya na mchezaji wa Manchester City, Mholanzi, Nigel de Jong mchezo walioshinda mabao 2-1 Jumapili iliyopita, lakini mwamuzi Martin Atkinson hakumpa adhabu.
 
Mchezaji huyo alitolewa nje kwa machela na hatacheza mechi zilizobaki msimu huu. Nasri alisema De Jong alidhamiria kumchezea rafu Arfa na kuonya kuwa endapo hatua kali hazitachukuliwa mchezo wa soka utaingia dosari nchini humo.
 
Katika hatua nyingine, kocha wa timu ya taifa ya Uholanzi, Bert van Marwijk, amemtema de Jong katika kikosi chake katika mechi ya kufuzu Kombe la Ulaya 2012.
 
Kocha huyo alisema amechukua uamuzi huo kwa madai mchezaji huyo alicheza rafu ya makusudi. " Muda mfupi baada ya rafu ile nilizungumza naye, nilimwambia umecheza mbaya ya makusudi, hakuwa na sababu ya kufanya vile," alisema Marwijk.
 
Mchezaji huyo anakumbukwa na mashabiki wa soka baada ya kumrukia mguu wa kifua kiungo wa Hispania, Xabi Alonso katika mechi ya fainali ya Kombe la Dunia 2010. Hispania ilishinda bao 1-0.

TORRES NJE KIKOSI CHA HISPANIA.

MADRID, Hispania
MSHAMBULIAJI, Fernando Torres ametemwa timu ya taifa ya Hispania inayojiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Ulaya 2012 dhidi ya Lithunia na Scotland.
 
Torres, mfungaji mabao wa Liverpool amekuwa akiandwa na majeraha ya mguu tangu msimu uliopita. Katika mchezo uliopita, Torres alitoka dakika 10 wakati mchezo ukiendelea ambapo timu hiyo ilipochapwa mabao 2-1 na kibonde Blackpool Jumapili iliyopita.
 
Baada ya kutoka, Torres alikwenda moja kwa moja kwenye vyumba vya kuvalia nguo kabla ya kufuatwa na kocha, Roy Hodgson huku akionekana kuugulia maumivu ya korodani.
 
" Ana maumivu ya korodani, lakini sifahamu ana maumivu kiasi gani. Madaktari wanaendelea kumfanyia uchunguzi wa kina ili kubaini ukubwa wa tatizo lake, tatizo lake lilitushangaza wengi kwasababu lilimtokea mapema kabisa ya mchezo" alisema Hodgson.
 
Kocha huyo alidokeza kuwa awali hawakufahamu kama mchezaji huyo anakabiliwa na maumivu ya korodani na hajui nini kilitokea kwa madai Torres alikuwa na kiwango bora kabla ya kuanza mchezo huo. Mshambuliaji huyo alifanyiwa vipimo vya mionzi kubaini ukubwa wa tatizo.

MAN UNITED YAMNYEMELEA LINDEGAARD.

LONDON, England
MANCHESTER United inakaribia kumnasa mrithi wa kipa mkongwe, Edwin van der Sar, Anders Lindegaard baada ya kocha, Eric Steele kumchunguza katika mechi tano alizokaa langoni ikiwemo ya Jumapili iliyopita.
 
Kocha huyo wa makipa, alikwenda Norway kufuatilia kiwango cha Lindegaard wakati timu yake Aalesunds ilipochapwa mabao 2-1 na Stabaeck, lakini mchezaji huyo mwenye miaka 26, alionyesha kiwango bora.
 
Steele pia alikwenda Hispania kuangalia kiwango cha kipa wa Atletico Madrid, David de Gea lakini kocha huyo alionekana kuvutiwa na kiwango cha Lindegaard. United tayari imeanza kumzungumzo na Aalesunds kuangalia uwezekano wa kumsajili kinda huyo anayewindwa na klabu za Liverpool, Arsenal na AC Milan.
 
United inaendelea kufuatilia kiwango cha Lindegaard kabla ya kufikia uamuzi wa kumsajili msimu wa dirisha dogo, Januari, mwakani ili kuchukua mikoba ya mkongwe Van der Sar ambaye mkataba wake unafikia ukingoni mwakani.
 
Mbali ya mchezaji huyo, United inamuwinda beki wa Uruguay, Bruno Montelongo. Mchezaji huyo mwenye miaka 23, anacheza kwa mkopo katika klabu ya AC Milan akitokea River Plate. Timu hiyo imepanga kumtupia ndoano Montelongo ili kusaidiana na Rafael da Silva baada ya nahodha, Gary Neville kustaafu soka mwakani.